Mawaziri matumbo joto

Mawaziri matumbo joto

Ndugu Mtanzania,

Tusisahau kwamba Salva pale Ikulu ni mtu wao...wanasema wana chanzo credible pale. The fact kwamba yaliyosemwa humu JF yanafanana na yaliyoandikwa na Raiamwema, inawezekana ni kuwa ya kweli yote ndiyo maana maelezo yanafanana. Kama chanzo cha JF kilipata taarifa Ikulu, na kama taarifa ya Raiamwema pia ilitoka ikulu, basi ndiyo maana taarifa zinafanana...mnaonaje wakuu?

...Thubutuuu...
Hamjui huyo salva ndiye aliye wasababishia wakaingia mkenge kuuza gazeti kwa RA? Mnajua nini kilichomfanya Ulimwengu aachie ngazi pale? Nasikia huyu salva ndiye haswaa mbaya wao. kama sio yeye leo tusingekuwa na gazeti Raia Mwema ambalo kila kitu hakina tofauti na enzi za uhai wa Rai.

...Hapo tujue mtu wao pale magogoni wanaye na labda asiwe salva kwani huyo jenerali ameshawahi kufanya kazi ktk nafasi nyeti ambazo zinamweka jirani na system hivyo lazma ana mdomo pale.....
 
..who cares kama matumbo joto,kwanza wapunguze idadi ya huo msururu wa mawaziri 60,wa nini wote hao kazi kututia hasara tuu kwa kodi yetu!
 
Tz, anazo nafasi mbili tu kwenye kuteua.. halafu miye sitaki maprofesa na hawa watu wenye CVs ndeeeefu wawe mawaziri (labda Ukatibu Mkuu). Upande wa mawaziri tunahitaji breed ya watu wanaoitwa Viongozi ambao CVs zao zimejaa "uongozi"!!! Haya ya kuamini kuwa maprofesa ndio watatuokoa kutoka katika shimo walilolichimba wenyewe ni njozi za Alinacha!

Mwanakijiji naamini Jk amekusikia,Msolla sasa hivi lazima aende nje ya nyumba
 
Hiyo habari ina siri kubwa,
Msola nje,
Msabaha nje,
Mramba nje,
Mungai nje,
Mwakyusa nje,
Mwandosya nje
,
upande wa manaibu..
Buriani nje,
Masha nje,
Mathayo nje
,
Nsanzugwako,

Naona kuna haja ya kumtafuta Sheikh Yahya asafishe nyota za mawaziri wenye majina kuanzia na M🙂
 
4 WILLIAM LIKUVI huyu inasemekana atapokezana na mungai na mkuu wa mkoa wa dodoma atateuliwa mwengine
Mwanasiasa,

nimeipata hiyo kwamba kuna Naibu waziri mmoja atakukwa na position mbili,ya ubunge na ukuu wa Mkoa,
Lengo la Jk si kuwang'oa watu ni kufanya Reshuffle tu katika madaraka..ni usanii flan hivi utafanyiak ili kuweka tija na chachu ya mandeleo ili mizigo tisa aliyojibebesha mzee wa kaya kufika atakako..
Kati ya Nchimbi au Ngeleja wanaweza kupewa Nafasi hizo,ila nafasi kubwa ya ukuu wa mkoa atapewa Nchimbi ili kuimarisha chama pale Dodoma na Hgeleja hatatolewa ila atabakizwa katika nafasi yake ,hii ni kwa mujibu wa watu wa system.Nimeona Ngeleja akiwa karibu sana na Muungwana kipindi tulipokuwa Lindi wakicheka pamoja,sasa kama akimng'oa huyu basi Jk atakuwa hana masihara
 
Kwani kikao cha bunge hili kinaisha lini wananchi????

Hivi jamani kupunguza serikali ni kupunguza mawizara au mawaziri;
Naamini hivyo vinapaswa viende pamoja ,je wana JF ikiwa huo ndio utaratibu inakuwaje haya mawizara yaliyopangiwa mafungu ,machapisho n.k???

Nawaomba ni vema tumuache Muungwana afanye kazi kwa style yake na kwa muda wake,punguzeni kifukenge jamani
 
Kwani kikao cha bunge hili kinaisha lini wananchi????

Hivi jamani kupunguza serikali ni kupunguza mawizara au mawaziri;
Naamini hivyo vinapaswa viende pamoja ,je wana JF ikiwa huo ndio utaratibu inakuwaje haya mawizara yaliyopangiwa mafungu ,machapisho n.k???

Nawaomba ni vema tumuache Muungwana afanye kazi kwa style yake na kwa muda wake,punguzeni kifukenge jamani

Tutamuacha tu aple tutakapo ona mamb yanakwenda sawa, kama yanaenda ndivyo sivyo lazima tuendeleze libeneke la kelele pengine masikio yake yatazibuka ili mambo yaende ndivyo
 
Kwani kikao cha bunge hili kinaisha lini wananchi????

Hivi jamani kupunguza serikali ni kupunguza mawizara au mawaziri;
Naamini hivyo vinapaswa viende pamoja ,je wana JF ikiwa huo ndio utaratibu inakuwaje haya mawizara yaliyopangiwa mafungu ,machapisho n.k???

Nawaomba ni vema tumuache Muungwana afanye kazi kwa style yake na kwa muda wake,punguzeni kifukenge jamani

KIkao cha bunge ni kama kinaisha kesho (tarehe 16/11/2007).
 
Naona JF tumepata watabiri kweli, haya tunawasoma, lakini sijajua kabisa inatusaidia sisi kama wakata ishu hapa. Au hii nayo ni kukata ishu?
 
Huyu JK wenu ni msanii tu, hana lolote anafikiri ukubwa wa baraza la mawaziri ndo kudeliver?
 
Wakuu kwa muda sasa kumekuwa na speculation nyingi za uongo hapa forum, kuhusiana na reshuffle ya cabinet, kwa hiyo leo niliamua kuwatafuta wakulu ili kupata ukweli, nimezungumza na wakulu kama watano, ili ku-clarify ishu za Cabinet Reshuffle, Why Mwakyembe? na kamati za Richmond na Madini, na Kingunge na cc, haya ndio niliyoyapata:-

1. Baraza la mawaziri, haliwezi kupanguliwa Bunge likiwa kwenye session kama lilivyo sasa hivi, kwa hiyo waliotuletea zile nyepesi nyepesi walikuwa simply ni waongo, ukweli ni kwamba Cabinet, itavunjwa rasmi anytime kuanzia kesho ambapo itakuwa ndio mwisho wa kikao cha bunge, hilo hata mawaziri wenyewe wanajua maana kila wakiombwa refferences na wabunge au viongozi wa juu wamekuwa wakisema kuwa wasubiri mpaka Reshuffle ipite kwanza.

2. Mwakyembe, nimeambiwa kuwa:-

(a). ndiye the best mbunge ambaye so far ndiye anahusika sana na kuwafundisha wabunge karibu wote ishu zinazohusiana na sheria katika siasa za bunge, na taifa kwa ujumla.

(b). Hata rais wa Jamhuri, humtumia sana kwa ushauri wa kisheria katika masuala ya kitaifa,

(c). The best of all, wakulu wote wameniapia kwa Miungu yao yote kuwa Mwakyembe, hanunuliki hata siku moja ni kiongozi ambaye yuko radhi kufa na mashati yake mawili.

3. Kamati za Richmond na Madini:-

(a). Kamati hiyo imeundwa kwa shinikizo la wabunge kumlazimisha Waziri Mkuu na Spika, kwa nguvu na sio kwamba imeundwa kwa ridhaa ya Spika. Spika amelazimishwa na wabunge ambao wamekuwa wakidai kwa muda mrefu iundwe, lakini wamekuwa wakitishiwa na Luwassa, kuwa rais hataki, majuzi baadhi ya wabunge wa CCM walimvulia Luwassa na Spika, kuwa wako radhi kufa na liwalo liwe, lakini hawatoki kwenye kikao mpaka kamati iundwe, ndio ikaishia kuundwa, huku wao wabunge wakimchagua Mwakyembe kuiongoza kamati hiyo.

(b). Kamati ya madini iliyoundwa na rais ni the ongoing showdown betweeen Muungwana, na Spika, na kwamba Spika sasa hivi yuko hoi kwa kuundwa kamati hiyo ambayo yeye na wabunge wengine walikataa na kumfukuza Zitto, the dataz ni kwamba Muungwana was ver upset na kitendo cha kumsimamisha Zitto, na hii ni just a message kwa bunge na Spika, kuwa wakae chonjo, na more are coming!

3. Kingunge:-

(a). The dataz ni kwamba alishindwa kwa kuwa na kura ndogo kwenye NEC, lakini akaongezewa kwa ujanja na kupita.

(b). Ilipokuja kwenye cc, the dataz ni Muungwana, ambaye hupewa kwanza matokeo yote kabla ya kutangazwa, alicheka sana kuona tena Mzee kura ndogo na kusema kuwa sasa ni clear kuwa wananchi hawamtaki tena huyu mzeee, huku akicheka sana na kuwaita viongozi wengine waliokuwepo huko faragha kuwa njoooni muone rafiki yenu alivyoangushwa na wanachi, huyu mzee sasa basi!!! Na mepigwa chini na wajumbe wote wapya ambao nasikia kuwa wameapa kuwa huo wa Kingunge ni mwanzo tu!

Ahsante Wakuu, heshima ya JF mbele na tunaendelea ku-monitor yanayojiri na tutayaweka hapa hapa giladi mchana kweupeeee!
 
Field Marshall ES,

Asante kwa hizi dataz, wewe nakuaminia. Hawa waliotanguliza speculations zilizoishia kuwa sivyo walishani-upset, angalao umenipoza.

Twasubiri.

B.J.Y. Kithuku
 
tunajua kuwa kuna mawaziri wengi wanaokuja hapa kutafuta dataz, ninaomba niwaambie kuwa cha moto kinakuja,

according to the dataz Muungwana, sasa ameamua kuwa waliomfadhili urais sasa zamu yao imeisha, ni zamu ya wale aliokuwa akiwataka rohoni kwake lakini akashindwa kutokana na kulipa fadhila kwanza, sasa itakuwa for real,

Mkuu Karamagi, nasikia yuko hoi bin taabani maana for the last at least two months, Muungwana hajaongea ana kwa ana na Karamagi, wala Rostam!

Kama nilivyoahidi, tunaendelea ku-monitor situation na tutaziweka hapa hapa JF tukufu!
 
Msee ES,
Asante sana kwa ufafanuzi, maana usanii ulikuwa umezidi hapa......this is like a breath of fresh air!!.
Thanx
 
3. Kingunge:-

(a). The dataz ni kwamba alishindwa kwa kuwa na kura ndogo kwenye NEC, lakini akaongezewa kwa ujanja na kupita.

(b). Ilipokuja kwenye cc, the dataz ni Muungwana, ambaye hupewa kwanza matokeo yote kabla ya kutangazwa, alicheka sana kuona tena Mzee kura ndogo na kusema kuwa sasa ni clear kuwa wananchi hawamtaki tena huyu mzeee, huku akicheka sana na kuwaita viongozi wengine waliokuwepo huko faragha kuwa njoooni muone rafiki yenu alivyoangushwa na wanachi, huyu mzee sasa basi!!! Na mepigwa chini na wajumbe wote wapya ambao nasikia kuwa wameapa kuwa huo wa Kingunge ni mwanzo tu!

Ahsante Wakuu, heshima ya JF mbele na tunaendelea ku-monitor yanayojiri na tutayaweka hapa hapa giladi mchana kweupeeee



Sijaelewa, ninajua kuwa Kingunge hayumo kwenye CC au nimekosea??
 
Back
Top Bottom