Mawifi inakuwaje? Kunakuwa na kutokuelewana na mke wa kaka yao

Hili halina ubishi tabu inayopatikana ni ya nguo kuchanika, hawa wanaojulikana mawifi inakuwa mtihani katika ndoa japo na wao huwa ni mawifi, yaani inakuwa hapaeleweki, embu wadada tupeni elimu inakuwaje?

Yani Acha kabisa mkuu! Alikuja mdogo wangu field nikakaa nae miezi 3 ilikuwa niyakutumia akili kama nasoma international school....

hamna rangi niliachaona hii kipindi nilikuwa natumia akili sana kubalance japo nilikuwa naona kabisa ndugu yangu anakosea na nilikuwa ni mkali sana hii ndo ilinisaidia”

Na dogo kwa sababu namjua alivyo haikunipa shida ila sijui ni kwann lazima purukushani kidogo na usipotumia akili unaweza kuharibu kabisa ni mtihani sana kuishi na ndugu om kwako ukiwa una mke
 
Nipo sana ila huwa nakomenti kidogo kama hivi.

Si unajua tena nadumisha mawifi wasigombane na wifi yao[emoji3][emoji3][emoji3]
Ukiwa unakomenti mara chache nitag ili niwe nakuona 🙈

Ugomvi wa mawifi unaweza kutokea bila wewe kujua chanzo 😁
 

Kuna wengine wanatenganisha familia kwakuwa na wivu wa kupitiliza na hawako tayari ndugu wapate mapenzi ya mumewe hata kama alikuwa anajua waliyapata!

Kuna wengine wanakwenda kwenye ndoa kwa lengo la kuwakomoa ndugu kwa hiyo hapo panakuwa hapatoshi!
 

Hahahaha hii formula ni kama ina ukweli kabisa!
 
Binafsi huwa nipo busy na mambo yangu. Sina muda wa kufuatilia familia za kaka zangu wala kwa upande wa mwenza wangu.

Nawapenda sana wifi zangu na wanajua lakini kila mmoja ashinde mechi zake, hii inapunguza malumbano na vioja vya kila aina.

Hahahahha hakika ni wachache kama wewe! Mawifi wengi lazima wafatilie maendeleo ya kaka zao na hii inatokana na upendo wa asili(bond) na katika bond hiyo ndipo kuna zalisha ugomvi!
 
Sitaki familia ambazo macho yote yapo kwa kaka yao
Familia ambazo kaka yao ni mtoto pekee wa kiume.
Familia ambazo zinampangia kaka yao maamuzi na hana sauti.
Familia ambazo mawifi ndio final say.

Mapema sana tutashindwana.

Basi kwa mtaji huu unaweza kuchagua sana na kuchelewa maana asilimia 70 za familia za kibongo ziko hivyo!
 

Na huu ni mtihani mkubwa sana maana mkeo anashindwa kusema na awezi kusema kabisa na wewe ukisema unaonekana unamtesa mdogo wako na pengine unawaza akirudi nyumbani atakwenda kusema nini?
 
Na huu ni mtihani mkubwa sana maana mkeo anashindwa kusema na awezi kusema kabisa na wewe ukisema unaonekana unamtesa mdogo wako na pengine unawaza akirudi nyumbani atakwenda kusema nini?

Acha kabisa mkuu lakini ndugu wa mke wakija mambo huwa shwari na ndo sababu hata kwa ndugu yangu nilijitaidi kwend nae ivyo ivyo.... Maana hili nilakuwa nalo makini hawa wake zetu nao niwakuishi nao kwa akili
 
Acha kabisa mkuu lakini ndugu wa mke wakija mambo huwa shwari na ndo sababu hata kwa ndugu yangu nilijitaidi kwend nae ivyo ivyo.... Maana hili nilakuwa nalo makini hawa wake zetu nao niwakuishi nao kwa akili

Na hili ni tatizo lingine kwa wanawake zetu yani ndugu zake wakija kunakuwa na utulivu sana na hakuna maneno wala malalamiko lakini wakija ndugu zetu wanaume lazima kichwa kikuume unaweza kuta mtu kalala tuu ndani hachangamki kama mwanzo!

Unaweza kuta malalamiko kila leo au wanawake wengine hawaongei lakini yeye kila mara ni kununa tuu hadi ndugu au watu wako wanaondoka!

Kwakweli wanawake wana changamoto sana....na ni mtihani sana kujaribu kuwa pande zote!
 
Hahahahha hakika ni wachache kama wewe! Mawifi wengi lazima wafatilie maendeleo ya kaka zao na hii inatokana na upendo wa asili(bond) na katika bond hiyo ndipo kuna zalisha ugomvi!
Tunawapenda kaka zetu lakini isiwe sababu ya kuingilia maisha yao na familia zao.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] walijuaje kaka yao yuko romantic
 
Juzi huko mwanza kuna mtu kamlisha mama mkwe sumu eti nyumba yake sio kituo cha kulelea wazee. Huyu naye unamzungumziaje
 
Sijawai kuwa na ugomvi na mawifi kwanza sina mazoea nao, mwaka unaeza katika hamna aliempigia simu mwenzake. Kitu kingine hamna hata mmoja nineishi nae mmkoa mmoja. Ni ngumu kugombana kama hamkai pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…