Mawazo Madogo madogo ya mitaji midogo midogo ..

Hornet

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
26,486
Reaction score
51,156
Kama tunavyojua biashara ni matokeo ya kusuluhisha changamoto zinazojitokeza katika maisha ya kila siku
Katika changamoto hizi ndipo unapogundua kuna jambo la kufanya kukuingizia kipato.

Haya hapa ni mawazo ambayo nimeyapata kwa kuangalia changamoto katika mazingira yetu ya KiTanzania ,pamoja na uzoefu wangu na uzoefu wa watu wengine

1.Utengenezaji wa bidhaa za urembo(jewerly)
Tanzania ina walimbendwe wengi wanaopenda kuvalia vivalio vya kuwaongezea urembo.
Hivyo basi unaweza kutumia nafasi hii kuanza kutengeneza vivalio kama vile hereni,bangili, vibanio vya nywele na hata kofia za nywele bandia.
jewelrymaking-300x225.jpg

2:Upandaji na uzaaji wa mbogamboga,maua na viungo

Hii inamfaa mtu mwenye eneo kidogo/ardhi kiasi ambapo anaweza kupanda maua yanayotumika kama urembo ndani na nje ya nyumba

Pia mboga mboga kama tembele,chinese n.k zinaweza kukuongezea kipato

Kwa upande wa viungo /herbs unaweza kupanda baadhi ya viungo ambavyo vinatosha hata kwenye vikopo kama vile mchaichai,giligilani au mint
Ambavyo unaweza kuuza kwenye hotel kubwa kubwa
10-essential-herbs-to-grow-coriander-03-sl.jpg

3 :Kununua,kusaga na kupack viungo mbalimbali

Hapa unaweza kupack viungo vya chai,pilau,nyama, n.k
Kinachotakiwa ni kufahamu mchanganyiko sahihi wa massala hizi kisha utavisaga kwa pamoja na kupack mchanganyiko wako na kuupeleka sokoni.

4; Ubunifu wa samani za Zamani

Pale watu wanapochoka samani zao za ndani unaweza kuzinunua,kuziongezea thamani na kuziuza upya
Unaweza kuongeza ama kupunguza kitu
Kubadili rangi
Au kuongezea nakshi mpya

images.jpg

5; kutembeza watalii

Katika nchi yetu kuna watalii wengi wanaokuja na wangependa kutembea maeneo tofauti tofauti
Kama unafahamu lugha ya kigeni na unafahamu maeneo yenye vivutio mbalimbali, ambayo ni unique hii ni fursa yako

Tembelea couch.Surfing.com
Au Airnbn ukutane na wateja wako.

6; Yaya
Je wewe unapenda watoto na una muda na eneo la kutosha ?
Hii inaweza kuwa fursa kwani kuna watu wanafanya kazi na hawana housegirl wa kuwaachia watoto

Unaweza kutumia mwanya huo kulelea watoto kadhaa katika mazingira yanayofanana na nyumbani kwao badala ya watoto kupelekwa shule,
Kwa muda ambao wazazi wanakuwa katika mishughuliko.

7:Usafi wa majumbani
Kuna watu hawalipendi jambo la kufanya usafi ikiwemo mabachelor
Unaweza kutumia nafasi hii
Kwa kuwafanyia watu usafi wa kina katika nyumba zao
Ikiwa ni pamoja na kuwafulia,kuosha vyombo,kusafisha madirisha n.k

#Nitaendelea#
Karibuni muongezee
 
Hiyo namba saba mwenye nayo hata humu anipe jamani
 
Namba moja nmeipenda. Malighafi zinapatikana wap??
 
Ahsante sana. Haya ndo mambo yanayotakiwa kusomwa na sisi watu wa nchi za dunia ya tatu
 
Kama tunavvijana.Youashara ni matokeo ya kusuluhisha changamoto zinazojitokeza katika maisha ya kila siku
Katika changamoto hizi ndipo unapogundua kuna jambo la kufanya kukuingizia kipato.

Haya hapa ni mawazo ambayo nimeyapata kwa kuangalia changamoto katika mazingira yetu ya KiTanzania ,pamoja na uzoefu wangu na uzoefu wa watu wengine

1.Utengenezaji wa bidhaa za urembo(jewerly)
Tanzania ina walimbendwe wengi wanaopenda kuvalia vivalio vya kuwaongezea urembo.
Hivyo basi unaweza kutumia nafasi hii kuanza kutengeneza vivalio kama vile hereni,bangili, vibanio vya nywele na hata kofia za nywele bandia.
View attachment 645314

2:Upandaji na uzaaji wa mbogamboga,maua na viungo

Hii inamfaa mtu mwenye eneo kidogo/ardhi kiasi ambapo anaweza kupanda maua yanayotumika kama urembo ndani na nje ya nyumba

Pia mboga mboga kama tembele,chinese n.k zinaweza kukuongezea kipato

Kwa upande wa viungo /herbs unaweza kupanda baadhi ya viungo ambavyo vinatosha hata kwenye vikopo kama vile mchaichai,giligilani au mint
Ambavyo unaweza kuuza kwenye hotel kubwa kubwa
View attachment 645320

3 :Kununua,kusaga na kupack viungo mbalimbali

Hapa unaweza kupack viungo vya chai,pilau,nyama, n.k
Kinachotakiwa ni kufahamu mchanganyiko sahihi wa massala hizi kisha utavisaga kwa pamoja na kupack mchanganyiko wako na kuupeleka sokoni.

4; Ubunifu wa samani za Zamani

Pale watu wanapochoka samani zao za ndani unaweza kuzinunua,kuziongezea thamani na kuziuza upya
Unaweza kuongeza ama kupunguza kitu
Kubadili rangi
Au kuongezea nakshi mpya

View attachment 645324
5; kutembeza watalii

Katika nchi yetu kuna watalii wengi wanaokuja na wangependa kutembea maeneo tofauti tofauti
Kama unafahamu lugha ya kigeni na unafahamu maeneo yenye vivutio mbalimbali, ambayo ni unique hii ni fursa yako

Tembelea couch.Surfing.com
Au Airnbn ukutane na wateja wako.

6; Yaya
Je wewe unapenda watoto na una muda na eneo la kutosha ?
Hii inaweza kuwa fursa kwani kuna watu wanafanya kazi na hawana housegirl wa kuwaachia watoto

Unaweza kutumia mwanya huo kulelea watoto kadhaa katika mazingira yanayofanana na nyumbani kwao badala ya watoto kupelekwa shule,
Kwa muda ambao wazazi wanakuwa katika mishughuliko.

7:Usafi wa majumbani
Kuna watu hawalipendi jambo la kufanya usafi ikiwemo mabachelor
Unaweza kutumia nafasi hii
Kwa kuwafanyia watu usafi wa kina katika nyumba zao
Ikiwa ni pamoja na kuwafulia,kuosha vyombo,kusafisha madirisha n.k

#Nitaendelea#
Karibuni muongezee
Hongera sana kwa ushauri mzuri na wenye kutukuka hasa kwa vijana. Hakika wewe ni Great thinker.
 
Back
Top Bottom