Wakuu,
Ni wazi shairi Mbowe si gaidi maana tulitegemea ushahidi utolewe Mahakamani na kesi iishe mapema tu.
Hawa Mawakili wakiongozwa na Peter Kibatala wamekuwa wakihoji mambo madogo kabisa yasiyokuwa na msingi wowote katika kesi hii.
Walituaminisha iko kidubwana kinachoitwa PGO kinaenda kumaliza hii kesi ndogo kumbe imechelewesha kesi yenye msingi.
Wamekuwa wakihoji maswali ya vyakula na vinywaji kama vile mo energy mara nani alilipia nk
Lakini pia waliigomea Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Jinai kwamba haina hadhi ya kujudge kesi hii ya Mbowe, yaani hata hili kweli walikuwa hawalijui?
Walishauri Mbowe agomee yule Jaji wa kwanza na akajitoa kusikiliza kesi hiyo, sasa hata huyu aliyeanza kuisikiliza amejiengua.
Kwa mwenendo wa Mawakili hawa naiona hii kesi inaenda kuishia kubaya kwani uwezo wao ni mdogo kulinganisha na kesi hii.
Ushahidi hujengwa na hivyo vitu unavyoviita 'vidogo vidogo' na vinapounganishwa vinatoa picha kamili ya tukio. By the way, ukimaliza ku'recharge' simu yako hakikisha unaharibu vocha iliyobaki, usitupe. Kama umezoea kutupa baada ya ku'recharge' ikitokea uhalifu ukatokea mfano sehemu uliyonunua, vocha zilizotumika nazo huwa zinaokokwa kwenye upelelezi na unaweza kujikuta ukaunganishwa kwenye kesi usiyoijua, isipokuwa kilichotokea ni kwamba polisi walikuta vocha zilizotumika na wakachukulia kwamba ni moja ya watu waliofanya uhalifu. Hata mimi nilikuwa na mazoea hayo, na tangu nipate somo hilo kutoka kwa askari nikimaliza ku'recharge' naharibu vocha iliyotumika. Sasa wewe unaweza kuona ni kitu kidogo, lakini ndivyo ushahidi unavyojengwa na vitu vyote vidogo na vikubwa. Actually, kwenye ushahidi hakuna vitu vidogo vidogo au vikubwa, bali vyote ni ama vidogo ama vikubwa.
Ni vema Tundu Lissu arejee kuisimamia ili kumnusuru Mwenyekiti.