"Maybe It's Time to Talk to Your Armed Opposition" - Ugandan Yoweri Museveni Tells Rwandan Kagame!

Mkuu Murutongore nakubaliana nawe kukwapuwa madawa ya binadamu kutoka Govt Medical Stores ni kitendo cha aibu! Sasa swali - unaweza kutueleza kwamba nchi yenu hiko immune na vices hizo tajwa? Mbona juzi juzi nilisoma somewhere kuhusu wizi wa madawa na vifaa vya Hospitalini huko huko kwenu i.e nchini RWANDA, je unaweza kuliteteaje Taifa lako kuhusu kisanga tajwa hapo juu, tatizo lako ni kwamba as far as you are concern Rwanda ni HOLLY i.e cannot do/go wrong. Kitu kingine, hivi ujui mmiliki wa gazeti la CITIZEN anatoka nchi gani? unategemea gazeti hilo linaweza kuandika habari +ve kuhusu Taifa letu muda wote? Mkuu Murutongore nakushauri tuombe uhai - niliyosema humu will come to pass muda si mrefu ujao. Narudia kusema kwamba tatizo la REGIME yenu wote mko 2 MYOPIC 'am afriad - in other words you can hardly see beyond your noses, you people don't u realise you are sitting on a Gunpowder Keg - consequently time doesn't seem to be your BEST ALLY right now - Master KABOOOOM is closing in faster than you think - you have been warned time and time again 2 amend your behaviour lakini amsikii la mtu mpo mpo tu awaiting the END. Sisi tunao wasema sema Wanyarwanda particularly (PK) tunawatakia mema ndio maana hatutaki kuwa wanafiki wakati tunaona kuna uwekano mkubwa wa kutokea mauuaji mengine makubwa zaidi katika Taifa lenu msipo kubali kukaa meza moja na wahasimu wenu mkamaliza tofauti zenu kihungwana - kwani ujui raia wanao taka mabadiriko/demokrasia ya kweli katika utawala wenu wanatoka makabila yote: Watutsi wenzenu walio uhamishoni, Wahutu nk - hivi PK on his own anafikili ana uwezo gani wa kuzuia Tsunami ambayo inafukuta karibu Duniani KOTE inamshinikiza afanye mazungumzo na mahasimu wake, lakini yeye na Regime yake yote hawataki kusikia la mtu, kama PK anaweza kumbishia rafiki na mshauri wake wa karibu i.e M7 - basi tukubali kwamba "Sikio la kufa alisikii DAWA". Mwisho labda nikuhulize kitu, Murutongore kwani wewe ni family member wa PK au lini ulitehuliwa kuwa his master's voice? Wewe kama Raia wa kawaida wa Rwanda unawezaje kujua magazeti, social networks zinazo tembelewa na Mh.Kagame - hivi inaingia akilini kwamba Mh.Kagame anaweza kuwa na account kwenye Twitter na Facebook aka-ignore kusoma jamiiforums, Mh. Kagame ana akili sana anaweza kuwa ni member wa jamiiforums kwa kutumia an alias NAME. Goodday Murutongore.
 
I doubt authenticity of this article

Was the reporter tapping kk conversation ?

Was the reporter present during the .pk inner circle meeting ?


 
RAIS MUSEVENI WA UGANDA AMSALITI RAIS KAGAME WA RWANDA NA KUMPA USHAURI ULE ULE ULIOMKOSANISHA NA RAIS KIKWETE....





.

WAKATI hatima ya kutiwa saini mkataba wa amani kati ya Serikali ya DRC na waasi waliosambaratishwa wa M23 ikiwa haijulikana, uhusiano wa maswahiba wawili wa eneo la Maziwa Makuu, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda umetikisika baada ya Museveni kumtaka mwenzake huyo azungumze na waasi.

Ni ushauri kama huo aliopewa Kagame Mei mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete ukilenga kuleta na kuimarisha amani Mashariki mwa Congo ndio ulioyumbisha uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda, kabla ya Kikwete kuifafanua na kisha kukutana na Kagame jijini Kampala, Uganda Agosti mwaka huu.


Kwa mujibu wa mtandao wa AfroAmerica Network, Museveni, baada ya kurejea kutoka kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za SADC na zile za Maziwa Makuu (IGGLR) huko Pretoria, Afrika Kusini wiki iliyopita, alimpigia simu Kagame na kumwambia: “Huenda sasa ni wakati muafaka wa kuzungumza na wapinzani wako wenye silaha.”

Chanzo cha habari cha mtandao huo kimemnukuu mmoja kati ya viongozi wa juu wa Jeshi la Rwanda (RDF), akisema Museveni alimwomba Kagame kuzungumza na waasi hao haraka kabla muda haujapita mara tu Rais huyo wa Uganda aliporejea Kampala Alhamisi iliyopita.

Mkutano wa pamoja wa wakuu wa nchi za SADC na ICGLR uliofanyika kuanzia Jumatatu wiki iliyopita chini ya uenyekiti wa marais watatu, Joyce Banda (Malawi, SADC), Museveni (Uganda, ICGLR) na wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ulitoa wito kwa M23 kuweka silaha chini. Siku mbili baadaye waasi hao wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda,walishindwa vita na kutangaza kuacha uasi.

Kagame hakuhudhuria mkutano huo, badala yake aliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Louise Mushikiwabo.

“Ni ushauri tu. Nimerejea kutoka kwenye mkutano na SADC uliojadili amani eneo la Maziwa Makuu. Bahati mbaya inaonekana kwamba karibu viongozi wote wanaamini kikwazo kikubwa cha amani ni kuwapo kwa waasi wa Kinyarwanda mashariki mwa DRC.

“Hakika suala hili linapaswa kuzungumzwa kwa njia moja au nyingine. Na viongozi hao wanaamini kwamba hili halitatatuliwa bila serikali ya Rwanda kukaa kwenye meza ya usuluhishi na wapinzani wake wenye silaha. Hata mimi ninaamini hivyo, huenda wakati umefika kwako kuzungumza nao,” alinukuliwa Museveni akimwambia Kagame katika mazungumzo ya simu yaliyodumu kwa takriban dakika 15.

Kagame alijibu: “Sitozungumza na FDLR, washiriki wa mauaji ya kimbari. Never, … , ever. Sitozungumza kamwe na wahalifu.”

Hata hivyo, inadaiwa Museveni alimkumbusha Kagame kuwa si waasi wote wa Rwanda walioko DRC ni wanachama wa FDLR au wahalifu na kwamba wapo anaoweza kuzungumza nao kwa kuanzia.

Baada ya mazungumzo hayo, Kagame aliitisha mkutano wa dharura na washauri wake wakuu na kuwaeleza walichozungumza na Museveni na kuongeza:

“Nimekuwa nikiwaambia mara kwa mara kuwa tuko peke yetu. Hata Yoweri, tuliyemwamini kama rafiki yetu na mwenzetu anatugeuka! Leo anatuambia hiki, kesho anakwenda kukutana na viongozi wengine na kutubadilikia.”

Baadaye akawataka washauri hao kuja na mpango mkakati wa nini cha kufanya wakati huu Rwanda ikizidi kutengwa na nchi za Afrika na hata za nje ya Afrika.

Mwanzoni mwa mwezi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry na mwenzake wa Uingereza walimwonya Kagame kuachana mara moja na ushiriki wake kwenye machafuko ya mashariki mwa DRC, ikiwa ni mara ya pili ndani ya mwaka mmoja kwa wakubwa hao kutoa onyo kama hilo.

Wakati hayo yakiendelea, zipo taarifa kwamba Rais Museveni amepanga kutuma ujumbe nchini kuja kuzungumzia mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaambia Watanzania kwamba Tanzania haijakiuka chochote katika makubaliano ya msingi, ila wenzetu hao ndio huenda wana ajenda yao.

Kauli ya Kikwete ilihitimisha hali ya wasiwasi wa Tanzania kujitoa EAC na iwapo ujumbe wa Uganda utakuja, itakuwa ni mwendelezo wa kilichofanywa mwishoni mwa wiki na Kenya waliomtuma Waziri wa Mambo ya Nje kuja Dar es Salaam kuweka mambo sawa.

>>>Hali nchini Kenya

Mapema wiki hii, aliyekuwa Mwanasheria wa Serikali ya Kenya, Amos Wako ambaye pia ni Seneta wa Bisia alitoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha kuwa EAC haisambaratiki, akidai kuwa watakaoumia zaidi ni Wakenya.

Wako aliyekuwa kwenye mkutano wa hadhara pamoja na Mbunge wa Budalangi, Ababu Namwumba, alisema wakati jumuiya ya awali ilipovunjika mwaka 1977, Wakenya wengi waliokuwa wakifanyakazi nje ya nchi ndio walioathirika zaidi.

“Wapo watu mashuhuri kama Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wanaokubalika ndani na nje ya nchi ambao kama Uhuru anataka wanaweza kumsaidia kuzungumza na Rais Kikwete wa Tanzania. Hatutaki jumuiya hii ivunjike, si busara hata kidogo,” alisema Wako.


-Mtanzania

 
Kagame ni mjinga sana kwakumchukulia kila atoae ushauri kwake ni msaliti. Ushauri unaweza ufanyia kazi au kuuwacha.
 
Kama Obama kaamua kuzungumza na Taribani ambao nchi imewalebo kama magaidi sembuse hao waasi!? Huyu ni rais wa ajabu sana A.mashariki. By the way Kikwete ni hero katika hili kama ambavyo amekuwa hero kwenye mgogoro wa kenya baada ya uchaguzi pia huko Mauritius n.k
 
hakuta kuwepo na peace maziwa makuu kama kagame na museveni wakiwa madarakani hata kidogo
 
Ukweli unabaki palepale, kwamba mtu anayenyeshewa mvua anapotembea mwambie kwa vyovyote kwamba kakate jani lile ujifunike na mvua. hapo unamnusuru asiathirike wala usingojee akifika kivulini ndo umwambie angejifunika na jani la mgomba kuzuia mvua isimnyee.
 
Source ya mwandishi si nzuri.
Ni maajabu kwa mwandishi kupata mazungumzo ya simu ya hao marais Museveni na Kagame.
Pia chanzo ni wanaompinga Kagame na kutaka support ya Museveni.
Museveni amekataa kuwakabidhi viongozi wa M23 kabla DRC na MONUSCO kuwacharaza makundi mengine ya FDLR na ADF-NALU.
Pomoja na nia ya kutaka kuonyesha uzuri au ubaya wa Kagame, mwandishi anatakiwa kuwa na uthibitisho wa anachokiandika.
Anjo
 
Museveni is an old fox!
He knows how to play his cards right and he has seen the writing on the wall for Kagame.

The problem with Kagame is that he is a stupid self centered leade who does not see the tommorrow of his internal politics.
My cue is he is loser and will continue losing all support from even his best friends.

The end game seems to be Kagame's ouster, one way or another.
 
Kagame hakuna kunegotiate na hao majambazi. Mbna m7 hataki kuzungumza na besigye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…