Mayai yamefurika Dar es salaam, Soko hakuna wafugaji ni Msiba

HALI HALISI YA MSIBA WA MFUGAJI WA KUKU WA MAYAI HUU HAPA:

Mahesabu yafuatayo yanaonyesha namna Mfugaji wa kuku wa mayai anavyopata hasara /faida kwa ujio wa mayai haya yanayouzwa Tsh. 4500 kwa tray.

Tunamchukulia mfugaji mdogo mwenye kuku 500 mtaji wake hadi kuku wanaanza kutanga ni Tshs. 5,000,000.
Kuku hawa waanaanza kutaga baada ya kutunzwa kwa wiki 20 (Miezi 5)

Production: Kuku hawa 500 wakiwa na hali nzuri kiafya watamtagia tray 12 -15 max. (Hesabu ni 75% ya idadi yao)
Tutachukulia tray 12 kwa siku.

Running costs: assuming mfugaji huyu anafanya kazi zote mwenyewe, cost pekee itaenda kwenye chakula cha hawa kuku 500 ambapo kila kuku anakula grams 125. kwa hiyo jumla ya grams kwa kuku wote itakuwa 625grms. Ambazo ni kilo 62.50. (Mfuko mmoja wa kilo 50 unauzwa Tshs 38,000.
kwa hiyo jumla ya kilo 62.50 zitamgharimu mfugaji huyu jumla ya Tshs 47,500 kwa siku.

Mauzo kwa siku: Kwa bei ya sasa, sokoni tray ni Tshs 4,500 kwa shida shida - Mfugaji huyu atapata Tshs. 54,000, kwa tray zake zote 12.

Pato kwa siku :
Mfugaji huyu atapata faida ya Tshs, 54,000 - 47,500 = 6,500. (ukitoa gharama za chakula)

Madawa na Vitamins kwa siku - 2,500 (Paketi inayouzwa 8500 atatumia siku 3 approx)

Faida kwa siku 6,500 - 2,500 = 4,000/= Faida hii sijaweka nguvu kazi ya mfugaji huyu, Mlo wa mfanyakazi, sijaweka gharama ya matibabu kwa magonjwa ya kuku yatakayotokea n,k

Kwa mfano tuchukulie una kijana unamlipa Tshs 60,000 kwa mwezi ili akusaidi kazi hii - kwa siku itakuwa Tshs, 2,000. kwa hiyo faida kwa siku inakuwa 2,000/-

Pia kumbuka kuku hawa lazima warudishe mtaji wa Tshs 5,000,000 alizowekeza mfugaji huyu miezi 5 iliyopita - wengi pesa hizi wamekopa kwa jamaa zao, mabenki, saccos nk. sasa sijui pesa hizi atazirudisha kwa namna ipi, kama mtiririko wa biashara hii upo hivi.

Ni muda gani utarudisha Tshs 5million ili u-break even? (assuming kuku hawaugui na wala hawafi kwa muda wote huo)

Kwa kipato cha Tshs 60,000/- kwa mwezi, kwa mwaka ni 360,000Tshs. Je utatumia miaka mingapi kurudisha mtaji wa 5 million ????

sasa huu ni mfano hai wa mfugaji mwenye mtaji wa 5mil, je hawa wenye kuku wachache inakuwaje??

Hapa ndipo kifo kitakatifu cha huyu mfugaji mdogo mdogo kinapotimia.
 

Mkuu FUSO ..... hawa kuku ni breed gani? ... hawanywi maji
 
Last edited by a moderator:
Mkuu FUSO ..... hawa kuku ni breed gani? ... hawanywi maji
kaka maji wanakunywa ila katika hesabu zangu sikuziweka, mara nyingi watu hutumia maji yao wenyewe!! ila nimeweka vitamins za kuchanganya kwenye maji ambazo gharama zake ni 2500 kwa siku.

Sijaweka vitu vingi tu ili kukuonyesha jinsi kifo cha mfugaji huyu kinavyotimia, kwa mfano kuna pia Dawa za matibabu ya hawa kuku kwa mwezi, kuna wakati mwingine gharama kidogo za usambazaji wa hizi tray zake 12, Gharama za ushauri toka kwa daktari wa mifugo nk.
 

Hata mimi pia nimeshangazwa hawa kuku hawatahitaji umeme, na hicho chakula cha tsh 38,000 utagaji utakua wa kusuasua mno.
 
Hata mimi pia nimeshangazwa hawa kuku hawatahitaji umeme, na hicho chakula cha tsh 38,000 utagaji utakua wa kusuasua mno.
mimi nimejaribu tu kuwaweka sawa kwamba tukisema msiba tuna maana gani?

Hata hivyo kuku hawa huhitaji umeme wakiwa chini ya wiki 8 ama 12 hivi za mwanzo, baada ya hapo hawahitaji mwanga tena baada ya saa za mchana sababu wanahitaji kupumzika pia. hawa si kama wale wa nyama wanaokula masaa 24 kwa siku.

Tshs 38,000 kwa Mfuko wa kilo 50 wa chakula cha kuku ni standard kabisa - sijui mwenzetu wewe umesomea wapi utupatie hiyo formulla yako ambayo itatoa 100% production ambayo ni zaidi ya Tshs 38,000 - 40,000 ( Layers Mash).

Kumbuka kuwa mchanganuo wa chakula hiki hupatikana hapa hapa Tanzania tena kwa bei nzuri - Mahindi, Soya, Dagaa, Mifupa, Mashudu ya Pamba na Alzeti, Ngano, Pumba ni moja ya vitu vinavyochanganywa kwenye chakula hiki ambavyo vinapatikana hapa hapa tena kwa bei nafuu.

Point yangu hapa ni kwamba chakula cha 38,000 mpaka 40,000 Tshs kwa mfuko wa kilo 50 ni standard na hakina tatizo, unless upate watengenezaji wasanii kitu ambacho ni nadra sana kutokea.
 
Nipo Arusha ntachukua kwa Tsh.4000 km upo tayari ni pm
 
Jamani Watanzania tuangalie namna ya kufanya ili yauzike kwa kutoa bidhaa sio kuuza Kama mayai
 
Jamani Watanzania tuangalie namna ya kufanya ili yauzike kwa kutoa bidhaa sio kuuza Kama mayai
na pia tuangalie opportunity nyingine mbuzi, ngombe nk. Mayonnaise ambayo ni product ya mayai haitangazwi hivyo haina soko kama pruducts za maziwa kuanzia cheese, mtindi, samli nk. Hata keki tu kupika watu wazito wakati mayai cheap. Lotion au shampoo za nywele je? jamani tuachane na trays sasa khaaa
 

kwanza umesema wafugaji wetu hawajazi soko. pili umesema kuna msiba. hawawafugaji kwa nini wasiangalie wenzao wakenya wamezalishaje? halafu hayo mayai yana ubora gani? kenya yanatumika?
 
Jamani Watanzania tuangalie namna ya kufanya ili yauzike kwa kutoa bidhaa sio kuuza Kama mayai

Unachosema ni kweli mkuu.Lakini hatuwezi kuacha kuwalinda wafugaji wetu dhidi ya Ushindani wa kampuni za nje zenye mitaji...

Wapi hawafanyi hivyo? Tunasikia Wamiliki wa Viwanda vya sukari wakilalamikia Sukari ya Brazil inaua soko lao? Kwani hawana mitaji mpaka walalamike? Au nao tuwaambie wafunge viwanda? Au wafanye biashara nyingine?

Cement ni hivyohivyo...Leo ya nje ingeruhusiwa kwa ushuru mdogo Tungeipata hata kwa 7,000 ila lazima tuwalinde wazalishaji wa ndani...
 

Mama Joe kuna msemo kabla ya kufuga Ng'ombe anza na kuku...
 
Tatizo la sukari ni case tofauti mkuu kwa uzalishaji wa sukari tz ni mdogo ukilinganisha na mayai pia sukari ya tz inazalishwa kwa technologia ya zama I ambayo ni gharama
 
Mama Joe kuna msemo kabla ya kufuga Ng'ombe anza na kuku...
Nakuelewa sana mkuu nami nimo same boat najaribu kuweka option ili kusaidiana. Ni kweli serikali ilitakiwa itulinde na hata kuondoka shoprite ni vile walikuwa wakibanwa wasiingize vitu ambavyo sie tunazalisha. Upande mwingine nasi tuangalie wapi kuna fursa na kuzitumia maana tunayeumia ni sisi sio wao.
 
Hayo mayai ya kidhhungu huwa yana vunjanguvu za kiume kama hamfahamu mulezi dokta yaani toka alfajiri hadi usiku ni kazi moja tuu ya kuwatilea dawa hadi kuwa yai si tatito hilo jamani ni bora ya kiyenjeji ndo huwa na ubora wa nguvu za kiume

Nani kakwambia kuku wa kisasa wanatiliwa dawa alfajiri mpaka usiku? Dawa wanazopewa hata kuku wa kienyeji waweza kuwapa maana magonjwa yanafanana.
 
Ina maana hujui kua hayo mayai ni sumu na yana madhara makubwa tu kwa afya? Nenda Ocean road watakuambia. Acha ubishi wa kikuda

Usituambie nenda ocean road... kama ww ni muungwana tueleze madhara yake ili nasisi wengine tuepuke.
 
1. Tanzania ina watu milion 50, hayo mayai yatakosaje soko??

2. Watanzania hawana utamaduni wa kula vyakula vyenye virutubisho, kwahyo mayai kwao ni anasa.

3. Elimu kwanza juu ya umuhimu wa kula mayai mkishindwa mnaweza ku-export kwa majirani wetu njaa kama Malawi, Kenya na Zambia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…