Max Malipo wawekeni wazi mawakala wenu kuhusu kupungua kwa kamisheni

Isbnmax

Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
29
Reaction score
33
Max Malipo wawekeni wazi mawakala wenu kuhusu kupungua kwa kamisheni, haiwezekani mkasema tu kuwa kamishen imepungua kutoka 2.5% hadi 0.5% ya mauzo anayofanya wakala kwny luku alafu muishie hapo hapo.

A). 0.5% ya 100,000 ni shilingi 500, yaani wakala akiuza umeme wa luku wa 100,000 anapata shilingi 500 kuanzia leo 02/04/2018 kama mlivyotutumia ujumbe kwnye mashine za maxmalipo jana usiku kuwa kamishen ya mauzo ya luku ni 0.5 ya kile nitakachouza.
B). Kumbukeni kuwa nikiweka 100,000 kwenye mashine ya maxmalipi kutoka kwenye laini yangu ya vodacom ninatozwa ada ya shilingi 700, huu ni utatatibu wa siku nyingi ####
#NB NIKIWEKA 100,000 KWENYE MASHINE YA MAXMALIPO NINAKATWA 700, NIKIIUZA HIYO 100,000 NINAPATA FAIDA YA 500 AMBAPO NINAKUWA NIMETENGENEZA HASARA YA SH 200
(C) Pia ili wakala aweze kuuza umeme kwa kutumia mashine ya maxmalipo ni lazima anunue roller ya karatasi na roller 1 ni shilingi 2000, hapo hapo anatakiwa alipe kodi ya pango la biashara, anatakiwa ale, anywe, avae, atunze familia, ajenge kwake, anunue gari n.k

SASA HII NI KAZI AU KADHIA?
 
Hii ni changamoto kubwa kwa wafanya biashara.
 
"mlizoea pesa za bure mlikuwa nafisadi,tufanye kazi kama hufanyi kazi hutapata hela awamu hii"lilisikika jiwe likisema
 
Sijui wanaofanya mabadiliko huwaga wanafanya upembuzi yakinifu,au ndo kutiana hasara tu.
 
Hii ni changamoto kubwa kwa wafanya biashara.
Yaaani awamu hii kila mtu ataguswa kwa wakati wake,watumishi walishaguswa walikuwa bado wafanya biashara hiki ni kiama yaani niwekeze 100,000/= nipate kamisheni ya 500/= dadadeki bora nipige bodaboda
 
hiyo ni kadhia, mimi mashine hyo nishaiuza majuzi, niliyemuuzia alinipa 80% ya malipo, kanipigia leo asubuhi kuwa anataka airudishe mashine hana hela ya kumalizia, nimemwambia hiyo 20% iliyobaki nmekusamehe, nakutakia biashara njema
 
Tukisema Magufuli ana demoralize biashara CCM Na mazuzu wengine wakabisha. Sasa mambo yako bayana
Kwani maxcom ni ya serikali? Au umevurugwa ndio maana unachangia ndivyo sivyo. Waulize maxcom kwani yeye ashushe kamisheni wakati wengine bado kamisheni ni nzuri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…