Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums Maxence Melo akiwa East Africa Radio asubuhi hii, 30 Agosti, 2022.
===
Amesema kuwa JamiiForums imeandaa muswada wa mfano ambao imeupeleka Serikalini pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria ili kutoa mapendekezo ya nini kifanyike katika kuhakikisha kuwa taarifa binafsi za watu pamoja na faragha zao zinalindwa.
Pamoja na mambo mengine, muswada huu unatoa mwongozo wa taarifa gani zikusanywe, zitatumikaje, zikusanywe kwa kiasi gani, mwisho wa matumizi ya taarifa hizo ni lini pamoja na uwepo wa chombo huru kitakacho simamia zoezi hili.
Ametolea mfano wa uwepo wa taarifa za watu mitaani kwenye makaratasi ya kufungia mandazi pamoja na kutumiwa jumbe mbalimbali za waganga wa kienyeji kwenye line za simu. Hii inatokana na uwepo wa udhaifu mkubwa katika ulinzi wa taarifa za watu kwenye makampuni ya simu pamoja na taasisi zilizo pewa mamlaka ya kukusanya tarifa hizi.
"Ili kuheshimu utu wa mtu ni vyema kuwa na sheria inayodhibiti utoaji wa taarifa za watanzania nje ya mipaka ya Tanzania. Sheria kuu ya nchi ni katiba, ambayo nasema katiba ya nchi inalinda taarifa za mtu. Hadi sasa hakuna sheria rasmi ya kulinda taarifa binafsi lakini nchi Jirani zote zina sheria ya kulinda taarifa za watu binafsi"
"Muswada ambao tumependekeza kuwa na chombo huru kinachosimama kuhusu usalama wa taarifa za watu. Tunajua baadhi ya watendaji wa serikali ni wachakataji wa taarifa za watu. UN imeelekeza mataifa wanachama kuwa na chombo huru, hali ambayo imechukuliwa na baadhi ya nchi na ndio sababu ya baadhi ya kamampuni kama Google na Facebook mmesikia zikitozwa faini"
Kuhusu takwimu za watumiaji wa vifaa vya kidigitali, hadi mwishoni mwa mwaka jana kulikuwa na vifaa vya digitali bilioni 16, lakini kufikia mwaka 2030 kutakuwa na vifaa bilioni Zaidi ya 200. Kilio chetu sio kupiga kelele tu ni kutaka kuheshimiwa kwa utu wa mtanzania.
Kutokuwa na sheria kunakuwa na urahisi wa watu kuchukua taarifa zetu na kuzitumia watakavyo nje ya mipaka ya nchi.
Amesema kuwa muswada wa awali uliotengenezwa na Jamii Forums ulikuwa umelenga Tanganyika, Wazanzibari wakaona wametengwa hivyo walifanya marejeo jumuishi yaliyohusisha upande huu wa pili wa muungano. Aidha, muswada huu ulikusanya pia maoni ya taasisi za dini, hospitali kubwa nchini pamoja na wadau wengine.
Kwa kuwa Mh. Rais ametaka uwepo wa sheria ya ulinzi wa data yapo matumaini makubwa kuwa muswada huu utazingatiwa.
Miongoni mwa faida zitakazopatikana kutokana na uwepo wa Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi na faragha ni kuwapa nguvu wananchi wanaopata madhila hayo kuziwajibisha kisheria kampuni na taasisi husika ili ikithibitika waweze kulipwa fidia kutokana na usumbufu wanaopata.