Mawazo mbadala

Mawazo mbadala

Tzania

Member
Joined
Jul 23, 2019
Posts
31
Reaction score
12
Habari zenu wakuu.

Natumaini wazima humu wote hebu tusaidiane mawazo wakuu mimi ni muajiriwa takribani 10 years kwa wahindi nimejitahidi nimebana kahela kangu nikafungua kaduka ka chakula kama chenye thamani ya 6,000,000 kana kama 2month Hadi sasa.

Kwa mawazo yangu niliitaji kukatia mkataba na mtu awe ananipa 30000 kwa kila siku kwa muda wa mwaka mmoja na miezi 3 baada ya hapo ofisi iwe yake je niko sahihi au nitakuwa nimefeli kwakuwa nikikomaa mwenyewe naona Kama hela nyingi natumia kiholela.

Je, nitakuwa nipo sahihi hapo kila kitu kuanzia mkataba? Ni juu yake mimi naitaji hela tu.
 
Nionavyo sio wazo baya, japo kuwa kama ni mtumiaji wa hela kiholela kama ulivyosema bado hata akikupa hiyo 30 per day zoezi linaweza kuwa gumu vilevile
 
Naomba hio kazi, mm nakupa hela yako vile utakavyo, hutajuta na utainjoi
 
Kwasiku unaoata mauzo ya kihasi gani na faida shingapi?
 
Unataka kufanya mchezo wa risk sana.
Atakupa wiki ya kwanza tu kuanzia wiki ya 2 ataanza kukupiga sound,sababu ni kwamba asili ya biashara ya duka ni tofauti na ya bodaboda kwa sababu ile ya bodaboda mtu akikaa stendi ana uhakika wa kupata vichwa kadhaa.
Lakini kwenye duka hakuna guarantee yaani hujui kama utauza pipi au utauza kiwembe au utauza kiberiti au sabuni au sukari au unga/mchele kwa hyo inakuwa ngumu sana mtu kuandaa hesabu ya kila siku
 
Back
Top Bottom