Tetesi: Mawaziri wa Kikwete: Lazaro Nyalandu, na Jumba la karibu milioni 600 Arusha!

Tetesi: Mawaziri wa Kikwete: Lazaro Nyalandu, na Jumba la karibu milioni 600 Arusha!

Mi nashangaa mtu unaamka asubuhi asubuhi unaanza kujadili mali za mwanaume mwenzako. Pigana nawe upate, kila kitu kinawezekena. Kuna nyumba nyingi sana zenye thamani zaid ya hiyo na zinamilikiwa na raia wa kawaida. Kuwa na nyumba nzuri siyo lazima uwe waziri au kiongozi serikalini. Hapa sion kama Nyalandu kumiliki hiyo nyumba ni big issue, hata wewe unaweza kumiliki. Chamuhimu ni kuacha bla bla na kufanya kazi kwa bidii.
 
Wakuu wa serikali na mamlaka zake kama takukuru wana wajibu wa kuchunguzamali za viongozi wote ili kuondoa ufisadi unaozidi kuongezeka na kuacha pengo kubwa kati ya maskini na matajiri.
 
Kwa mshangao wa wengi huyu mwizi Nyalandu atateuliwa kuwa waziri kamili wa viwanda
 
Mimi sishangai kwa huyu Lazaro kuwa jumba la thamani hiyo,kwasababu ana pesa ndefu kabla hata hajawa mbunge na hatimaye waziri,japo hili halimzuhii kufuja mali za umma.Na kama mchangiaji mmoja alivyododosa tatizo ni utumiaji rasilimali za nchi kufanya mambo binafsi kama hayo.kama mleta uzi ana ushahidi hata wa kimazingira tu,aumwage hapa ili huu uzi usikae kiswaziswazi.

Pesa ndefu zipi? Au summer camp inawafanya watu kuwa matajiri haraka? Au za EOTF? Msiwe wajinga wadanganyika mwizi ni mwizi haijalishi kaiba lini na wapi, ila inavyoonekana humjui Lazaro wewe usingediriki kusema eti ana pesa ndefu kabla hajawa waziri! Ujinga mtupu.!
 
Hapa Tz mwanasiasa anakuwa ktk cheo fulani ktk muda halafu then anajulimbikizia mali utadhani ametumika 50yrs. Utajiri sio dhambi ila tunahoji utajiri usio halali kwani vigezo vya kawaida vinakataa (kulinganisha na hiyo proportion of wealth).

Pia ni udhaifu mkubwa sana wa UWT, haina uwezo wa kuchunguza, kuchuja au kusimamia maslahi ya nchi hii kwa sasa. Kikwete ana madhaifu makubwa lakini tungeona TISS' role ktk kupunguza madudu haya. Ingevunjiwliwa mbali. Hata jeshi la Polisi nalo ni ku-disband na kuanza upya.
 
Hapa hakuna anayezuia waziri kumiliki nyumba. Tatizo ni pale anapomiliki jumba la mamilioni ndani ya muda mfupi. Hivi unafikri wangekuwa na nyumba z. 100 hadi 200m nani angepiga kelele? Haya majumba ipo siku tutayarudisha kwa wakala wa majengo au NHC!
 
Kumbe ana nyumba nyingine tena! Mi nyumba ninayoijua iko barabara ya Njiro kabla ya Tiger Supermarket upande wa kulia wa barabara inayoelekea Njiro. Hii ndiyo nyumba aliyokuwa akiishi na Faraja Kota yule mlimbwende wetu wa Tanzania

kaka hapa upande wa kulia wa tiger supermarket mbona kuna nyumba za ppf,. Uneza fafanua vizuri apo
 
Kuna kasumba inajengeka kwa kasi sana kuwa ukiwa kiongozi hupaswi kuwa na maendeleo binafsi hivyo kila mwenye mali anaonekana mwizi. Jaribu kijiuliza huyu kiongozi labda kapata uongozi mwaka 2005 na yuko kwenye mid 40s, kipindi cha nyuma alikuwa anajishughulisha na nini? Alikuwa amekaa tu anasubiri uongozi uje? Hakuwa na shughuli zake za kumletea kipato na tena labda ni msomi? Kwa mazingira ya ccm ya sasa hivi viongozi wana biashara nyingine kibao! Huo ndo mfumo walioukubali, hivyo kiongozi mwenye mali ni lazima apewe tuhuma endapo tu tuna wasiwasi kama mali alizonazo amepata kwa kiuba. Ukileta taarifa kuwa mbunge au waziri anamiliki mali fulani halafu kwenye utendaji wake hauna dosari hata siku moja, hatujawahi kusikia kashfa sidhani kama ni fair kumtuhumu. Binafsi nina taarifa kuwa nyalandu yupo kwenye bad terms kwa muda mrefu tu pale wizarani na waziri wake na pia katibu mkuu, kiasi kwamba katibu mkuu analimit hata safari zake za kikazi kwa kumnyima mafungu! Sasa huo ufisadi wa kumpatia mabilioni then accounting officer wa wizara akuangalie tu wakati mpo kwenye bad terms! Sidhani. Mngeangalia dili zake nyingine, labda zile nyara alizokuwa anakimbiza usiku juzi kati hapa.
 
Mimi kwangu sioni tatizo kama ni pesa zake. Ila tatizo linakuja kama kazipata kupitia kazi yake ya Uwaziri. Kama mnafikiria hivyo hamna Kiongozi wa nchi hii ni msafi
 
NO magamba wote baada ya zoezi la kujiongezea posho kushindikana wakaamua kuidhainisha chenji ya Rada hivyo hawa watu waligawana we acha tu
 
....Hii sio habari, nilitegemea utueleze hapa namna alivyoitumia nafasi yake ya Unaibu Waziri kuipata nyumba hiyo, otherwise nakumbuka huyu alikuwa ni mgombea pekee wa Ubunge kwenye uchaguzi wa 2010 aliyekuwa anatumia helkopta kwenye kampeni zake, na wakati huo alikuwa hajawahi kushika uwaziri wala unaibu waziri....

...Ukumbuke, kuna Watanzania wengi ambao hawajawahi ata kushika Ubunge na wana nyumba kali zaidi ya hizo, hivyo sintashangaa kama amezipata nje ya Ubunge na Uwaziri wake wa miaka 2 hii...

...N.B: Azimio la Arusha lilishakufa, kwa Tanzania ya sasa kuwa tajiri sio kikwazo cha mtu kuwa Kiongozi...
 
Hapa Tz mwanasiasa anakuwa ktk cheo fulani ktk muda halafu then anajulimbikizia mali utadhani ametumika 50yrs. Utajiri sio dhambi ila tunahoji utajiri usio halali kwani vigezo vya kawaida vinakataa (kulinganisha na hiyo proportion of wealth).

Pia ni udhaifu mkubwa sana wa UWT, haina uwezo wa kuchunguza, kuchuja au kusimamia maslahi ya nchi hii kwa sasa. Kikwete ana madhaifu makubwa lakini tungeona TISS' role ktk kupunguza madudu haya. Ingevunjiwliwa mbali. Hata jeshi la Polisi nalo ni ku-disband na kuanza upya.

Hao TISS ndo wanaongoza kwenye ligi ya ufisadi, sasa unategemea wamchome nani? Tunahitaji mtazamo mpya! Imefikia mahali kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake. Tatizo ni pale mbuzi wengi wanapokuwa wamefungiwa mahali ambapo hakuna majani; lazima watakata kamba zao na kuingilia wale waliofungiwa kamba palipojaa majani. Lazima watapigana vichwa tu, halafu yule mbuzi aliyefungiwa penye majani atakuwa hatarini zaidi, kwani mbuzi waliokata kamba ni wengi. Yanayoendelea sasa ndio dalili za kuwa mwanzo umeshaanza!

Tunatarajia watu watajirike kwa kufanya shughuli halali. Shughuli halali hazijifichi! Tena shughuli halali hazileti mafanikio ya haraka haraka ki-hivyo; labda kwa kurithi. Haiwezekani serikali yote kila mtu akawa kwenye mfereji wa kujichotea; ni wachache tu watakaopata hiyo nafasi. Sasa wale ambao nafasi zao haziwapi nafasi ya kujichotea, hawawezi kukubali wao kulala njaa wakati wenzao wanazidi kujichotea.

Nchi zinazosambaratika zote, huanza na mitindo hii ya mbuzi kula kwa urefu wa kamba yake. Mambo huanza pole pole hivi, lawama zisizoisha. Wale walio, penye majani ya kutosha, huziba masikio, wakiendelea kula kwa urefu wa kamba zao - hadi hapo wanapojikuta wamezungukwa na kundi la waliokata kamba zao nao wakitaka kuja kula pale pale penye majani. Itafikia wakati kila mtu atataka afanyie kazi Benki kuu, TRA au hazina! Halafu hiyo hazina, TRA na benki kuu watakuwa wakikusanya kutoka wapi? kodi zitaendelea kuwabana wachache, wengi wakizikwepa. Hadi wale wanaozilipa watafirisika wote, watabaki wanafanya biashara wale tu wasiolipa kodi, hatima yake nini? Wale waliosoma uchumi wanajua.

Walianza watu kidogo kidogo. Akiiba anajenga, hasumbuliwi, anaonekana ndo alikuwa mjanja. Sasa wanaiba wale walioko juu kabisa. Ni nani wa kumzuia mwenzie??? Somalia, Congo zinashangaa tunajiunga nao kwa kasi ya ajabu!!
 
zaidi ya mshahara wa waziri na posho zake ambazo haziwezi zidi m7 kwa mwezi. Kuna kipato gani zaidi cha kumuwezesha mtu kujenga nyumba ya b1 kwa kuzingatia na maisha mengine yanaendelea?
nawasihi tuache wivu na fitina,,,mambo haya ndio yanasababisha watu kuwekeza na kuficha fedha nje ya nchi,,,,mimi nina miaka 15 ya utumishi...afisa mdogo,,,mshahara wangu na marupurupu yangu yote,,,leo hayazidi 1.5mil kwa mwezi,,,sijawahi pata take home laki nne,,mimi ni kukopo kukopa na mimi,,nawekeza,,najenga,,mwishon walevi,,wachangia harusi,wasiopitwa na fashion ya magari na mavazi,,,wananiita fisadi,,thaman ya nyumba ile na heka 6 nilizonunua miaka 13 iliyopita,,kibaha kwa eka elfu50,,,mshahara ukiwa laki mbili,,,leo sina hata bajaji,,nikimaliza nitanunua magari,,,si mtaandamana,,,hivi waziri wetu kuwa na heka tatu ni issue,,na nyumba ya mil500,mavaluer wasaidie,,,sitetei ufisadi naangalia logic,,,,zipo mali za kupigia kelele,,hazielezeki,,,,,:yo:
 
Back
Top Bottom