Mayai yamefurika Dar es salaam, Soko hakuna wafugaji ni Msiba


Its business man, kama mtaji wako wa kupuliza unapigwa chini. Nimeenda UK kipindi flan kuna ma supermarket kama "poundland'' wanauza all products for just one pound....unakuta bidhaa mtaani ina thamani ya pound 5 lakn wao wanauza pound 1. Hii inavuta wateja wengi mno....lipo lingne linaitwa 99pence stores....tha same case. Issue ni ku deliver quality products at relative low prices to increase turnover and demand. Unaweza google ukasoma habari zao. Hlo ndio soko huria bna ....so wa TZ tujipange...hio ndio biashara. Sio ufisadi wala nn cz mwisho wa siku wa Tz wanataka vitu bora kwa bei nafuu. Daily watu wanabuni mbinu ku gain market share.
 

Nice mkuu, hili ni soko huria kina hitaji mbinu na si ujanja ujanja
 
kwa kauli hii ni sawa na kutanganza rasmi kwamba wafugaji wadogo wadogo - wakulima wadogo wadogo hatma yetu imeshafika ukingoni.

Je hii dhana ni sahihi hasa ukizingatia historia ya nchi yetu? - kwamba asiye na mtaji tumwache bila usadizi wowote ule wa kulinda product zake? hakuna mbinu za kitaifa za kumlinda mtu huyu ili ajikwamua kiuchumi?
 
Nice mkuu, hili ni soko huria kina hitaji mbinu na si ujanja ujanja

Mkuu nakuambia kitu true...hakuna biashara inayolipa hapa duniani kama biashara ya chakula. Ni kujipanga tu wenzetu wanauza mpaka viazi vya chips vimeshamenywa na ku katwakatwa, well packaged ready for frying chips on different sizez and weight. Na unakuta ni brand ya mtu na inaheshimika, Kuna kachumbari, salads, ready made meals yan makorokoro ya kila aina na watu wananunua kweli kweli. Imefanya niwaze ndio maana azam anapiga hela sanaaa. Sio lazma mtu ukaange chips mtaani ndio uwe mjasiriamali unaweza kufungua kiji kiwanda chako nyumbani unatengeneza viazi vya chips una pack fresh una supply sokoni....TRA hawakutambui wala nn. Unakuta viazi vi 3 au 4 unapata sahani ya chips nyingi tu (machinery za kufanya hyo kazi sio tatzo zipo kibao ww tu kufatilia).....sasa imagine una manufacture viazi vya saani kama 3 unapack then unauza kama 1500 au 2000....utakua unapiga hela namna gan ?? #WabongoTuamke.
 

Unajua sumtyms nahisi serikali yetu imezidi sanaaaa kudekeza wananchi...heb tembea nchi za watu uone they way wanavyo ishi na ujasiriamali ni kitu hasa ndio utaelewa. Serikali inabdi ifike wakat iseme anaeweza kufanya na afanye...asiyeweza akae pembeni apishe wengine ili mradi sheria zote zifatwe. Sioni sababu ya msingi kuzuia kitu kisifanywe na watu wanaopenda maendeleo eti kisa sabab watu flan wanaumia....Kama unaona biashara inakushinda nenda ka join au partner na mtu anayeweza kufanya. Kama unaona kuzalisha mayai kwako ni gharama kubwa kwann usimfuate yule anayeuza kwa hyo bei nafuu i.e 4500 au 5000 umuambie unataka kuwa reseller wa mayai yake then wewe upige faida yako hapo kdgo ??? If you can't beat them, Join them. (Its Simple)....huoni hapo utakua umetatua hilo tatzo in a more professional manner/way ???
 

Hakuna taifa lolote lisilolinda ajira za watu wake duniani. Ndiyo maana kuna tariffs, import duties mbalimbali siyo kwa nia ya kuongeza mapato tu bali hata kulinda wajasiriamali wa ndani kwa nia ya kukuza zaidi uchumi. Logic kubwa ni kujaribu kwa kiasi kikubwa kumiliki mlolongo wa thamani (value chain) kwa kiasi kikubwa ili kulinda ajira na kupanua uchumi kupitia backward and forward linkages. Mayai yakiingizwa kutoka Kenya ajira zimabaki Kenya, n.k. Ukiachia kila kitu kuwa huru matokeo ni haya tunayoyaona sasa hivi, vijana wote wanaamia mjini kuuza soksi na vikorokoro vinazotengezwa China na kwingineko. Tunalima, na tunachopata tiunawapelekea Wachina wazidi kujiimarisha! Hatutakiwi kuruhusu, pale inapowezekana, nchi nyingine zitengeneze mfereji wa kuvuta vyetu kwenda kwao kama kuna uwezekano wa mfereji huo kuwepo nchini ukinywesha wenye kiu wa humu ndani! Mlolongo wa thamani ukiwepo humu ndani kwa kiasi kikubwa kutafanikisha hilo.

Kuna tetesi kwamba Amadori anamwaga mayai humu nchini!!
 
sasa hapa ndipo watanzania maskini wasio na mitaji mikubwa watakapomkumbuka Mwalimu!!

Yaani tunavyoongea hapa, hayo mayai yanauzwa kama jungu kule Mbagala, jamaa wana stoo ya kufa mtu imejaa mayai - 4500/- tu beba utakavyo.

Msiba ni hasa kwa wale wamama wafugaji wadogo waliokopa kwenye vikoba, Saccos, Thinker na kwengineko wajiandae - dhamana zinakuja kuchukuliwa.

Hii ina maana kwamba mwenye kuku wa mayai idadi chini ya 500; production ya 12 trays per day avg (Mtaji chini ya 5 mil approx) tayari ameshaondoka kwenye soko hili rasmi.
 
Ubunufu,ubunifu,ubunifu....watanzania tuwe watafiti na wabunifu. Kama mayai ni mengi wafugaji mbuni miradi mingine ambayo raw material ni mayai kama utengenezaji keki,cutles,vibama nk. Pia unganeni muanze kutafuta masoko ya nje,kwani hao wa nje wamewezaje kupata masoko yetu?
 
Niwapi aiseee.. Kama ni mabibo, tabata au ubungo nayafata...

Ungepitia Gazeti la Tanzania Daima la jana Jumapili kuna habari Imeandikwa kuhusu hayo mayai...

Yanatoka Kenya yanaingizwa na kampuni kubwa iliyopo Mkuranga (Amadori nafkiri).Kwa Ufupi ni mayai mabovu...nashangaa watu wanayashabikia humu...Hayana Vibali, yanaingia kinyume na sheria.

Kuna kijana namfahamu alikuwa ananunua mayai kwa Jirani yangu kwa Jumla..akayashobokea hayo mayai..Analalamika amepiga shoti sababu mengi yalikuwa mabovu na Aliowauzia wanamdai...Bure aghali mkuu...
 

Hayo Mayai ni mabovu mkuu..Hakuna cha ubunifu..yanaingia kinyume cha taratibu bila vibali...

Nchi Ipi utapeleka bidhaa mbovu/feki zaidi ya Tanzania?
 
4500/= wap wanauz na mim nkanunue maana hku kwetu kitunda hayajashuka sn wanatugonga 7000 na 6500
 
4500/= wap wanauz na mim nkanunue maana hku kwetu kitunda hayajashuka sn wanatugonga 7000 na 6500

Niwapi aiseee.. Kama ni mabibo, tabata au ubungo nayafata...

Mbezi ya Kimara, njia ya kwenda Goba karibu na sehemu wanakopaki boda boda yapo pale kibao chaonyesha vizuri tu kama kuwa bei ni Tshs 4,000/=. Yaani ukiacha barabara ya Morogoro ni kama hatua 50 hivi za mtu mzima upande wa kushoto
 
Mbezi ya Kimara, njia ya kwenda Goba karibu na sehemu wanakopaki boda boda yapo pale kibao chaonyesha vizuri tu kama kuwa bei ni Tshs 4,000/=. Yaani ukiacha barabara ya Morogoro ni kama hatua 50 hivi za mtu mzima upande wa kushoto

Asante sana. Ngoja nifanye maarifa
 
Tatizo bidhaa zinazozalishwa bongo zote bei ziko juu kuliko same product toka nje,serikali haitoi upendeleo kwa wazalishaji wa ndani,vilevile wazalishaji wa ndani wakipewa umonopoly wanajisahau na kujiona miungu watu.
 

Mkuu inawezekana asiwe amadori, kuna kampuni nyingine ya kuku wa mayai kubwa sana ipo kijiji cha Mkiu, huwa naona mayai kibao pale Mkuranga mjini, lakini huyu naye anazalisha na kusafirisha, pia kuna kampuni nyingine iko usawa wa mwandege pale kwa ndani hivi, nayo pia inazalisha mayai.

Wafanyabiashara wa Kibongo mashaka matupu, sijui hawa watatu wa Mkuranga kama wanaweza kufanya hivi.
 
Mkuu hongera kumbe soko unalo, ukifikishiwa hayo maeneo uliyotaja waweza nunua trey ngapi!?

Minimu supply yako ni tray ngapi? Kwa sh. ngapi? Niko ubungo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…