Mawazo ya biashara

Smith Kiombo

Member
Joined
Jun 15, 2023
Posts
28
Reaction score
45
Habari zenu wana JF, Naamini wote ni wazima wa afya.

Mi ni kijana mpambanaji na kwenye harakati za utafutaji nikajikuta niko nje nchi na ni mda sasa tangu nilipotoka tz, Mungu amesaidia nimekusanya 150M ambazo napenda kuwekeza lkn kwa sababu nimekaa nje kwa mda mrefu sasa na mambo mengi yamebadilika.

Nilikuwa naomba ndugu zangu ni biashara ipi ambayo naweza nikaanza na huo mtaji na ikanitoa( 150M) naamini kuna watu wana mawazo mengi na mazuri lkn hawaja jaliwa kuwa na mitaji na kuna wengine wameanza lakini si kwa ukubwa wanao utaka kutokana na mitaji yao. karibuni kwa mawazo

Nb: kwa atakaye leta wazo nzuri na nikalipitisha tutafanya kazi pamoja au kulinunuwa kabisa wazo lake. Asanteni na karibu kwa mawazo
 
Nakushauri Fanya biashara ya restaurant,
Uza vyakula vikavu ,,,,
Kama
Chips
Burger
Kuku crunch,
Bites
Fresh Juice Tu!
Vitu vya kuzngatia ni kama
Eneo lenye watu wengi na parking iwepo baasi. Ubunifu mzuri wa kisasa wa ofisi.
 
Kama una usimamizi mzuri uza vinywaji vya jumla.
Pombe kali, bia, soda, juice nk.
Kama ukiwiwa basi pia hilo duka lako liwe na mahitaji ya nyumbani jumla na rejareja.

Kua na vijana wa usambazaji kuanzia wawili, ila kwa kuanza anza na mmoja unaemfahamu vyema na kumuamini then utaongeza wengine kadri ya mahitaji.

Fungua hiyo biashara eneo ambalo ndio linakua na halina upinzani mkali ili uvune wateja wengi.

Wateja wa biashara hii wengi ni wa kudumu, inakua kama wanakufanyia biashara kama utakua vizuri kuimaintain.

Kazi kwako.
 

ni sehemu hipi nzuri kwa hii biashara?
 
Kuna mashamba ya mpunga mkoani Mbeya wilaya ya Mbarali yanakodishwa kwa Kilimo cha mpunga waweza fanya uwekezaji na ukazalisha.

Waweza Wekeza kwenye biashara ya nafaka mfano mchele, kwa kusambaza mchele mikoa tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…