jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
TAKUKURU WAPO KAZINI HADI WANABATIZWA JINA LA WATU WASIOJULIKANATAKUKURU kazini na watu mmefukua kaburi!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
TAKUKURU WAPO KAZINI HADI WANABATIZWA JINA LA WATU WASIOJULIKANATAKUKURU kazini na watu mmefukua kaburi!
Baada ya mawaziri wawili wa JK kuhusishwa na umiliki wa majumba/makazi ya mamilioini ya shilingi muda mfupi tu baada ya kushika nafasi zao Waziri mwingine anatajwa kumilimi jumba kubwa ambalo vyanzo vyetu vinakisia thamani yake kuwa ni zaidi ya nusu bilioni. Kutokana na vyanzo hivyo vya kuamika jumba hilo liko kwenye Elkirevi, Kitongoji cha Olorukwa.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya ndani kabisa eneo hilo linadaiwa kuwa lilipatikana baada ya Bw. Nyalandu kununua ardhi yenye eneo la Eka 3 hivi kutoka kwa wanavijiji watano. Jumba lenyewe limejengwa chini ya mwaka mmoja na kukamilikama mwishoni mwa 2011. Jumba limezungushwa na ukuta wa karibu futi 10 na juu yake inadaiwa limewekwa waya wa umeme (electric fence)
Ni kwenye jumba hili ambapo Bw. Nyalandu alifanyia Sherehe ya Mwaka mpya na bila ya shaka ilikuwa ni 'house warming' party. Taarifa hizi zinaendana na zile za mawaziri wengine ambao tayari habari zao za umiliki wa majumba yenye thamani kubwa kuliko vipato vyao na walizopata ndani ya muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Mawaziri wengine ni Bw. Maige na Ngeleja ambao wote thamani ya nyumba zao zinakaribia shilingi bilioni 1!
Hata hivyo hadi hivi sasa Tume ya Maadili ya Viongozi haijaonesha kujua mambo haya wala kufuatilia na kuyaweka wazi kama wanazo taarifa na kama kweli vyote hivyo vinaendana na mishahara yao.