Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mazao jamii ya maharage ni maharage, kunde, choroko, mbaazi, njugumawe nk. Kutokana na idadi ya wasio kula nyama duniani kuongezeka soko la mazao haya limeongezeka sana. Mazao haya hutumiwa na watu wa dini na race zote.
Licha ya mabara mengi kuwa watumiaji wazuri wa mazao haya, Afrika ya Magharibi na Kaskazini ambako kuna idadi kubwa ya Waisalmu, mwezi wa Ramadhani mazao haya ni keki ya moto.
Changamoto kubwa ni kuyaanda mazao haya katika ubora. Yasiwe na vumbi, mawe na yawe katika vifungashio bora, imara na vya kuvutia.
Kabla ya covid pandemic nilibahatika kufika Morocco, nilishangaa kuona kunde kutoka China ziko dukani. Nilikumbuka kuwa sehemu kubwa ya Morocco ni jangwa lakini pia niliwaza yaani Mchina amepata hili soko na sisi Waafrika hatulioni.
Kunde za Wachina zilifungwa katika ujazo wa nusu kilo na kilo moja. Zilikua safi na zinavutia kwakweli katika macho ya mnunuaji.