Mr mutuu
JF-Expert Member
- Jan 27, 2023
- 2,869
- 14,501
Siku ukienda kuuza ndo hapo hapo watakupiga spana....Nilijaribu kuwaza vile na nikatafuta mtu wa kununua lakini pesa niliyokuwa napatiwa haikuwa rafiki kwangu. Sijuwi ni kwa vile waliona nina tatizo 🤷
Nikupe ushauri ndugu, utakuja kufa kwa mawazo, mtaji wa laki alafu una presha ya kufukuzia milion 12 ya watu hautatoboa kaka nikuambie tu ukweli
Tafuta watu wa busara huko kwenu, then urudi ukae na hao wanakikundi mpange njia rafiki ya kuwalipa, wakikataa acha waende mahakamani deni halifungi mtu, tena ukiona ni watata Katoe tahadhari ya usalama polisi na uwaambie kabisa chochote kitakachokupata watahusika
Fanya hustle ukiwa umerelax nyumbani uwatafutie hela Yao, ila hili la kufanya biashara roho juu juu unajificha kama digidigi huwezi kutoboa chief utaishia kua chizi tu