Tatizo la bongo
Sky Eclat Ni uwekezaji. Kuna uwekezaji mdogo kuanzia kwenye uzalishaji mpaka processing. Naweza kusema 60% ya wakulima wanalima chini ya vieka 5. wengi Sana eka 1-2 baaasi. Hapa Ni Lazima aforce kuweka high profit margin ili apate kitu. Ndio maana unakuta Kama huyo mchangiaji hapo juu alivyosema kuwa Kigoma wanauza 1.5 kg kwa 2500 sawa na 1,000/kg wakati DSM (ambapo Ni jiji la larger consumers wa mazao) Ni 2,000/kg.
Kwa sababu ya mtu mmoja mmoja kuzalisha kidogo kidogo gharama za kusafirisha kuunganisha mzigo zinakuwa juu sana. Ukumbuke pia wakulima hawasafishi vizuri Wala kuweka katika grades. Ukianza pia na kugrade ndipo usishangae kukuta grade 1 Ni 20% ya mzigo mzima, 60% Ni grade II. Hapa Sasa utakuta mazao ya Tanzania Yana Bei juu mno, Kama ilivyo kwenye mahindi. Mahindi ya Zambia Ni mazuri mno na Bei chini kidogo kuliko ya Tanzania. Soya ndio balaa lake bila angalau 1,200/kg mkulima anaona Bora atupe.
Suluhisho Ni Ushirika/Co-operatives societies. Kupitia ushirikani ndipo uhamasishaji wa kilimo unafanya, mazao yanaweza kukusanywa kwa Pamoja, kusafishwa inavyotakikana, kutafuta soko.
Tatizo jingine Ni wanasiasa na Serikali kuingilia kazi za Co-operative society mfano la mkuu wa wilaya ya Songwe.
Ushirika uliopo Sasa hivi umejaa wazee wasio na ubunifu, hawana soft marketing skills na hawajui hasa kazi ya Ushirika.
Now najifunza canning process, inshallah mwenyezi Mungu akijaalia in 5 years niwe nafunga njugu mawe.
Anayetaka njugu mawe kutoka Bukoba zipo karibu kukomaa, tutafutane.
View attachment 1755251