Aliyekua kocha mkuu wa Taifa Stars mbarazili Maxio Maximo amesema kwamba Frederick Mwakalebela ndio mgombea pekee anayefaa kuchaguliwa kuongoza TFF.
Maximo amesema kwamba MWAKALEBELA alifanya kazi kama Katibu mkuu enzi za Rais Leodgar Chilla Tenga na kila mtu aliona jinsi soka la Tanzania lilivyopiga hatua kipindi kile.
Maximo akaongeza kwamba Mwakalebela atatumia mbinu na mikakati ileile aliyoitumia wakati wa Tenga ili kuendeleza mpira wa miguu Tanzania.
Akamaliza kusema Mwakalebela ni mtu anayeamini katika soka la Vijana, soka la wanawake na uadilifu katika utawala.
Sent using
Jamii Forums mobile app