Mayele sio wa kwanza kutogusa mpira

Mayele sio wa kwanza kutogusa mpira

------------------------------------------

Kilichomtokea Fiston Mayele jana sio kigeni kwenye ulimwengu wa soka hasa ukiwa mchezaji no 9 asilia. Siku hazifanani na jana siku nzuri iligoma kuwa upande wa Fiston.

Wakati Congo wanaongoza goal 3-1.
Dakika ya 88 mwalimu alimtoa muuaji Cedric Bakambu aliyefunga goal la pili, akamuingiza Fiston Mayele. Mayele alicheza hadi dakika ya 95 mpira ulipotamatika.

Lakini tukio la kuhuzunisha ilkuwa ni yeye kutokugusa mpira kwa dakika 7 alizoshiriki mchezo. Yeye sio wa kwanza. Haya matukio ya wachezaji wakubwa kugusa mipira mara chache imewatokea wengi duniani.

February 20th 2022 kwenye mechi kati ya Crystal palace na Chelsea. Romelu Lukaku akiwa Chelsea aligusa mpira mara 7 tu kwa dakika zote 90. Dakika 45 kipindi cha kwanza aligusa mara 1 pekee.

Chelsea walishinda 1-0 mechi hii. Shukrani kwa goal la Hakim Ziyech.

Tarehe 13rd August 2022 mechi kati ya Bournemouth dhidi ya mancity. City walishinda goal 4-0. Lakini tukio lililoistua dunia ni Herling Halaand kugusa mpira mara 8 tu kwa dakika 90 alizocheza.

Hii ni mifano hai michache kati ya mingi inayopatikana kwenye maktaba za soka.

Hivyo Mayele kutogusa kabisa mpira kwa dakika 7 alizoingia jana sio kitu cha kushangaza. Ukiwa mchezaji no 9 kuna siku huduma hazifiki mara kwa mara kwako. Timu pinzani zinaziba mianya na njia zote za mipira kukufikia.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Kwani Mayele mwenyewe anasema ni kwanini hakugusa? Au kakutuma uje umlinganishe na wachezaji wenzie wakubwa akina Halaand na Lukaku?

Au aliamua makusudi kutokuugusa mpira ili aingie kwenye rekodi ya mastaa wasiogusa mpira wakiingia uwanjani kama Halaand na Lukaku?

Suala ni kwamba, kocha alimwingiza dakika za mwisho timu ikiwa ina uhakika na ushindi ili kumpatia uzoefu na michuano hiyo, sidhani kama aliingizwa ili akaweke rekodi ya kutokugusa mpira. Kama alikutuma amekutuma utueleze hayo mwambie arudi kwa kocha wake wakayapange. Au unasemaje mtani wangu Shadeeya
 
Hahahaaa. Kawaida sana hiyo Mtani hasa mtu akiingizwa dkk za majeruhi. 🤣🤣
 
Hii ndio umeandika nini sasa????
Ila akiandika mwingine ni chuki,
Pumbavu kabisa.
Nakusalimia Dula.

Naona uzi wetu umeukimbia kabisa. 😅😅 ufanye utuletee vile vichekesho vyako banaa. Hahahaaa.
 
Sidhani hata kama hii ilitakiwa iwe hoja,unless ni kufurahisha genge tu
kwa ufupi congo dakika 7 za mwisho walicheza pungufu uwanjani, walikuwa 9 uwanjani

mayele is useless, kocha asimpe tena hata dakika 1
 
Hahahaaa. Kawaida sana hiyo Mtani hasa mtu akiingizwa dkk za majeruhi. 🤣🤣
Ila mtani tusemee tu ukweli, dk saba zote kweli. Hata kama🤣🤣🤣

Ila yote kwa yote Mayele kacheza mechi moja ya AFCON qualification round🤣🤣. CV imekua japo hajagusa mpira, sawa na yule aliitwa timu ya akina Mane wa Bayern watu wakashangilia😂
 
Hahahaa. Hivi yule wa kwa kina Mane naye alipangwa kweli Mtani? 🤣🤣
 
Itakuwa wamemchukua kwa lengo la kuwachekesha. 🤣🤣🤣

Uwanjani watacheza wengine. 😀
Huyu itakuwa walitaka azoee kambi ya wakubwa kama yule aliyeingizwa uwanjani azoee dk 90 za uwanjan zinakuwaje 🤣🤣. Hizo shughuli za wakubwa, wasidhan wanacheza na akina Ruvu au Gwambina wanatusumbua kutikisa manyonyo na vichwa. 🤣🤣🤣

Wakazane wapate namba
 
Ewaaa! Ni kweli usemavyo Mtani.

Na siku zote kuitwa na kucheza ni vitu viwili tofauti. Hahahaaa.
 
Maisha haya hayatabiriki. Mayele, Aziz Ki, Diarra, Musonda wote hawajagusa mpira huko AFCON ila Peter Banda ambaye hana namba ya uhakika Simba kakiwasha huko Misri hadi kavunjika bega.
 
Kwanza dkika saba chache sana jaman mchezj anawez znguka hta dikka 18 bila kugus mpil nyie mnashangaa dkka 8 jamn
 
Back
Top Bottom