GE2025 Mayeye: Kigoma Kaskazini imekuwa shamba la bibi la wachache wanaojinufaisha huku wakisahau maslahi ya wananchi wengi

GE2025 Mayeye: Kigoma Kaskazini imekuwa shamba la bibi la wachache wanaojinufaisha huku wakisahau maslahi ya wananchi wengi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia chama cha ACT Wazalendo, Kiza Mayeye, ameeleza kuwa jimbo hilo limegeuzwa kuwa “shamba la bibi” la wachache wanaojinufaisha huku wakisahau maslahi ya wananchi wengi.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge, Mayeye amesema kuwa amejitosa kugombea nafasi hiyo ili kuwatumikia wananchi wa Kigoma Kaskazini akisisitiza kuwa uongozi kwake ni wito na si njia ya kujinufaisha binafsi.

“Nimezaliwa Kigoma Kaskazini na nimekulia hapa, vijiji, kata na vitongoji vyote navifahamu. Wananchi wa Kigoma Kaskazini wanakabiliwa na changamoto nyingi hivyo nimeamua kugombea ubunge ili kushirikiana nao kuleta mabadiliko ya kweli,” amesema Mayeye

Ameongeza kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge, ataanza kampeni katika kata 16, vijiji 49 na vitongoji 280 vilivyopo Kigoma Kaskazini ili kuwahamasisha wananchi kushiriki katika mchakato wa kuleta maendeleo huku kipaumbele chake cha kwanza akisema ni kusimamia upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa jimbo hilo


 
Back
Top Bottom