Wakuu kwa muda sasa kumekuwa na speculation nyingi za uongo hapa forum, kuhusiana na reshuffle ya cabinet, kwa hiyo leo niliamua kuwatafuta wakulu ili kupata ukweli, nimezungumza na wakulu kama watano, ili ku-clarify ishu za Cabinet Reshuffle, Why Mwakyembe? na kamati za Richmond na Madini, na Kingunge na cc, haya ndio niliyoyapata:-
1. Baraza la mawaziri, haliwezi kupanguliwa Bunge likiwa kwenye session kama lilivyo sasa hivi, kwa hiyo waliotuletea zile nyepesi nyepesi walikuwa simply ni waongo, ukweli ni kwamba Cabinet, itavunjwa rasmi anytime kuanzia kesho ambapo itakuwa ndio mwisho wa kikao cha bunge, hilo hata mawaziri wenyewe wanajua maana kila wakiombwa refferences na wabunge au viongozi wa juu wamekuwa wakisema kuwa wasubiri mpaka Reshuffle ipite kwanza.
2. Mwakyembe, nimeambiwa kuwa:-
(a). ndiye the best mbunge ambaye so far ndiye anahusika sana na kuwafundisha wabunge karibu wote ishu zinazohusiana na sheria katika siasa za bunge, na taifa kwa ujumla.
(b). Hata rais wa Jamhuri, humtumia sana kwa ushauri wa kisheria katika masuala ya kitaifa,
(c). The best of all, wakulu wote wameniapia kwa Miungu yao yote kuwa Mwakyembe, hanunuliki hata siku moja ni kiongozi ambaye yuko radhi kufa na mashati yake mawili.
3. Kamati za Richmond na Madini:-
(a). Kamati hiyo imeundwa kwa shinikizo la wabunge kumlazimisha Waziri Mkuu na Spika, kwa nguvu na sio kwamba imeundwa kwa ridhaa ya Spika. Spika amelazimishwa na wabunge ambao wamekuwa wakidai kwa muda mrefu iundwe, lakini wamekuwa wakitishiwa na Luwassa, kuwa rais hataki, majuzi baadhi ya wabunge wa CCM walimvulia Luwassa na Spika, kuwa wako radhi kufa na liwalo liwe, lakini hawatoki kwenye kikao mpaka kamati iundwe, ndio ikaishia kuundwa, huku wao wabunge wakimchagua Mwakyembe kuiongoza kamati hiyo.
(b). Kamati ya madini iliyoundwa na rais ni the ongoing showdown betweeen Muungwana, na Spika, na kwamba Spika sasa hivi yuko hoi kwa kuundwa kamati hiyo ambayo yeye na wabunge wengine walikataa na kumfukuza Zitto, the dataz ni kwamba Muungwana was ver upset na kitendo cha kumsimamisha Zitto, na hii ni just a message kwa bunge na Spika, kuwa wakae chonjo, na more are coming!
3. Kingunge:-
(a). The dataz ni kwamba alishindwa kwa kuwa na kura ndogo kwenye NEC, lakini akaongezewa kwa ujanja na kupita.
(b). Ilipokuja kwenye cc, the dataz ni Muungwana, ambaye hupewa kwanza matokeo yote kabla ya kutangazwa, alicheka sana kuona tena Mzee kura ndogo na kusema kuwa sasa ni clear kuwa wananchi hawamtaki tena huyu mzeee, huku akicheka sana na kuwaita viongozi wengine waliokuwepo huko faragha kuwa njoooni muone rafiki yenu alivyoangushwa na wanachi, huyu mzee sasa basi!!! Na mepigwa chini na wajumbe wote wapya ambao nasikia kuwa wameapa kuwa huo wa Kingunge ni mwanzo tu!
Ahsante Wakuu, heshima ya JF mbele na tunaendelea ku-monitor yanayojiri na tutayaweka hapa hapa giladi mchana kweupeeee!