Mazda CX-5: Gari yenye muonekano mzuri sana Interior na Exterior

Kama sita kuwa na hela ya kununua Fortuner Basi sitanunua Gari kabisaaa

Unaanza kidogokidogo kaka .

Unanunua gari ndogo,unajichanga unaenda tena unanunua kubwa kidogo.


Badae unanunua gari ya ndoto yako.

Wengine tunanunua gari yoyote kuokoamuda na kuepuka msongamano wa kwenye basi na daladala
 
Hamna ni mil 26-30 pamoja na kodi


Mimi naona ni chaguo zuri kwa watu wa town ukiringanisha na Harrier au kluger.

Kwa upande wa ukisasa na fuel consumption
Upo sahihi kabisa
Yaani huwa naona imekaa vizuri mno na mambo yake mengi yapo vizuri ukilinganisha na hizo ulizozitaja.
26M?
Wacha nijipigepige
 
Wakenya wenzetu wapo vizuri mno kwenye magari tofauti na Sisi wabongo ndiyo maana kilasiku tunishia kwenye IST Tu
 
Wakenya wenzetu wapo vizuri mno kwenye magari tofauti na Sisi wabongo ndiyo maana kilasiku tunishia kwenye IST Tu
Hiyo IST 16 ,17 unapata ila CX5 bila 25 kuendelea hupati na wala siyo kwamba tunaipenda sana IST tatizo ni imezidiwa parefu sana na CX5

Sent from my CPH1823 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo IST 16 ,17 unapata ila CX5 bila 25 kuendelea hupati na wala siyo kwamba tunaipenda sana IST tatizo ni imezidiwa parefu sana na CX5

Sent from my CPH1823 using JamiiForums mobile app
Upo sahihi kabisaa isipokuwa huku bongo tumelogwa na Toyota Tu.
Ukimiliki gari tofauti na Toyota unapata shida Sana kuanzia mafundi na spare parts hii ndiyo yetu Hadi tunafanana barabarani maana kila MTU anaenda kwenye IST
 

Uzuri wa za diesel ni fuel consumption na power. Tatizo lake ambalo hata hivyo kwa bongo lina tiba ya kudumu ni DPF.
Pia badili na coolant junction toka inayokuja na gari ya plastic kwenda ya bati (zinauzwa kama spare), tou are good to go.
CX 5 kama ilivyo Gari zote za miaka ya kuanzia 2010 zinataka service nzuri na clean diesel

HII GARI INAKUOA THAMANI YA HELA YAKO KULIKO gari nyingi kama vanguard, rav 4 au Honda za miaka hiyo.
Ulaji wake wa mafuta na power unaweza kupata kwa gari chache sana zisizo hybrid
 
DPF na EGR delete niliambiwa 850k. Nikasema no way. Mtu mwenyewe weekend lazima niipelekee moto gari hafu wanataka wanile hela.
 
Kuna hii mazda demio ya mwaka 2015 / 2016' naielewa saana hii basi tu yaani
Demio aka Mazda 2. Unayosema wewe ni 3rd generation. Unyama sana. Kana engine ndogo sana 1.5L kuna option ya diesel pia.


Kana unyama wake sana.

Tafuta na Axela aka Mazda 3 nako ka HB moja katamu sana. Nimekaendesha Dar to Mwanza ka diesel. Aisee. Very sport.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…