Mayele: Yanga wanajali sana maslahi yao kuliko ya mchezaji, nikirudi watanipokea tu

Mayele: Yanga wanajali sana maslahi yao kuliko ya mchezaji, nikirudi watanipokea tu

Half american

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
38,283
Reaction score
97,793
Msikie mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele raia wa Congo DR ambaye kwa sasa anasakata kabumbu la kulipwa Pyramids FC ya Misri.

“Pamoja na kwamba kumekuwa na vita kubwa juu yangu kwenye mitandao ya kijamii, bado naamini kwa asilimia 100% kwamba nikirudi Yanga mashabiki watanipokea.

“Kitu ambacho nimejifunza Tanzania ni kwamba mashabiki wengi huwa wanajali maslahi yao na sio ya wachezaji.
“Kucheza misimu miwili ndani ya yanga ilikuwa ni furaha sana kwao, ila ilipofika hatua ya mimi kuondoka, watu walianza kunichukia bila sababu yoyote.

“Mbona wachezaji wengi tuu wanaenda pale na kuondoka ila mimi tuu ndo wawe na chuki kubwa na mimi!!?, kosa langu kubwa liko wapi?

“Japo kuwa naamini kabisa nikirudi napokelewa kwa sababu narudisha maslahi kwenye upande wa timu na mashabiki, ila sidhani kama wanachokifanya ni sahihi,” amesema Mshambuliaji wa zamani wa Yangasc, Fiston Mayele.

Huyu jamaa anatapatapa alishajichanganya, kwa uongozi makini wa Yanga kwasasa sidhani kama ilo analoliwaza Mayele litawezekana. Naona kama anajifariji na kujutia, Mayele bado anaipenda Yanga ila aliikosea.

Je, litakuwa jambo sahihi kwa yeye kutaka kurudi kuitumikia Yanga tena baada ya yote yaliyotokea?

images (18).jpeg
 
Kama kasema hayo basi ajiangalie Kuna namna hayuko sawa halafu mkumbushe niyonzima alichomewa jersey
Metacha alitukana mashabiki
Makambo aliondoka na wote walirudi na kupokewa hatuna gubu Wala shida
Hata Manara tulimpokea si huwa tunafurahia dk 90 Kisha tunaendelea na shida zetu
 
Nilikuwa namkubali sana ila sitamani tena awe ndani ya kikosi cha yanga.
 
Tatizo lako Mayele una mdomo sana, punguza huo mdomo unaponza kipaji kilichopo miguuni mwako.

Kwa kipindi cha hivi karibuni hakuna mchezaji aliyependwa kama wewe ila umegeuka mchezaji unayechukiwa kuliko wote, umemzidi hadi Faeisal hujiulizi kwanini?
 
Msikie mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele raia wa Congo DR ambaye kwa sasa anasakata kabumbu la kulipwa Pyramids FC ya Misri.

“Pamoja na kwamba kumekuwa na vita kubwa juu yangu kwenye mitandao ya kijamii, bado naamini kwa asilimia 100% kwamba nikirudi Yanga mashabiki watanipokea.

“Kitu ambacho nimejifunza Tanzania ni kwamba mashabiki wengi huwa wanajali maslahi yao na sio ya wachezaji.

“Kucheza misimu miwili ndani ya yanga ilikuwa ni furaha sana kwao, ila ilipofika hatua ya mimi kuondoka, watu walianza kunichukia bila sababu yoyote.

“Mbona wachezaji wengi tuu wanaenda pale na kuondoka ila mimi tuu ndo wawe na chuki kubwa na mimi!!?, kosa langu kubwa liko wapi?

“Japo kuwa naamini kabisa nikirudi napokelewa kwa sababu narudisha maslahi kwenye upande wa timu na mashabiki, ila sidhani kama wanachokifanya ni sahihi,” amesema Mshambuliaji wa zamani wa Yangasc, Fiston Mayele.

Huyu jamaa anatapatapa alishajichanganya, kwa uongozi makini wa Yanga kwasasa sidhani kama ilo analoliwaza Mayele litawezekana. Naona kama anajifariji na kujutia, Mayele bado anaipenda Yanga ila aliikosea.

Je litakuwa jambo sahihi kwa yeye kutaka kurudi kuitumikia Yanga tena baada ya yote yaliyotokea?
View attachment 3001783
WanaYanga jifunzeni kumove On mkiachwa muachike; Mbele Daima, Nyuma mwiko hamuifuati kwa Vitendo. Kila siku Mayele mayele mayele.
Kila siku Goli la Mamelodi mamelodi mmekuwa kama mataahira. Learn to move on, otherwise nyinyi ndio wagonjwa wa akili maana mnarudia vitu vile vile ppasipo sababu. Mnakera nyie pimbi mjue. Kwanza mnipe buku nikale makande hasira ziiishe basi.
 
Kama amesema kweli haya basi kumbe ana shida kumkichwa.
Wanayanga wengi tulikuwa tunamfuatilia Pyramids, na tulikuwa tunafurahi akifunga huko na kumuombea afunge tu.
Tuliamini hakuondoka kwa ubaya, tulifurahia magoli yake Pyramids utafikiri yanaiongezea points Yanga.

Wakati tunawakanda Simba 5 alijumuika nasi kufurahia. Wengi tulikuwa na imani kwamba aliondoka kwa amani

Alipoharibu ni alipotutukana na kuonesha kutokuwa na Fadhira, madai yake juu ya majini. Wengi tulitamani akanushe kwamba amenukuliwa vibaya.
 
Inaonekana mambo hayamuendei sawa kwa sasa na anaona mahali pa kumuweka sawa ni Yanga ila alishaharibu. Ana tofauti na mtu ambae anamkandia mtu anaempenda baada ya kuachana ila bado anamhitaji.
Jitu lipo kikosi cha kwanza ndio mchezaji tegemei pyramid na hayuko sawa basi wachezaji wite hawapo sawa
 
Hebu afanye mambo yake bwana.
Alivyoondoka watu tulimlilia sanaa asitupake matope! Ubaya nae ulianza rasmi baada ya kusema tumemtupia majini! Na hilo ni doa halitafutika!!! Aende Simba tu hatumtaki !!! Akileta shobo atanunuliwa akae benchi msimu mzima
 
Back
Top Bottom