Mazda wamezindua 3rd generation CX-5: Ina option ya Hybrid na Hakuna buttons kwenye cockpit!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Hatimaye Mazda wamezindua 3rd gen ya SUV yake pendwa duniani, CX-5 Itakayoanzwa kuuzwa mwaka 2026.

Mazda CX-5 itakuja na option ya 2.5L engine Petrol na 2.5L Skyactiv-Z engine Hybrid itatoka kuanzia 2027 na option ya Diesel mtaendelea kusubiria.

Kwa muonekano wa nje imeongezeka ukubwa kutoka kwa 2nd gen, na pia imezidi kufanana na CX-50 na CX-70. Muonekano mwingine umebaki “almost” ule ule uliozoeleka.

Kwa ndani Mazda naona amebadirisha muonekano wa screen na kaweka mpya kubwa ya 15” na ikiwa na UI kutoka Google, kwahiyo Maps, Chrome, na App zingine za Google zitakuja moja kwa moja.

Pia, Mazda wameacha baadhi ya capacitive buttons kwenye steering wheel ila physical buttons wamezitoa. Na kama haitoshi pale mbele ya cockpit haina button ata moja. So kucontrol AC, radio, wipers, etc ni kupitia kwenye screen (kama Tesla)!

Wapenzi wa Mazda tuisubirie na hii kama vipi.

Edits:
Kutoka Mazda, bei ya kuuza (MSRP) itakua $32,000 hadi $37,000 tu.

Kwanini wameondoa buttons, wao wamesema “wateja ndio mmeomba”.
 
Hizi chuma za Mazda lazima uwe na namba ya kila fundi wa gereji

Kwa uzoefu wangu kwa Africa kama unanunua SUV za Japan ruka na TOYOTA na sio NISSAN wala MITSUBISHI au MAZDA na pacha wake ISUZU
​
 
Hizi Mazda CX-5 nashindwa kutofautisha za diesel na petrol au zenye turbo au non turbo
 
gari yangu pendwa ila sasa nasikia ina mavipengele ina maliza pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…