Mawakili zaidi ya 390 wa Tanzania Bara Hatarini Kupoteza Uwakili wao

Mawakili zaidi ya 390 wa Tanzania Bara Hatarini Kupoteza Uwakili wao

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
778
Reaction score
1,592

Je, kuwa na Shahada ya Sheria na kufanya kazi kwenye mazingira ya sheria ni sawa na kuwa na mafunzo maalumu yanayomwandaa mtu kuwa Wakili?

Hili ni moja ya maswali makubwa ambayo mimi na wenzangu wengine wanne katika shauri hili tumeamua kulipeleka mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

Tarehe 30 Julai 2026, tuliwasilisha shauri la kikatiba kuhusu namna kifungu cha 16(2) cha Sheria ya Mawakili kinavyotumika kutoa msamaha (exemption) kwa baadhi ya watu kutopitia mafunzo ya kitaaluma ya Law School of Tanzania.

Mbali na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Msajili wa Mahakama Kuu, Council for Legal Education, Tanganyika Law Society na Law School of Tanzania, shauri hili linawahusu pia Mawakili 399 walioapishwa chini ya utaratibu huo katika vipindi vya Desemba 2025 na Julai 2026.

Miongoni mwa maombi yetu ni kwamba, endapo Mahakama itakubaliana na hoja zetu, uapishwaji wa Mawakili hao chini ya utaratibu huo utangazwe kuwa kinyume cha Katiba na majina yao yaondolewe kwenye orodha rasmi ya Mawakili (Roll of Advocates).
​

Lakini kwa nini tumeona ni muhimu kulipeleka jambo hili Mahakamani?

Kwa sababu kuwa na LL.B. si mwisho wa safari ya kuwa Wakili, mtu anaweza kusoma Shahada ya Sheria na akapata LL.B, lakini kusoma sheria si kitu kilekile na kufundishwa jinsi ya kuwa Wakili ndiyo maana kuna Law School of Tanzania.

Law School haipo kwa ajili ya kumpa mtu cheti kingine tu cha kuweka kwenye CV.

Mafunzo yake yanalenga kumfundisha mtu mambo ya kutumia sheria kwa vitendo, namna ya kufanya kazi ya uwakili, maadili ya kazi hiyo na namna ya kujiendesha kama mtaalamu wa sheria.

Kwa mfano, mwanafunzi hafundishwi sheria kwa kusoma vitabu pekee. Anafundishwa pia jinsi ya kutumia sheria katika kazi halisi ya uwakili.

Ndiyo maana kuna mafunzo kwa vitendo, mitihani na mfumo wa kuangalia kama mwanafunzi amefikia kiwango kinachohitajika kabla ya kuwa Wakili.

Mfano rahisi

Fikiria mtu amesoma udaktari, akaanza kufanya kazi hospitalini kwa miaka kadhaa.

Je, kwa sababu tu amefanya kazi hospitalini, basi automatically anaweza kuwa daktari? Na je, kwasababu hiyo haitaji tena mafunzo na mitihani ya kitaaluma inayohitajika ili kuwa daktari?

Kwa mtazamo wetu ni HAPANA.

Kwa sababu kufanya kazi hospitalini si sawa na kuthibitishwa kitaaluma kuwa daktari.

Vivyo hivyo katika sheria.

Mtu anaweza kuwa na shahada ya sheria, anaweza kuwa amefanya kazi Mahakamani, anaweza kuwa amefanya kazi Serikalini, anaweza kuwa na uzoefu wa miaka mingi.


Lakini bado swali ni Je, uzoefu huo umehakikiwa na mfumo wa kitaaluma na kuthibitishwa kuwa unalingana na mafunzo na mitihani inayotakiwa kwa mtu anayetaka kuwa Wakili?

Hapo ndipo suala hili lilipo.

Uwakili si cheo tu. Ni mamlaka.

Mtu anapokuwa Wakili, haongezi tu neno “Adv.” mbele ya jina lake.

Anapewa mamlaka ya kumwakilisha mtu Mahakamani.

Anaweza kumwakilisha mtu anayekabiliwa na kifungo.

Anaweza kupigania mali ya mtu.

Anaweza kuandaa na kusimamia kesi.

Anaweza kutoa ushauri wa kisheria ambao unaweza kuathiri maisha, biashara, mali na haki za mtu.

Kwa hiyo, tunapoamua nani apewe mamlaka hayo, hatupaswi kujiuliza kama tu ana shahada ya sheria, tunapaswa pia kujiuliza ameandaliwa kiasi gani kufanya kazi hiyo?”

Shahada ya sheria ni msingi.

Lakini professional training ndiyo inayomsaidia mtu kutumia msingi huo katika kazi halisi ya uwakili.

Kwahiyo, kama mfumo wa kawaida unasema:

Shahada ya sheria → Law School → Mafunzo kwa Vitendo → Mitihani → Uwakili

kwa nini mtu mwingine awe:

Shahada ya Sheria → Masamaha → Uwakili

Bila kuwepo na uwazi wa:​
  • Ni mafunzo gani mengine amepitia?​
  • Ni mtihani gani amefanya?​
  • Ni uzoefu gani umehesabiwa?​
  • Ni kiwango gani kimepimwa?​
  • Nani amethibitisha kwamba uzoefu huo ni sawa na mafunzo anayopata mtu Law School?​
Hili ndilo swali la msingi.

Kwa sababu kama mtu anaomba asipitie njia ya kawaida, lazima kuwe na sababu inayoeleweka na njia ya kuthibitisha kwamba kile ambacho Law School inalenga kuhakikisha kimepatikana kwa njia nyingine.

Hiyo ndiyo tunaita professional equivalence.

Kwa lugha rahisi ni kama mtu hatakiwi kupita njia ya kawaida, tunahitaji kujua ni kwa nini, na ni kitu gani kinachothibitisha kwamba bado amefikia kiwango kilekile.

Na hapa ndipo Katiba inaingia

Katika shauri letu, tunadai kwamba utekelezaji wa kifungu cha 16(2) umefanyika bila kuwepo kwa vigezo vya wazi vya kisheria vinavyoeleza nani anastahili exemption na bila kuwa na safeguards zinazoeleza namna mamlaka hayo yanapaswa kutumika.

Pia tumeonyesha kwamba kwa muda mrefu mialiko ya kuomba exemption imekuwa ikielekezwa zaidi kwa Maafisa wa Mahakama na Watumishi wa Umma wenye Shahada ya Sheria., wakati watu wenye sifa sawa. waliokuwa nje ya makundi hayo hawakuwahi kupata msamaha huo.

Kwa hiyo tunajiuliza:

Kama wote wana shahada ya sheria, kwanini mmoja apewe nafasi ya msamaha na mwingine asipewe?

Na kama kuna tofauti, msingi wa tofauti hiyo ni upi?
Je, umeandikwa kwenye sheria?
Je, kila mtu anaweza kuujua?
Je, unaweza kutumika kwa usawa?

Haya ni maswali ya usawa mbele ya sheria, haki sawa na utawala wa sheria.

Hili si suala la nani atakuwa Wakili tu.

Taaluma ya sheria ina nafasi kubwa katika mfumo wa haki.

Mawakili ndio wanaowakilisha wananchi Mahakamani.

Na watu wanaoingia kwenye taaluma ya uwakili wanaweza baadaye kushika majukumu mengine makubwa katika mfumo wa utoaji haki kama uhakimu na ujaji.

kwahiyo kukubali mawakili ambao kwa maelezo ya jaji mkuu ni kwamba wanaandaliwa kuwa mahakimu, basi inamaana tumeamua kukubali kuwa na waamuaji wa haki ambao hawajapitia mafunzo maalumu ya utohaji haki hiyo, na hiyo ndio hatari kubwa zaidi kwa taifa.

Kwahiyo suala hili si la wivu zidi ya mawakili hao, bali ni suala la kulinda ubora wa mfumo wa utoaji haki.

Kwa sababu mtu anayemsaidia mtu mwingine kutafuta haki lazima mwenyewe awe ameandaliwa vizuri kuelewa jinsi haki hiyo inavyotafutwa na kutetewa.

Ndiyo maana tumeenda Mahakamani

Hatukuenda Mahakamani kwa sababu tunadhani sisi ni bora kuliko wengine.

Hatukuenda kwa sababu tunajutia kupitia Law School.

Na hatukuenda kutafuta huruma.

Tulienda kwa sababu tunaamini kwamba taaluma ya sheria haiwezi kuwa na njia mbili za kuingia kwenye taaluma hiyo bila kuwepo kwa sababu ya wazi, vigezo vya kisheria na mfumo wa kuhakikisha kwamba kiwango cha taaluma hakishushwi.

Kama mtu anapaswa kusamehewa kwenda Law School, basi inapaswa ifahamikr ni kwa nini anasamehewa, kwa vigezo gani ?

Na ni kwa namna gani tumethibitisha kwamba kiwango ambacho Law School inalenga kukihakikisha hakijapungua?

Hilo ndilo tunalotaka Mahakama ilijibu.

HATA HIVYO, SHAURI BADO LINAENDELEA

Shauri lilitajwa kwa mara ya kwanza tarehe 6 Agosti 2026 mbele ya Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu masijala kuu Dodoma, na litakuja tena kutajwa kwa mara ya pili tarehe 24/08/2026 kwa njia ya kimtandao.

Kwa sasa hakuna hukumu iliyotolewa kuhusu kama utekelezaji wa kifungu cha 16(2) ni kinyume cha Katiba au la, wala hakuna uamuzi wa mwisho kuhusu hatima ya Mawakili hao 399.

Tunachofanya ni kuiomba Mahakama itoe mwelekeo kuhusu mipaka ya msamaha huo, usawa mbele ya sheria, Rule of Law na viwango vya kitaaluma katika kuingia kwenye taaluma ya uwakili.

Kwa sababu mwisho wa siku issue si nani anataka kuwa Wakili? Bali ni, tunataka aina gani ya Wakili katika mfumo wetu wa haki?

d8effe52-de03-41f9-b23d-8eb054b23fa7.jpeg

7cc2ba4d-3a47-4573-a67e-f30e0529e99d.jpeg
73bf28ef-a250-43a0-b590-44a48b33aab7.jpeg

88c54670-a9bd-42b1-87e0-0774897f6aa2.jpeg

7209cd10-9a1f-45b7-84f9-57235bafc28b.jpeg

7a33a8ca-6e3d-4295-9f1d-46237a6401e4.jpeg

c6e063f3-3e33-470d-b4b0-65c1a64833e4.jpeg

7a1e19ec-6ea2-4b52-9782-ed48ef1c1736.jpeg

80bdadf8-25f3-46d8-b43d-8ece218fe384.jpeg

38b84b1a-c5e0-4e2b-908c-e80cd6c3ed14.jpeg
 
Mawakili wa exemption wawekewe vidoti vyeusi kwenye paji la uso..............kama issue ni experience kwanini wasitumie huo uzoefu kufaulu law school? Kwanini hoja ya uzoefu haitumiki kwa watu waliopo private sectors, huku kwenye private practice kuna watu ni Senior Legal Officer amekaa
firm miaka 15 lakini hapati msamaha anaenda kupewa karani ambae ana mwaka mmoja kazini na kazi yake kubwa kuwapa tarehe wadaawa.

Worse enough goli likatanuliwa zikaanza kutolewa exemption Hadi kwa watu ambao daily activity zao hazi involve active practice mfano exemption zimetolewa hadi kwa Watendaji wa Kata, Waandishi wa Vikao, maafisa usajili RITA & other agencies yaan kigezo kikawa ni check namba ya kada yoyote na LL.B lakini mtu wa private sector ambae kwa nature ya kazi anazofanya ni active ananyimwa exemption.
Hata tangazo tu la exemption linatolewa kama internal memo kuwa encourage kundi flani kuomba na kupewa.

Binafsi exemption ingekuwa inatolewa kwa legal officer wenye uzoefu kwenye ofisi kama OSG nisingekuwa na swali coz wanafanya mpk appearance

Mbona hatuoni msamaha wa kupata CPAs & alike?
The issue ni kwamba kama kuna exemption viwekwe vigezo vilivyo wazi ni viwe wazi kwa wote wa private na public sector waone kama kuna mtu ataenda kwenye hiyo Shule yao.
 
Mawakili wa exemption wawekewe vidoti vyeusi kwenye paji la uso..............kama issue ni experience kwanini wasitumie huo uzoefu kufaulu law school? Kwanini hoja ya uzoefu haitumiki kwa watu waliopo private sectors, huku kwenye private practice kuna watu ni Senior Legal Officer amekaa
firm miaka 15 lakini hapati msamaha anaenda kupewa karani ambae ana mwaka mmoja kazini na kazi yake kubwa kuwapa tarehe wadaawa.

Worse enough goli likatanuliwa zikaanza kutolewa exemption Hadi kwa watu ambao daily activity zao hazi involve active practice mfano exemption zimetolewa hadi kwa Watendaji wa Kata, Waandishi wa Vikao, maafisa usajili RITA & other agencies yaan kigezo kikawa ni check namba ya kada yoyote na LL.B lakini mtu wa private sector ambae kwa nature ya kazi anazofanya ni active ananyimwa exemption.
Hata tangazo tu la exemption linatolewa kama internal memo kuwa encourage kundi flani kuomba na kupewa.

Binafsi exemption ingekuwa inatolewa kwa legal officer wenye uzoefu kwenye ofisi kama OSG nisingekuwa na swali coz wanafanya mpk appearance

Mbona hatuoni msamaha wa kupata CPAs & alike?
The issue ni kwamba kama kuna exemption viwekwe vigezo vilivyo wazi ni viwe wazi kwa wote wa private na public sector waone kama kuna mtu ataenda kwenye hiyo Shule yao.
Unahoja, usikilizwe.
 
Naomba kuuliza maswali mepesi haya.

1. Kwa utaratibu wa sasa ili mtu awe wakili inahitaji vigezo gani?
2. Hiyo Shule ya Sheria ilianzishwa kwa malengo gani?
Utaratibu ni kwamba
1. Awe na shahada ya sheria
2. Akasome na afaulu mitihani ya Law school
3. Awe na cheti kutoka Law school

Law school ilianzishwa kwa malengo ya kufundisha sheria kwa vitendo na kuandaa mawakili
 
Back
Top Bottom