Habari?
Jina Langu ni Mr Equator. Ni kijana ambaye najaribu kuyatafuta maisha. kwa njia mbali mbali.
Nimekuwa nikitafuta wazo la biashara ya pembeni (Side-hustle) ya mtaji kati ya Laki 1-2. Kwenye pita pita zangu nimepata wazo la biashara ya bahasha na nika angalia video baadhi Youtube. Nika pata ka mwelekeo kidogo.
Mimi swali langu ni je ushawahi kufanya biashara hii?
Je una hitaji na unapata changamoto?
Soko lake likoje?
Wanaouza kwa jumla wanauza kwa bei gani?
Wazo gani unaweza ukamshauri kijana kama mimi mwenye masaa 4 kuwekeza mwenye mtaji wa kama laki 1 au 2.