Mazda CX-5: Gari yenye muonekano mzuri sana Interior na Exterior

Kitu sijui ni passport sijui ya muda wala kudumu kwa Nairobi hadi maaskari wananifaham kikubwa niwe na Ksh 100/- ya kuwapa na sijawahi ulizwa ID wako poa sana upande wa rushwa hadi mahakamani blockers wapo kesi yako anaomba iwe yake kikubwa umtangazie fungu zuri kingine fine na vifungo nje kwao ni nje nje hasa hizi kesi ndogo ndogo
 
Mkuu. Bongo ushuru aisee. Cheki Ushuru wa CX5 2.2 ya 2017
View attachment 2767571
Usihangaike huko mm ninayo ya mwaka 2013 na ilinigharimu km sh 26.5 M nikawa jimekamilisha tangu 2019 hadi leo sijawahi kujutia ,kuna kipindi nilipata shida ya kioo cha mbele lakini nilipata kariakoo mtaa wa gerezani kwa muhindi kwa 400 k bei ya kawaida sana
 
Good. Vipi kuishi na Diesel na DPF ?
 
Sijaona hiyo changamoto hata kidogo japo huwa kuna muda inawaka naweka injector clinar ya total kwenye tank taa imazima haina usumbufu hata kidogo

Suala la DPF kwa Quality ya diesel ya bongo na kama hutembei umbali mrefu gari nadhani ni suala la muda tu. gari nyingi zenye dpf au EGR. Ningekuwa mimi ningeitoa kabla haijaanza kuzingua na turbo
Ila kwa kuwa una uzoefu nayo zaidi inawezekana ulipata gari ikiwa bado mpya au luck.
 
Umetoa madini adimu sana. Naomba unitafute dm weekend moja tukae sehemu tule nyama na Serengeti lite ukinipea madini zaidi
 
Hivi hii windshield za Hizi Mazda CX-5 huwa zinapatwa na changamoto gani hadi zinaparanganyuka nimesikia sana shida hii kwenye hizi gari.
 
Ni vituo gani vya mafuta ambavyo vinakupa guarantee ya kupata diesel fuel nzuri ambayo haina taka taka za kuichefua hii gari?
 
Sijaona hiyo changamoto hata kidogo japo huwa kuna muda inawaka naweka injector clinar ya total kwenye tank taa imazima haina usumbufu hata kidogo
Mmmmmmhmn mzee, wataka kutuambia gari yako haifanyi DPF regeneration? [emoji848]
 
Hii gari matata sana,nimeshaona kuna kila dalili Subaru Forester,Toyota Kluger na Toyota Vanguard zikafunikwa very soon...
 
Ni vituo gani vya mafuta ambavyo vinakupa guarantee ya kupata diesel fuel nzuri ambayo haina taka taka za kuichefua hii gari?

PUMA, TOTAL labda na Engen. Ila bado hao nao wanapata mafuta yenye kikubwa cha sulphur so sidhani kama wana treatment ya kiwango cha kufanana na nchi zilizoendelea. Ila yana afadhali kuliko wengine huku. Ushauri wangu kwa mtu mwenye hii gari afanye dpf delete (atoboe kabisa). Coolant junction pia atafute ya after market ya metal.
 
Hii dpf delete gharama yake kiasi gani? Na kwa DSM wapi wanafanya?
 
Hii dpf delete gharama yake kiasi gani? Na kwa DSM wapi wanafanya?

Sina hakika na gharama zake tho nasilia bei imechangamka kidogo, tegemea kitu kati ya laki 5 - 8 (sina hakika). Kuna jamaa wanaitwa amur auto electronics (insatgram) naona huwa wanajinasibu kutoa hizo hudima na nyinginezo zinazofanana na hii mifumo ya magari ya diesel. (Za petrol hazina hii kitu)
 
Hii gari matata sana,nimeshaona kuna kila dalili Subaru Forester,Toyota Kluger na Toyota Vanguard zikafunikwa very soon...
Ni nzuri ila inataka m'miliki smart kwasababu nyingi watu wanaingiza ni za Diesel na sio petroleum. Gari za Diesel za hii brand zinataka umakini na usimamizi mzuri.

Kwa wanawake na wanaume wazembe wazee wa Toyota hii gari siwashauri maana haitaki uzembe wa kitoto. Itakuja kukusumbua na pengine utatakiwa kununua engine mpya kabisa sababu ya uzembe.
 
Hii dpf delete gharama yake kiasi gani? Na kwa DSM wapi wanafanya?
Watakwambia kuanzia laki 5 huko na kupanda. Ni upigaji tu wa bei. Ila ukimuendea fundi kirafiki atatazama namna ya kukusaidia. But sikushauri uende kwa hawa mafundi uchochoroni.
 
Mmmmmmhmn mzee, wataka kutuambia gari yako haifanyi DPF regeneration? [emoji848]
Ndio nachokwambia ,na hauwezi kuambini tatizo mnaamini sana picha na VIDEO ZA UTUBE kuliko uhalisia zaidi hii gari ukijua inataka nini huwezi kuogopa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…