Tetesi: Mawaziri wa Kikwete: Lazaro Nyalandu, na Jumba la karibu milioni 600 Arusha!

Tetesi: Mawaziri wa Kikwete: Lazaro Nyalandu, na Jumba la karibu milioni 600 Arusha!

1.Jumba lenyewe hata picha hamna
2.Watumishi ni sawa na watu wengine sio dhambi kuwa na nyumba ya kuishi kwa taste ya mtu
3.Ni maono na mapenzi yenu watumishi waishi NHC HOUSES MAISHA YOTE
4.Tujiongeze na kuweka thread zenye mashiko.....
 
Hivi watanzania lini tutaendelea?, mlitaka waziri asijenge?, je, mtampangishia nyumba katika maisha yake yote hata akiwa nje ya uongozi? Acheni wivu wa kike. Naomba mawaziri wote wajenge majumba ya zaidi ya shilingi Bn 3 ili wachonga midomo wachonge zaidi hadi midomo itanuke.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".

Ushauri wako naamini watauzingatia. Ingawa sijui ni kiasi gani Ngosha atakubaliana nao.
 
Kumiliki nyumba nayo ni hoja nzito ya kujadili??? Unajua mkulu ana miliki mijumba ya aina gan?? Na mawaziri wengine ..
Hoja yako iko weak.
 
Wakuu,mimi binafsi sioni kujenga nyumba ni issue kwa hawa wateule wa jk,issue hapa ni gharama kubwa wanazotumia kujenga hizo nyumba.hii hali inanipa "question mark" ni kweli haya majumba wanayojenga wanaweza ku justfy pesa wanozojengea wanazipata wapi?
Je? Ni mishahara na posho tu kweli? Kamati ya maadili ipo wapi?

Wakati wa JK tuliambiwa tuna wivu. It is only now tunajua kwamba walikuwa wanaiba pesa zetu kwa 10% ya mikataba mbali mbali ya serikali.

Wizi wa mali ya umma hauwezi kumuacha mtu salama. Siyo enzi hizi.
 
Una uhakika mimi chadema? Unaweza nitajia namba ya kadi yangu? Nawewe uweke akiba ya maneno usihukumu mtu kama humjui itikadi yake wala hujawahi kutana naye kwenye mikutano. Sina chama na sihitaji chama chochote kuishi nchini mwangu.
Kwani ukiwa chadema Ni dhambi Kamanda?
 
Baada ya mawaziri wawili wa JK kuhusishwa na umiliki wa majumba/makazi ya mamilioini ya shilingi muda mfupi tu baada ya kushika nafasi zao Waziri mwingine anatajwa kumilimi jumba kubwa ambalo vyanzo vyetu vinakisia thamani yake kuwa ni zaidi ya nusu bilioni. Kutokana na vyanzo hivyo vya kuamika jumba hilo liko kwenye Elkirevi, Kitongoji cha Olorukwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya ndani kabisa eneo hilo linadaiwa kuwa lilipatikana baada ya Bw. Nyalandu kununua ardhi yenye eneo la Eka 3 hivi kutoka kwa wanavijiji watano. Jumba lenyewe limejengwa chini ya mwaka mmoja na kukamilikama mwishoni mwa 2011. Jumba limezungushwa na ukuta wa karibu futi 10 na juu yake inadaiwa limewekwa waya wa umeme (electric fence)

Ni kwenye jumba hili ambapo Bw. Nyalandu alifanyia Sherehe ya Mwaka mpya na bila ya shaka ilikuwa ni 'house warming' party. Taarifa hizi zinaendana na zile za mawaziri wengine ambao tayari habari zao za umiliki wa majumba yenye thamani kubwa kuliko vipato vyao na walizopata ndani ya muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Mawaziri wengine ni Bw. Maige na Ngeleja ambao wote thamani ya nyumba zao zinakaribia shilingi bilioni 1!

Hata hivyo hadi hivi sasa Tume ya Maadili ya Viongozi haijaonesha kujua mambo haya wala kufuatilia na kuyaweka wazi kama wanazo taarifa na kama kweli vyote hivyo vinaendana na mishahara yao.

WW kweli unashangaza waziri kuwa na nyumba ya hiyo hela unaona kahujumu wivu tu unakusumbua.unafahamu akisafiri kwa siku alikuwa anapata gapi acha kijicho bwana! Pambana na hali yako.
 
Mi nashangaa mtu unaamka asubuhi asubuhi unaanza kujadili mali za mwanaume mwenzako. Pigana nawe upate, kila kitu kinawezekena. Kuna nyumba nyingi sana zenye thamani zaid ya hiyo na zinamilikiwa na raia wa kawaida. Kuwa na nyumba nzuri siyo lazima uwe waziri au kiongozi serikalini. Hapa sion kama Nyalandu kumiliki hiyo nyumba ni big issue, hata wewe unaweza kumiliki. Chamuhimu ni kuacha bla bla na kufanya kazi kwa bidii.

Haaaaaa! Umeonaee wivu tu hajaona hata wafanyabiashara wana mijengo ya maana zaidi ya hiyo anayosema pambana usiwaze kupigia hesabu mali za watu.
 
Mtu amekaa Kwenye ubunge zaidi ya Miaka 5 na uwaziri Miaka 10.Ingekuwa nyumba inajengwa mfukoni tungesema haikuonekana Wakati inajengwa.kujenga siyo dhambi ila dhambi ni Kama hela imepatikana Ktk njia chafu..
 
zaidi ya mshahara wa waziri na posho zake ambazo haziwezi zidi m7 kwa mwezi. Kuna kipato gani zaidi cha kumuwezesha mtu kujenga nyumba ya b1 kwa kuzingatia na maisha mengine yanaendelea?
HII NI KWA AJILI TU AMEMCHANGIA LISSU AMBAYE NI KAMA NDUGUYE TOKA SINGIDA NA PIA NI MTANZANIA MWENZIE WACHENI UJINGA WENU OYEE
NYALANDU SASA HAPA NDO TUTAJUA AKILI ZA BOSSI WENUI ANA AKILI YA PH AMA NINI LETA POPCORN
 
Baada ya mawaziri wawili wa JK kuhusishwa na umiliki wa majumba/makazi ya mamilioini ya shilingi muda mfupi tu baada ya kushika nafasi zao Waziri mwingine anatajwa kumilimi jumba kubwa ambalo vyanzo vyetu vinakisia thamani yake kuwa ni zaidi ya nusu bilioni. Kutokana na vyanzo hivyo vya kuamika jumba hilo liko kwenye Elkirevi, Kitongoji cha Olorukwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya ndani kabisa eneo hilo linadaiwa kuwa lilipatikana baada ya Bw. Nyalandu kununua ardhi yenye eneo la Eka 3 hivi kutoka kwa wanavijiji watano. Jumba lenyewe limejengwa chini ya mwaka mmoja na kukamilikama mwishoni mwa 2011. Jumba limezungushwa na ukuta wa karibu futi 10 na juu yake inadaiwa limewekwa waya wa umeme (electric fence)

Ni kwenye jumba hili ambapo Bw. Nyalandu alifanyia Sherehe ya Mwaka mpya na bila ya shaka ilikuwa ni 'house warming' party. Taarifa hizi zinaendana na zile za mawaziri wengine ambao tayari habari zao za umiliki wa majumba yenye thamani kubwa kuliko vipato vyao na walizopata ndani ya muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Mawaziri wengine ni Bw. Maige na Ngeleja ambao wote thamani ya nyumba zao zinakaribia shilingi bilioni 1!

Hata hivyo hadi hivi sasa Tume ya Maadili ya Viongozi haijaonesha kujua mambo haya wala kufuatilia na kuyaweka wazi kama wanazo taarifa na kama kweli vyote hivyo vinaendana na mishahara yao.
Yaani Huu ni wivu na uchonganishi ., nyumba ya Nyalando naifahamu ni nyumba kubwa lakini ya kawaida , na kwa status ya Nyalandu ni nyumba anayostahili kuishi . Acha wivu na uchonganishi Mganga wa kienyeji ww , unapigia wenzanko ramli tu, kama umeshindwa kufanikiwa endelea kubanana kwenye nyumba za kuoangashi na uache wenzanko waishi.

Halafu Mods Muwe mnaangalia , Jamii Forum isiwe mahala pa kuchafua majina ya watu kwa vile tu wao hawapo huku others thread kama hii wala isingepaswa kuendelea kuwapo
 
Hv hamjui wabunge /mawaziri hukopeshwa tena hela ndefu ya yale ma vx, Vp na kile kiinua mgongo alichopata baada ya kumaliza muda wake? posho za waziri, per diem? Aisee pambaneni na hali zenu hakuna waziri wala katibu mkuu masikini nchi hii
 
kama hiyo namba ni sahihi basi kazi ipo.

Haaaa! kweli umasikini mzigo 600m inaonekana kahujumu lo! ni ndogo sana kwa waziri na hujui alisave miaka mingapi kama ww kila ukipata unatumbua hutaelewa.
 
Haaaa! kweli umasikini mzigo 600m inaonekana kahujumu lo! ni ndogo sana kwa waziri na hujui alisave miaka mingapi kama ww kila ukipata unatumbua hutaelewa.
sawa,ila naweza nikawa namfahamu background yake vyema tu hata kukuzidi.
 
Nyalandju sasa atazushiwa mpaka ugoni na mbuzi sababu tu kawaza tofauti na wenziye! Plastic hearted nation we are.....
 
Kwani ukiwa chadema Ni dhambi Kamanda?
Siyo ila siyo vizuri watu wakisoma kuwa umekwenda tofauti nao wanakubambika vyama. By the way Mbona siku hizi CUF hawaitaji au NCCR mageuzi au vimekufa?
 
Tutasikia kila baya la Nyalandu kisa kaenda Nairobi,. Anayetaka kwenda Nairob kwanza aikane nafsi yake.
 
1.Jumba lenyewe hata picha hamna
2.Watumishi ni sawa na watu wengine sio dhambi kuwa na nyumba ya kuishi kwa taste ya mtu
3.Ni maono na mapenzi yenu watumishi waishi NHC HOUSES MAISHA YOTE
4.Tujiongeze na kuweka thread zenye mashiko.....
kweli
 
Back
Top Bottom