informer 06
Senior Member
- May 11, 2024
- 184
- 170
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari amesema kuwa katika jitihada za kukuza umahili wa Mawakili wa Serikali nchini kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo usuluhishi wa migogoro na uandishi wa Sheria amesema kwamba Ofisi yake imeandaa mafunzo ya siku tano ambayo yatawaleta pamoja Mawakili zaidi ya 300 ambao watanolewa na wataalamu wa Sheria kutoka ndani na nje kupitia mijadala.
Akizungumzia mafunzo hayo leo Machi 19, 2025 ,Hamza S.Johari amesema kwamba mafunzo hayo yatafanyika Mkoani Arusha, kuanzia Machi 24-28, 2025 na kwamba tayari maandalizi yamefikia hatua nzuri.
Amesema kwamba wataalamu ambao watapewa fursa ya kuchokoza mada watajikita katika masuala mbalimbali, ikiwemo kujadili nasuala ya usuluhishi wa migogoro, Uandishi wa Sheria, mchakato mzima wa utungaji wa Sheria, jukumu la Mawakili katika kulinda uzalendo na maslahi ya Taifa, kujadili masuala ya hati fungani pamoja na hatari zinazoweza kuwakumba.
"Moja ya mkakati wa kuhakikisha tunaboresha na kuimarisha uwezo wetu kama Mawakili wa Serikali katika maeneo mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yetu, kwahiyo mwaka jana (2024) tulikuwa na mafunzo mahususi ambayo tuliyafanya pale Dodoma na tulikuwa na mada mbalimbali tulizojadili" amesema Mwanasheria Mkuu
View: https://youtu.be/JxawwtfoFow?si=J3wWe2ZXQ05dSYMT
Ameongeza"Mwaka huu tutakwenda Arusha, na Mawakili wote wa Serikali tunawaalika na mwitikio ni mzuri, ambapo kwa kipindi cha siku tano kuanzia tarehe 24-25 / 3/ 2025 tutakuwa tunafanya mafunzo. Mafunzo hayo yataendeshwa na Wanasheria wabobezi wa ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mada tofauti"
Aidha ameeleza tija ambazo wanatarajia kuzipata kwenye mafunzo hayo, ambapo ameweka wazi kuwa wanalenga kuongeza umahili zaidi wa masuala mbalimbali ya kisheria ili kuendana na mabadiliko mbalimbali ya kisheria yanayofanyika ndani na nje.
Amesema kwamba inapotokea Wanasheria wakawa na umahili inawaweka katika nafasi nzuri ya kutekeleza vyema majukumu ya kisheria hususani masuala ya mikataba na usuluhishi wa migogoro pamoja na uandishi wa Sheria.
Lakini ameedelea kutoa wito na msisitizo kwa Mawakili wa Serikali kuendelea kujisajili ili kupata fursa ya kuongeza umahili ambao utaenda kuwaongezea tija kwenye utendaji wao.