Ni msimu wa kilimo hasa kwa zao la mpunga kwa hapa nilipo. Nipo kijijini.
Kuna furaha kubwa sana kwa sisi wakulima mazao yakipanda bei sokoni! Thamani yetu na hali ya maisha inapanda sana.
Kundi ambalo lilisahaulika na kuwa kundi kwaajili ya kulisha watu mijini huku tukiumia mpaka tunaitwa wazee! Haha lakini kwa miaka hii miwili thamani yetu imeanza kuonekana mpaka tunapigiwa simu na jamaa zetu wa mjini waliulizia mvua kama zinanyesha.
Inachekesha sana mtu unaulizia mvua kuhofia mkulima kukosa mavuno hapana ni kwa yeye mtu wa Dar kuhofia bei ya mazao! Hivi hamjui kuwa mwaka jana kulikuwa na mvua kubwa sana jiulize bei ya mpunga wangu itakuwaje kwa hizi mvua za kwenye kikombe.
Issue sio mvua ila ni mkulima naye kaona thamani yake lakini pia standard ya maisha yake imepanda hii imekaa vyema sana.
Ndugu zangu wa mjini rudini kijijini mlime, leta mtaji wa hicho ukifanyacho uwekeze kwenye kilimo nenda hata Mkuranga tu hapo kalime mihogo, nazi, maembe, matunda kwa ujumla utapata kipato na chakula!
Hatutakuwa watumwa wenu wa kila siku mkae vijiweni mpige story mkirudi kijijini mtuletee mikate mtegemee kuondoka na debe la mchele thubutu.
Mwaka huu mpunga wangu tegemea kilo 5000 hutaki kausha, mpunga hauozi msisahau tunafuga bata, kuku ng’ombe nk hizo ni hela tegemea bei kuwa kubwa lakini kwa afanyaye kazi yake inayomwingizia kipato hatalalamika kuhusu chakula kupanda bei. Habari za asubuhi