Naibu waziri wa Afya Aisha kigoda amezima minongono ya muda mrefu ,baada ya kuamua kuweka wazi Bungeni kuwa waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano mhe Seif khatib ndiye barafu wa moyo wake
mambo yalikuwa hivi
Mwenyekiti wa Bunge mh job Ndugai alimwita naibu waziri, Dr kigoda kuchangia kwa dakika 20 kabla ya waziri wake prof mwakyusa kupewa nafasi ya kuhitimisha hoja hiyo
Baada ya kusimama, Dr kigoda alianza kumshukuru Rais jk kwa kumwamini na kumteua kushikilia wadhifa alionao, alimshukuru bosi wake profesor mwakysa kwa ushirikiano anaompa kazini pia akawashukuru wafanyakazi wnzake
Naibu waziri huyo akamalizia kwa kumshukuru mpenzi wake Mhe Seif khatib ndiye barafu wa moyo wake