carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Wanadiplomasia wakuu wa nchi tatu za Ulaya watafanya mazungumzo mjini Istanbul na wenzao wa Uturuki, Saudi Arabia, Pakistan na Misri. Mkutano huo utajadili hali nchini Yemen, Ukanda wa Gaza na mzozo nchini Iran.
Nchi saba zinakutana kwa mara ya kwanza chini ya mfumo wa E3 unaoundwa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, na kundi jipya la R4, chanzo hicho kilisema, wakati vita vinavyohusisha Iran, Yemen na Ukraine vikiendelea kutishia njia muhimu za usafirishaji wa baharini na usalama wa kikanda.
Mawaziri hao wanatarajiwa kujadili suala la isarel na palestina hali ya hivi karibuni katika Mlango wa Hormuz, mambo yalivyo katika mapigano yanayoihusisha Yemen, juhudi za kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine, pamoja na fursa za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za kikanda na za Ulaya.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Fidan anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa kupata suluhisho la kidiplomasia katika vita kati ya marekani na Irani
Pia atasisitizia tena uungwaji mkono wa Uturuki kwenye suala la usalama wa Saudi Arabia kufuatia mashambulizi ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen, chini ya Mkataba wa Pamoja wa Ulinzi wa Makka, uliosainiwa na Uturuki, Pakistan na Saudi Arabia.
Chanzo : Dw swahili