Mawazo utaratibu wa kuchanja

Mawazo utaratibu wa kuchanja

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Juzi ndugu yangu aliweza kuwasajili wazazi wetu kwa chanjo kwa kutumia mtandao.

Walipewa tarehe 5 kwenye kituo kule Ununio. Leo hii wakagundua kuna utaratibu mwingine wa kwenda kupanga line na kupata chanjo papo kwa papo kwa kujaza form. Sasa waliojiandikisha ni kama wanarukwa na hawa ambao wanaenda pale kwenye kituo moja kwa moja.

Ameenda leo na wamefanikiwa kupata chanjo.
Ushauri wangu ni serikali kuwa na utaratibu mmoja badala wa huu wa kupanga foleni waanze na watu wanaojiandikisha maana wazee ni vigumu kushindana na vijana kwenye foleni. Lakini kwasa Chanjo ni chache ingependeza kuwe na utaratibu mzuri zaidi.

Tatizo lingine kwenye vituo hawana computer sasa kama mzee wangu kachanja leo tarehe 3 na bado mtandao utaonyesha anatakiwa kuchanjwa tarehe 5 aliyopangiwa na mtandao sasa watapeleka dose ya chanjo kule kumbe mzee kasha chanja .

Ni muhimu kuingiza data zote kwenye computer palepale kwenye vituo ili kama mtu kachanja wasipeleke chanjo kwenye vituo mara mbili na wawape wale ambao wanahitaji
 
Usumbufu ni mkubwa sana.....hawafuati ulichojaza kwanza hawana hata access mtandao.....labda aga khan na IST
 
Afrika na mambo ya ICT/teknolojia ni sawa na tai vs sungura pori😅
 
Back
Top Bottom