OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Mh.Makonda akikagua gwaride
Kuna tetesi kuwa mawaziri wanaoingiliwa na Mkuu wa Mkoa Dar kimajukumu wanatarajia kuanzia kesho visivyo rasmi kumjadili. Mawaziri hao wamekuwa wakilalamika Makonda kukwapua majukumu ya wizara kupita kawaida jambo linalowafanya wao waonekane wapumbavu mbele ya Rais.
Wametolea mfano Makonda kumpoka Waziri Mwigulu katika kusimamia na kuamrisha jeshi la polisi mkoa wa Dar.
Tukio la juzi Makonda kuzuia bomoa bomoa imewaumiza sana na kuonekana Waziri wa Ardhi hatimizi wajibu wake. Pia mawaziri hao wamekuwa wazito kuchukua hatua kwa masuala ya Dar es Salaam wakihofia kudhalilika ikiwa Makonda atatengua maagizo yao
Vikao hivyo vitaanza Dodoma wiki kesho na vitaendelea kwingineko kadri watakavyokuwa wanakutana