Tetesi: Mayele kwenda Simba, Chama kwenda Yanga

Tetesi: Mayele kwenda Simba, Chama kwenda Yanga

Hii ni kwa mujibu wa Gamondi au Eng. Hersi ?
 
Gamondi Falsafa yake hairusu mchezaji mwenye spidi ya Kono Kono.
 
Chama hana uwezo wa kufanya majukumu ya Mudathir.

Chama anacheza nafasi ipi na Mudathir anacheza nafasi ipi? Halafu ukipata jibu nambie kati ya mimi na wewe nani Mbumbumbu.
Hapo hawezi kuelewa atabisha mpaka kesho,

Ni kweli chama mchezaji mzuri ila hawezi kufanya majukumu ya Mudathiri
 
Wananchi hatumtaki chama sisi tuna Masia wa mpira Pacome.
 
Mpira ni ajira! Mpira ni fedha! Kama Mrisho Halfan Ngassa na mapenzi yake yote yake kwa Yanga, bado alizichezea Azam na Simba!

Hivyo sioni kama kuna kosa kwa huyo Mayele kusajiliwa na Simba, au hata kwenda Azam! Na pia Chama kusajiliwa Yanga. Maana ni jambo la kawaida tu kwenye mpira.
 
Mpira ni ajira! Mpira ni fedha! Kama Mrisho Halfan Ngassa na mapenzi yake yote yake kwa Yanga, bado alizichezea Azam na Simba!

Hivyo sioni kama kuna kosa kwa huyo Mayele kusajiliwa na Simba, au hata kwenda Azam! Na pia Chama kusajiliwa Yanga. Maana ni jambo la kawaida tu kwenye mpira.
Utamuweka nani nje acheze Chama au utamtoa nani ili aingie Chama kama sub?

By the way kwa jicho la kimpira na timu yenye malengo makubwa mtu kama chama na umri wake ni ujinga kumsajili.
 
chama huu ndio msimu wake wa mwisho, na kakataa kuongeza muda. mayele naye anaomba kuvunja mkataba kule pryamid, maana yake mayele anaenda simba na chama anaenda yanga.
Hizo ni tetesi, Chama ni mchezaji mzuri ila sidhani kama Yanga inahitaji mchezaji wa aina yake. Yupo vizuri timu ikiwa ina mpinzani dhaifu, hakabi na kwenye kukaba anazidiwa hadi na Aziz Ki.

Yanga inahitaji kuongeza beki wa kati na kiungo mkabaji mzuri. Mayele na Chama wakaongeze nguvu Azam FC.
 
Chama ni mchezaji akuna wa kumfikia kwenye ligi yetu, ila kwa speed ya Yanga Chama hatoweza labda akienda huko abadilike.
Yanga ina mpira wa kasi na nguvu, hii ndio falsafa yao, Simba wanamiliki mpira, sio rahisi Chama kucheza Yanga.

Mbali na hapo, sioni mtu ambae atawekwa nje na Chama pale Yanga.
 
Hizo ni tetesi, Chama ni mchezaji mzuri ila sidhani kama Yanga inahitaji mchezaji wa aina yake. Yupo vizuri timu ikiwa ina mpinzani dhaifu, hakabi na kwenye kukaba anazidiwa hadi na Aziz Ki. Yanga inahitaji kuongeza beki wa kati na kiungo mkabaji mzuri. Mayele na Chama wakaongeze nguvu Azam FC.
Kweli mkuu, tunahitaji imarisha kiungo tena, beki wa kati na ikiwezekana hata mshambuliaji wa uhakika.
 
Kiukweli bongo hakuna vipaji kabisa.. Chama akiwa Chipolopolo huwa haanzii kwenye First Eleven. Huanzia bench na kwa dakika chache. Hata Mayele akiwa Leopards haanzii first XI
 
Back
Top Bottom