Maxence Melo: Nilipoteza marafiki wengi, tuna Sheria mbovu ya Makosa ya Mtandao. Tuna haki ya kuhoji

Bishanga naye ishu yake ilikuja kwisha nadhani.

Ila kawa mpole sana.

Tunakushukuru sana Max kwa kulinda taaarifa zetu.

Ili tusije ngolewa kucha zetu mzee.

Thanks again na kazi njema hapo JF.
 
@
Viva Maxence Melo , Viva JamiiForums
 
yani mambo ya ajabu kabisa, eti unamuamini Rais..
una uwakika gani kuwa atapitisha hiyo sheria....
 
Name and shame Maxence, JF ni jukwaa na uwazi na ukweli bila woga, sasa wewe unapaswa kuwa wa kwanza kuonyesha hilo. Tuambie nani alikuambia maneno hayo, hata kama ana cheo kikubwa leo haihalalishi ujinga aliokufanyia
Ni SIMONI kwa Sasa ni Mkuu wa Kamata Kamata. Kipindi hicho alikuwa Kamanda kwenye mkoa ulioongozwa na Kondakta.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Maxence Melo. Hongera sana Kiongozi, uliyopitia ni makubwa, sio rahisi kwa watu humu jukwaani kuelewa, hasa vitisho ulivyokuwa unapewa.

Mpaka sasa najiuliza courage ya uvumilivu uliipata wapi, ikizingatiwa kipindi kile wasio julikana walikuwa hawana cha kuremba.

Anyways, kwakuwa tayari umefocus kupanua mtandao wako, angalia namna ya kuongeza udhibit wa taarifa (privacy) kwa watumiaji wako.

Lakini pia naona bado kuna shida ya attachment, na hasa kwenye video zenye mb nyingi! please work on it.

Mwisho, pale kwenye jukwaa la Elimu, binafsi naona ingekuwa ndani yake kuna majukwaa madogo!
1. Jukwaa la Elimu Msingi.
2. Jukwaa la Wlimu Secondary.
3. Jukwaa la Elimu ya Juu.
4. Jukwaa la Elimu ya Ufundi.

Hii itarahisisha topic inayohusu maeneo hayo kwenda moja kwa moja katika jukwaa husika kulingana na level ya elimu husika.
 
Kaka kwanza tunakushukuru sana kwa kuendelea kutulindia faragha zetu binafsi naamini humu wapo mpaka viongozi wa serikali kiasi kwamba ukimwanika mtu kama huyo unahatarisha kazi yake either umlazimishe kuwa mrengo wa serikali na hivyo kuondoa maana ya uhuru wa mawazo. Shukrani sana Maxence Melo
 
Name and shame Maxence, JF ni jukwaa na uwazi na ukweli bila woga, sasa wewe unapaswa kuwa wa kwanza kuonyesha hilo. Tuambie nani alikuambia maneno hayo, hata kama ana cheo kikubwa leo haihalalishi ujinga aliokufanyia
Safi boss,amweke wazi
 
Hongera Sana mkuu Max ... Una msimamo japokuwa ilikugharimu lakini wameelewa na kujua kuwa hao wanaoitwa wananchi wanawaonaje!

Mungu akuzidishie neema na JF idumu daima maana ndio sehemu pekee tunayoweza kuongea walau kutema nyongo kwa mengi si siasa tu!

Naamini wengi imewafaa Sana kila mtu kwa uhitaji wake.

Na Kama haitasumbua tunaomba basi .. mtaje Yule zimwi ulosema Ana cheo..
Tumia tu I'd nyengine ..utoboe tobo mkuu..Mana wanabana kila Kona mradi tusipumue!
 
Maxence Melo leo niongee hapa hapa.

Mara kadhaa nakuona jf ukiwa na watu wa dini.

Hii ni sifa yako niliyoona wewe siyo mbaguzi wa dini, heko sana.

Swali langu kwako, unawaza kuingia kwenye dini zaidi au kwenye siasa, tuseme mbunge au kwa cheo kinginecho.


Pia nikuulize japo sijui kama utanijibu, unailinganishaje jf na fb au tweeter.

Je, unatamani jf ifikie kiwango kipi?

(picha hazihusiani sana)View attachment 2201391View attachment 2201426View attachment 2201428
 
Post No. 40

Maxence Melo Wewe ni Role Model wangu. Nasoma sana nije kuwa kama wewe au kufanya kazi pamoja nawe nakufuatilia mno hasa kule Twitter na hata Vitabu unavyosoma na watu unaokutana nao najitahidi na mimi nivisome na kukutana na hao watu.

JamiiForums ni Mtandao Mkubwa Sana Sanaa kuhusu suala la faragha (Privacy) naufananisha na Duckduckgo pamoja na Telegram.

Just-in-case unahitaji Kijana makini mwenye ujuzi wa Information Systems Management & Security, Nipo hapa.

Continue to keep up the good work. Mr. Great Thinker

Ahsante sana, Nakupenda Sana & Mungu Baba Akulinde Brother.[emoji1431][emoji56]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…