Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Melo amesema ameshirikiana na Marehemu kwa mambo mengi, pamoja na watu wengi kumtambua kama Le Mubebez yeye anamtambua kama “Sauti ya Umeme”, mwanachama wa mwanzo kabisa wa JamiiForums na mtu aliyekuwa anaamini kuwa binadamu wanapaswa kusemezana bila kuoneana haya.
Ameongeza, “lakini zaidi kulipotokea sheria mbalimbali au kanuni, William alitoa ushirikiano mkubwa na alikuwa sehemu ya kuomba marekebisho yafanyike ili space hii ya digitali iwe rafiki kwa kila mtu. Kwa mantiki hiyo, pamoja na mambo mengine yote, tumkumbuke William kama mtetezi wa Uhuru wa Kujieleza na mtetezi wa uwajibikaji nchini”