Mawakili wanaosimamia kesi ya Mbowe wana uwezo mdogo

Kumbuka jaji aliyetoa hukumu katika shauri dogo amepandishwa hivi karibuni cheo na kuwa Jaji Kiongozi. Uamuzi wa kumpa cheo kipya katika kipindi anaelekea kutoa uamuzi hauwezi kukwepa hisia za uwepo wa "undue influence" kutoka kwa mamlaka iliyomteua.

Lakini tukiachana na hisia hizo zenye kufikirisha, ni vyema tukaelewa uwepo wa mamlaka kuu iliyokuwa juu ya watu wote. Mamlaka hii kuu alitajwa na Yesu Kristo alipokuwa mbele ya kiti cha hukumu cha Ponsio Pilato akituhumiwa kwa kosa la uhaini.

Kristo alimwambia Pilato kwa uwazi kabisa kuwa asingeweza kuwa na mamlaka hayo aliyokuwa nayo pasipo kuwa na kibali kutoka mbinguni. Pilato aliweka pamba masikioni licha ya kutambua ubatili wa mashitaka yaliyoletwa mbele yake, naye alitoa hukumu ili kutetea maslahi yake na pia ili kuwafurahisha wana wa Israel.

Uamuzi huo ulikuwa na gharama zake, kwani ulipelekea taifa la Israel kuja kusambaratishwa na Warumi. Wakati viongozi wa Kiyahudi walipoteza hadhi yao, Pilato naye alikuja kuishia kujinyonga kutokana na misukosuko ya maisha.

Wenye mamlaka na wapate kusikia ya kwamba haki huliinua taifa. Wakishupaza shingo zao nao pia huadhibiwa. Wana na binti za Mungu wakianza kupaza sauti na kutoa vilio vya uchungu kutokana na uonevu na dhuluma, basi naye hasiti kutoa hukumu yake ya haki.

Ole wenu enyi wenye madaraka ya kidunia. Shoka lipo juu ya shingo zenu zilizoshupaa. Hatutaki kuona bendera zikipepea nusu mlingoti kutokana na hukumu iliyotoka mbinguni ili kubatilisha matendo yenu maovu.
 
Jiwe alishaharibu Mihimili mingine ikiwemo huu wa Mahakama. Hakimu/Jaji wote hao hulitewa hukumu mezani kazi yao ni kuisoma tu. Jiwe aliwajaza watu wasiojulikana kwenye Mihimili hizo ili aweze kuwacontrol. Itachukuwa miaka mingi kuirejesha Mahakama kwenye misingi yake.
 
Yote kwa yote
Mawakili wameonesha uwezo mdogo sana kupitia mapingamizi waliyokuwa wanaweka na maswali wanayouliza
 
Ni punguani peke yake ndiye anaweza kuamini kuwa Tanzania kuna mahakama au mifumo ya kutenda haki.

Jaji alitoa maamuzi kwa kutumia maoni yake binafsi badala ya kutumia vifungu vya sheria pamoja na kurejea kesi za nyuma halafu wewe unakuja hapa na uzi kama huu.Nikikuita kuwa wewe ni punguani nitakuwa nimekuonea?
 
Acha ujinga kama unaakili timamu nendavkwenye space ya jana ya maria then msikilize vyema adv d.matata na fatma karume hapo ndipo utajiona kiazi mbatata.
 
Kila mwenye akili timamu ameona kabisa rafu alizofanya Mh Rais yaani anampa ujaji mtu wakati akiwa anaendesha keao nyeti hasa baada ya kuona mzani umelala kwao na kila kitu kilikua wazi...kiufupi imefanyika hila ya wazi.
Kwa akili zako finyu mtu kama anasifa zote za kupanda cheo basi asipandishwe kwa sababu anaongoza kesi ya Mbowe?
 
Mawakili wa Mbowe ingekuwa kwenye mpira wa miguu tungesema wanacheza na jukwaa

Kuhusiana na Upande wa Utetezi Mawasilisho yaliandikwa na John Malya

Jaji: Kwamba Maelezo yalichukuliwa Siku ya tarehe 07 ambapo Masaa Manne yalikuwa yameshapita

Kuhusiana na Mazingira yaliyowekwa na Sheria kifungu cha 50 kwamba Mahakama inapaswa kingatia Masaa Manne na kuyaondoa yale ya kusafirisha Watuhumiwa

Jaji: Moshi palikuwa na Nyenzo zote ambazo zingeweza kuwezeha Maelezo kuchukuliwa

Kuhusiana na Mateso, Wakili Malya anasema Mateso siyo lazima yawe ya kimwili, Bali Fikra na utu.

Au Mateso yanayotweza Utu wa Mtu

Jaji: Wakili Mallya akaturejesha Kwenye katiba pia

Na Pia akaturejesha Kwenye Tamko la Umoja wa Mataifa linalozingatia Mateso na Utu wa Mwanadamu.

Wakili Malya ametutaka Mahakama tuzingatie Nyaraka hizo.

Jaji: Wakili Mallya ametupa kesi za Marejesho
 
Wanasheria wako Kenya

Ndio maana kesi zote muhimu hurushwa mubashara luningani.
 
CCM acheni kuingilia uhuru wa mahakama, hii mnafanya ni dhambi kubwa mno yaani sasa mmepitiliza kiwango. Sasa mtafanya hata huyo Jaji mpya atakayepangwa afanye kazi kwa shinikizo kubwa kuwaridhisha nyie huku nako wananchi wote tukifuatilia kwa karibu - nawashauri kama mmeamua kumfunga Mbowe basi fanyeni kesi hii iwe ya SIRI.

Yale maamuzi hata wa darasa la nne la mkoloni anajua fika kwamba ilikuwa ni mipango.
 
Maamuzi ya kimahakama yanaambatana na rejea ya vifungu vya kisheria au kesi zilizokwisha kufanyiwa maamuzi, Je kwenye maamuzi ya Hilo so shauri dogo hayo yameonekana?
Huyu bwana kwa jinsi tu alivyoandika, Anaonekana kuwa ana uelewa mdogo.
 
Mbona povu linakutoka hivyo? Halafu kauli zako zina viashiria vya kigaidi gaidi. Tunakufuatilia na likitokea lolote kati ya uliyotabiri basi nawe tutakuhesabu kuwa ni mmoja kati yao.
 
Fafanua wapi Kibatala na squad yake wamekosea.Maana UMESEMA Wana UWEZO mdogo. Hebuelezea. Maana white KESI tumeisikiliza mwanzo mwisho. Hata asiyesomea SHERIA anaona wapi mwelekeo. Swali kwako wapi Mawakili WA MBOWE waliko teleza?
 
Mbona povu linakutoka hivyo? Halafu kauli zako zina viashiria vya kigaidi gaidi. Tunakufuatilia na likitokea lolote kati ya uliyotabiri basi nawe tutakuhesabu kuwa ni mmoja kati yao.
Yamekuwa hayo tena .Kweli UWEZO unao. Mfanyizie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…