Mawazo na ushauri wako vitanisaidia.

Nilijaribu kuwaza vile na nikatafuta mtu wa kununua lakini pesa niliyokuwa napatiwa haikuwa rafiki kwangu. Sijuwi ni kwa vile waliona nina tatizo 🤷
Siku ukienda kuuza ndo hapo hapo watakupiga spana....

Nikupe ushauri ndugu, utakuja kufa kwa mawazo, mtaji wa laki alafu una presha ya kufukuzia milion 12 ya watu hautatoboa kaka nikuambie tu ukweli

Tafuta watu wa busara huko kwenu, then urudi ukae na hao wanakikundi mpange njia rafiki ya kuwalipa, wakikataa acha waende mahakamani deni halifungi mtu, tena ukiona ni watata Katoe tahadhari ya usalama polisi na uwaambie kabisa chochote kitakachokupata watahusika

Fanya hustle ukiwa umerelax nyumbani uwatafutie hela Yao, ila hili la kufanya biashara roho juu juu unajificha kama digidigi huwezi kutoboa chief utaishia kua chizi tu
 
Nilijaribu kuwaza vile na nikatafuta mtu wa kununua lakini pesa niliyokuwa napatiwa haikuwa rafiki kwangu. Sijuwi ni kwa vile waliona nina tatizo 🤷
Pole sana mkuu,
Kama uliweza kukuza elfu 20 bas Pia Mungu akuwezeshe tena kukuza mtaji huo...

Kigenge tu ndio best (matunda
 
Daaah mii mwenzako niliachana na masomo ila huyo aunt aliyenifanya niache alikua na uhakika wa kunifanya niwe stable economically....

Ushauri
Rafiki kabla ya kuchukua maamuzi ya wewe kuondoka eneo hilo haukuweza kuongea nao ili uweze hata kuwalipa pesa zao kidogo kidogo?? Naamini ingekua ni njia nzuri ungeweza endelea na biashara yako hapo hapo
 
Sikulaumu kuondoka mkuu, kuna watu sio waelewa kabisa, mola akufanyie wepesi uweze kuwalipa!
Yaani we acha tu. Nilijaribu
Penye wengi mambo ni mengi.
Hisia zako zisikilize ila sijawah kutumia pesa za mtu ninayemtunzia kwa maana muda wowote atazihitaji. Ila sina neno
 
We acha tu. Ila wengi wao nilikuwa nikiwatunzia mfano laki hamsini kwa wao kuogopa kuzitumia ila lilipotokea wapo waliosikitika ila kiukweli nilipata tabu sana
 
Kukimbia ndo itakua imechochea gadhabu ya wanakikundi japo wasiwasi ndo akili!fanya kuuza hata kiwanja uwapunguze na mathalani kama hata utauza 8milion,wape 6 au 7 zingne zungusha uwalipe taratibu,uzuri hata mkienda kisheria yanazungumzika,wakati mwingne usilale ndani na pesa ya watu kwan unaweza kuta kuna wanakikundi wanajua mchongo!
 
Maelewano duni ndiyo maana nikaamua kuondoka
 
Nitaufanyia kazi ushauri huu japo vitisho ninavyovipata mpaka sasa ni hatari tupu
 
Pole sana ndugu!! Pesa yoote iyo umekaa nayo ndani!! Ni hatari


KAZI ni kipimo cha UTU
 
Kabla ya kuondoka nilijaribu kutafuta njia ya kumaliza tatizo lakini sikupata ushirikiano nikaona nitakuwa matatani ndipo nikaamua kuondoka.
 
Kabla ya kuondoka nilijaribu kutafuta njia ya kumaliza tatizo lakini sikupata ushirikiano nikaona nitakuwa matatani ndipo nikaamua kuondoka.
Bora urudi mkuu, matatizo utakayopata ukirudi yatakua nafuu kuliko kulazimisha kujitafuta upya ukiwa na laki
 
Nitaufanyia kazi ushauri huu japo vitisho ninavyovipata mpaka sasa ni hatari tupu
kama vitisho vimezid toa taarifa kwenye mamlaka i.e polisi ili waitwe na kuonywa!mimi sion kwanin wanakutisha wakat unalitambua deni na uko tayar kulpa!ndugu kimfaacho mtu ni alichonacho,uza kiwanja walipe afu ingine walipe taratibu!
 
"Kwa maana katika kikundi hiyo ilikuwa ni pesa ndogo tu. Ila kwangu mimi ni kubwa sana".

Hii hapa ni sababu kwanini hukupaswa kukimbia

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Nilijaribu kuwaza vile na nikatafuta mtu wa kununua lakini pesa niliyokuwa napatiwa haikuwa rafiki kwangu. Sijuwi ni kwa vile waliona nina tatizo 🤷
Ndivyo inavyokuwa, matatizo ni fursa na watu huyatumia sana kupiga hela.
Tuliza akili anza upya kwakuwa tayari unao uzoefu wa biashara mambo yatakuwa sawa.
 
Sio fupi ndefu sana
Mie nataka kujua kama unakunywa wanzuki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…