Mayai ni chaguo zuri, ila mwachezi Malinzi amalizie aliyoyaanza

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Uchaguzi TFF unakaribia.

Ally Mayai Tembele na Jamal Malinzi wanaonekana washindani wenye nguvu zaidi wa nafasi ya Urais.

Ila napenda turudi nyuma,twende mbele. Miaka 4 haijawahi kumtosha na haitokuja kumtosha yeyote yule kwenye nafasi ya Uraisi wa TFF kufanya jambo ambalo linaweza kupendeza sana wapenda kandanda.

Ukizingatia watanzania tupendavyo short-cut ya Maendeleo, wengi wetu tunaona hakuna kitu chochote alichofanya JEM kwa kipindi chake chote cha Miaka 4.

Najua kunawengine tumezaa chuki mioyoni mwetu kutokana na Usimba na Uyanga tu.

Ila jambo muhimu ni kuwa JEM anahitaji miaka 4 zaidi muda wake uweze kupimwa na Maendelea aliyohusika nayo.

Kuna hii dhana ambayo tumejijenge kuwa soka la bongo linaposhndwa kupiga hatua kidogo, basi wa kulaumwa ni rais wa TFF. Hivi mmeshawahi kujiuliza vilabu vyenu vya Simba na Yanga vinafanya jitihada gani kukuza soka la bongo?
Au mnatarajia TFF iandae progamu za kukuza soka vilabuni vyenu humo?

Binafsi naipongeza TFF na rais wake kwa kuonyesha njia hasa kwenye suala la kukuza soka la vijana.

Ninaamini kuna mengi mno ambayo yapo kwenye mipango ya JEM kuhusu soka la Bongo....
Licha ya kuwa na muda mchache sana wa kutimiza hayo .....nimefurahia jitihada zake za kutokata tamaa na kuwania nafasi ya Urais kwa Mara nyingine tena ili kukamilisha yale makubwa zaidi aliyo yakusudia kwa ajili ya soka la Bongo.

Sina kinyongo kabisa na mdogo wangu Ally Mayay naye namtakia kila la kheri, ila akae akijua kuwa huu si wakati wake.
Na kwamba JEM amejipanga vilivyo kumgaragaza kwenye uwanja wa Uchaguzi.

Namshauri Ally Mayay ajipange upya kwa ajili ya Uchaguzi wa mwaka 2021.

Ninauhakika kuwa wajumbe wapiga kura watahakiksha ushindi wa kishindo kwa JeM



@TeamMalinzi
 
Tatizo lake kubwa ni kukumbatia uyanga na usimba bac ila vingine yuko poa,ila kama atatumia pesa kupata kura hapo ataharibu sana.
 
Utawala wa kumalizia cku hzi nooooo apumzike kwa aman tu
 
Umejipambanua vizuri kwamba ni mshabiki wa huyo Malinzi..
Nadhani tukumbuke na haya kabla ya kukubaliana na wewe;
1.Kuhamisha ofisi ya TFF kuzipeleka alipokuwa anahisi atapiga Tshs .Hasara hapa
2.Kufukuza kocha Kim alafu kutuletea kocha wake na kumrudisha Kim kiaina..hasara hapa..
3.Wote tunakumbuka taifa starz maboresho..Hasara hapa..
4.Nani asiyejua madudu ya ligi daraja la kwanza na mlolongo wa tuhuma za rushwa.
5.Uozo wa ligi kuu..ratiba hovyohovyo
6.Soka ya vijana imebaki maandishi tu..wamejaribu kufanya bonanza wakati huu wa kuelekea uchaguzi..
7.Rais huyu hata wanaofanya naye kazi wanasema hashauriki.
8.Rais ana vyeo viwili
9.Rushwa..hasa kwenye ligi zote
10.Taifa starz viwango kila mmoja anajua tulipo.
Tunamshukuru kwa mema aliyofanya ni wakati wa kupisha watu wengine
 
Kwenye ulimwengu wa demokrasia, hakuna sababu inayoweza kuthibitika ili imfanye asiweze kuendelea na nafasi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…