------------------------------------------
Kilichomtokea Fiston Mayele jana sio kigeni kwenye ulimwengu wa soka hasa ukiwa mchezaji no 9 asilia. Siku hazifanani na jana siku nzuri iligoma kuwa upande wa Fiston.
Wakati Congo wanaongoza goal 3-1.
Dakika ya 88 mwalimu alimtoa muuaji Cedric Bakambu aliyefunga goal la pili, akamuingiza Fiston Mayele. Mayele alicheza hadi dakika ya 95 mpira ulipotamatika.
Lakini tukio la kuhuzunisha ilkuwa ni yeye kutokugusa mpira kwa dakika 7 alizoshiriki mchezo. Yeye sio wa kwanza. Haya matukio ya wachezaji wakubwa kugusa mipira mara chache imewatokea wengi duniani.
February 20th 2022 kwenye mechi kati ya Crystal palace na Chelsea. Romelu Lukaku akiwa Chelsea aligusa mpira mara 7 tu kwa dakika zote 90. Dakika 45 kipindi cha kwanza aligusa mara 1 pekee.
Chelsea walishinda 1-0 mechi hii. Shukrani kwa goal la Hakim Ziyech.
Tarehe 13rd August 2022 mechi kati ya Bournemouth dhidi ya mancity. City walishinda goal 4-0. Lakini tukio lililoistua dunia ni Herling Halaand kugusa mpira mara 8 tu kwa dakika 90 alizocheza.
Hii ni mifano hai michache kati ya mingi inayopatikana kwenye maktaba za soka.
Hivyo Mayele kutogusa kabisa mpira kwa dakika 7 alizoingia jana sio kitu cha kushangaza. Ukiwa mchezaji no 9 kuna siku huduma hazifiki mara kwa mara kwako. Timu pinzani zinaziba mianya na njia zote za mipira kukufikia.
Sent from my Infinix X665 using
JamiiForums mobile app