Wakuu,
Ni wazi shairi Mbowe si gaidi maana tulitegemea ushahidi utolewe Mahakamani na kesi iishe mapema tu.
Hawa Mawakili wakiongozwa na Peter Kibatala wamekuwa wakihoji mambo madogo kabisa yasiyokuwa na msingi wowote katika kesi hii.
Walituaminisha iko kidubwana kinachoitwa PGO kinaenda kumaliza hii kesi ndogo kumbe imechelewesha kesi yenye msingi.
Wamekuwa wakihoji maswali ya vyakula na vinywaji kama vile mo energy mara nani alilipia nk
Lakini pia waliigomea Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Jinai kwamba haina hadhi ya kujudge kesi hii ya Mbowe, yaani hata hili kweli walikuwa hawalijui?
Walishauri Mbowe agomee yule Jaji wa kwanza na akajitoa kusikiliza kesi hiyo, sasa hata huyu aliyeanza kuisikiliza amejiengua.
Kwa mwenendo wa Mawakili hawa naiona hii kesi inaenda kuishia kubaya kwani uwezo wao ni mdogo kulinganisha na kesi hii.
Ni vema Tundu Lissu arejee kuisimamia ili kumnusuru Mwenyekiti.
Hukumu hupaswa kuzingatia ushahidi usioacha shaka na kifungu husika cha sheria.
Jaji Siyani katumia ushahidi pekee wa upande wa mashtaka bila kuonyesha kwanini ushahidi huo ni wa kweli.
Jaji Siyani katupilia mbali ushahidi wote wa upande wa utetezi bila kuonyesha kwanini ushahidi huo si wa kweli.
Detention register ya Moshi ilihitijika angalau Jaji kuweza kusema yaliyosemwa na upande wa mashtaka yangeweza kuwa kweli.
Tathmini ya daktari kwa washitakiwa ilikuwa muhimu japo kwa Jaji kujiridhisha tu kuwa hawakuwa wameteswa.
Kwani Jaji Siyani ni malaika wa kujua ushahidi upi ni kweli na upi ni uongo kwa kusikiliza tu wakati majumuisho ya upande wa utetezi na yale ya mashtaka yanakinzana 100%.
Haina shaka kuwa ya Jaji Siyani ni visingizio tu vya kufikia hitimisho lile lile ambalo angelifikia hata kama wakili wa utetezi angekuwa Mungu!
Mawakili wa utetezi wako vizuri:
1. Hawakuwa na haja ya kuhitaji detention register ya Moshi kuthibitisha kuwa Adamoo aliandikisha maelezo baada ya masaa 4 kupita tokea kukamatwa Moshi.
--> Hili ni wazi hata kwa mtoto mdogo anajua kuwa maelezo yalichukuliwa nje ya muda.
2. Hawakuwa na haja ya kuikataa detention register ya Central ili kuonyesha Adamoo aliteswa huku Jaji akiyaona makovu kwa macho juu ya ushahidi wa mashahidi kuhusu kuteswa.
-->Hili hata mtoto mdogo anajua washitakiwa waliteswa.
Mengine wakuu ni utopolo mtupu.