Maxence Melo: Tumkumbuke William (Lemutuz) kama Mtetezi wa Uhuru wa Kujieleza na Mtetezi wa uwajibikaji Nchini

Maxence Melo: Tumkumbuke William (Lemutuz) kama Mtetezi wa Uhuru wa Kujieleza na Mtetezi wa uwajibikaji Nchini

Nimesoma comment nyingi kuhusu marehemu. Mungu ampumzishe kwa amani. Kwamba akikuwa na attitude simple kuhusu maisha. Pengine ni kweli ila alichelewa kuwa nayo. Amefariki kwa matatizo ya moyo. Labda kama alizaliwa na hayo matatizo, ila navyojua na kudhania ni kwamba, nyuma ya tabasamu lake pana na angavu, jamaa alikuwa na maumivu mengi moyoni yaliyopelekea kumkosesha amani ya moyo. Kukosana na kina Mange si jambo dogo. Kukosana na wanawe, hadi kumdhalilisha si jambo dogo.

Haya na mengine yalimpelekea kutafuta faraja kwa general public pamoja na bebez. Kubwa ni kwamba pengine alijua hatadumu sana ndio akaanza kutafuta suluhu, hasa na familia yake. Pengine alipaswa kuomba msamaha kwa mkewe kwanza.

Hayo yameshatokea tuyachukue mazuri yake na kuishi nayo
 
Tatizo hutumii akili kujibu
Wapi nimejibu kitu wewe hamnazo? unajua matumizi ya question mark?
Wewe ni miongoni mwa walioshikiwa akili na huyo? nini kimekuwasha wakati sikukuquote wewe?
Wewe hata hizo akili za kutumia huna.
 
In a nutshell Mwendazake alikuwa mwamba Kwa kulinganusha na watu wa umri wake.
.............................
Wishing tranquility and serenity to his spirit
 
Asante sana Maxence Melo , umemtendea haki!.
P
Wakati huo huo
Wana JF,
Kwanza tuendelee kupeana pole kwa kifo cha member mwenzetu William Malecela, Le Mutuz.

Kila mtu yuko huru kumlilia kwa namna yoyote kutegemeana na alivyoguswa.

Msiba wa Regia, JF ili organize watu tukapiga sare, na wengine wetu tukachoma wese hadi kuzika kule deep interior na kuuguza some 6-Figure!.
Baada ya msiba vikafuata vikao, tukaazimia kumfanyia compilation ya michango yake JF na kumtolea kitabu!.

Japo umoja ni nguvu, lakini nimekuja kugundua, kama una wazo na unataka li materialize, just do it peke yako usishirikishe watu!.

Jana baada ya kupokea taarifa ya msiba, baada ya kumaliza kwa Membe, nilitia timu nyumbani kwa Le Mutuz, Sea View.

Nikapandisha bandiko hili Tribute to Mwana JF Mwenzetu William Malecela Le Mutuz, Alikuwa Mtu wa Watu

Nikaamua namna yangu ya kumlilia Le Mutuz, sio kumlilia machozi ya mamba, but kum celebrate kwa kutembelea mabadiliko yake yote humu JF, toka ile 2006, kwanza kwa kumshukuru kwa kuyakongolea like, kisha kumuaga kwa kuyafukua ili wengine wajue huyu mwamba alichangia nini JF.

In so doing, modes wakatafsiri kuwa nafanya spamming!, hivyo nikapigwa ban kule jukwaa la siasa!.
"You have been banned from forum "Jukwaa la Siasa" until May 20, 2023 at 4:14 PM for the following reason: SPAM"

Kuyakumbushia mabandiko ya member aliyetangulia mbele ya haki mabandiko yake ndio yanageuka spam?!.

Modes, please tuacheni tumlilie member wetu, at least hadi akiisha zikwa!. it's not a small job kusoma mabandiko yote ya mtu, ku like na kumuaga!, na kwa maoni yangu hii ndio namna nzuri ya kumtendea haki member yoyote wa jf anapokufa kwa kuibua michango yake aliyoianzisha hivyo badala ya kumlilia let's celebrate him!.

Nimefanikiwa kumuaga kwa kum celebrates mabandiko yake ya toka 2023 kurudi nyuma hadi 2007 ndipo nikapigwa stop.

Nimebakiza mwaka mmoja tuu, 2006!.

Ninachokifanya ni kitu kizuri sana kwa new comers wa JF ambao hawakumjua Le Mutuz and what he stands for.

Nawaomba mniache nimalizie!, please!.

Paskali

Tatizo hili inabidi likomeshwe kwani Hawa watoto wa Maxence kuna wakati wanakuwa kama wale Serengeti boys wa Task force wa TRA Kariakoo hawana reasoning wala vision ya kunusa kijacho.....naomba members wa JF tumsaidie Max kufanya shortlist pale panapohitajika
 
Nasoma kila comment watu mna chuki binafsi na lemutuz.

Max yeye aliongea sifa anazojizua tangu jf ilipoanzishwa na kasema ni kati ya wale watu wachache wakiokuwepo enzi hizo jf inaanzishwa.

Sasa wewe na chuki zako umejiunga 2010, 2012 , 2015 2017 etc una lipi la kumuongelea lemutuz wakati alikutangulia humu? Una lip jipya?
Chuki binafsi zinawashushia heshima.

Hata hivyo sio rahisi lemutuz apendwe na baadhi ya watu humu maana ni juzi tu alikuwa akikemea vikali tabia chafu za ushoga na usagaji na kama mashoga na wasagaji wako humu wataanzaje kumsema lemutuz mazuri?

Ista hakuna wa kukemea ushoga na usagaji il tunamshukuru lemutuz aliweza kukemea tabia chafu.

Wewe Mungu baba mlaze mahali pema mbinguni amina.
 
Tatizo hili inabidi likomeshwe kwani Hawa watoto wa Maxence kuna wakati wanakuwa kama wale Serengeti boys wa Task force wa TRA Kariakoo hawana reasoning wala vision ya kunusa kijacho.....naomba members wa JF tumsaidie Max kufanya shortlist pale panapohitajika
Andiko la mayalla lilikua na mambo gani ya ajabu mpk kupigwa ban,
Ilikua tribute tu kwa mzee wa sauti ya umeme.
Tupo pamoja humu miaka yote hiyo.
 
Back
Top Bottom