Smart codetz
JF-Expert Member
- Jan 25, 2023
- 218
- 875
Mshambuliaji wa @yangasc1935 Fiston Mayele ameushukuru uongozi wa timu hiyo pamoja na benchi la ufundi kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kudhihirisha kipaji alichokuwa nacho.
Kinara huyo wa mabao wa Yanga, amesema mafanikio aliyokuwa nayo hivi sasa yanatokana na imani ya pande hizo mbili na siku zote ataendelea kuziheshimu.
“Juzi nimeitwa timu ya taifa ya DR Congo, ni kutokana na kiwango bora nikiwa na timu yangu, naushukuru uongozi, benchi la ufundi na wachezaji wenzangu kwa kunipa ushirikiano",