Mazingaombwe (Jugglery) ni Sayansi au Uchawi?

Mazingaombwe (Jugglery) ni Sayansi au Uchawi?

Salaam wakuu

Nimeangalia video nyingi Sana za hawa magicians Wazungu kwa Waafrika na nimejikuta najiuliza maswali mengi Sana kuwahusu wao na pia kila kukicha wanaibuka wapya

Unakuta mtu anatafuna viwembe vya kutosha tu alafu anatafuna na uzi alafu anashushia na maji baada ya hapo anavitoa vile viwembe vikiwa vimejipanga kwenye ule uzi [emoji15] na maajabu mengine mengi tu

Hivi wakuu hawa magicians nguvu zao zinazowawezesha kufanya magics wanazitoa wapi/wanazipataje?

Je,Kuna vyuo wanavyofundisha magics?

Au niwaongo tuu hawafanyi ukwelii kwamba wanafanya tricks?View attachment 1807346View attachment 1807347View attachment 1807348
Kuna chuo kipo India kinafundisha mambo hayo sema nimekisahau jina lake nikikumbuka takwambia
 
Kuna siku nilienda kufanya mazingaombwe kule Sumbawanga. Nilikuwa na uwezo wa kumgeuza binadamu kuwa panya kisha nikamrudisha tena na kuwa binadamu.
Basi nikaenda sokoni nikawakusanya watu, nikamgeuza jamaa kuwa panya.
Kulikuwa na mama mmoja pembeni akajigeuza na kuwa paka, kisha akammeza yule panya, na baada ya hapo akarudi kwenye umbo lake la ubinadamu.
Nilijuta kuzaliwa, sitaki kukuelezea kilichotokea baada ya hapo.
🤣 🤣 🤣 🤣
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji23] we jamaa kumbe hz pigo zako umezianza kitambo eeeh[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],

BTW naona ID nyng zilizo comment kwny huu uzi zimepotea sana vp wamestaafu kutumia JF au?!
 
kuna vitu huwa ni ujanja na wepesi wa matendo, lakin kuna criss angel huwa sielewi ni nguvu ya ki magic au ni ujanja ujanja, alikuta watu wanaogelea akawaambia 7 kila mmoja achukue karatasi na markpen afikirie herufi yoyote moja na aindike, akawaambia wajipange kwa mstari wakaonyesha zile karatasi, wote walikamilisha neno BELIEVE kwa zile herufi. wewe acha tu
He can influence your decision. They use magic powers.
 
Tayari umeshajibu. Ni ujanja ujanja tu.
Ujanja ujanja na wakati nakumbuka nilishika panga lilinolewa vizur kwa mkono wangu nikaambia nimpige mwanafunz la kichwa lakin la kushangaza sikupata kesi yoyote maana dogo alikua akiongea huku stanless steel alikua akitembea nayo
 
Hapana sio uchawi mkuu....ni sayansi. Naijeria kuna chuo kinafundisha hii mambo
Kuna mpaka ambao unatenganisha kwa beginner utaambiwa ni tricks, but magic is more than tricks. Hata ukiomba ufundishwe utafundishwa tricks za kawaida. Huwezi kufundishwa kuingia ndani ya tv au kumtoa nje mtu aliyepo kwenye tv na kisha ukamrudisha, au mtu akufunike na turubai hapa halafu akifunua within a second haupo kabisa au upo upande mwingine. Hii inaitwa teleportation kama sikosei.

Magician ni kweli wanatumia tricks ambazo ni sleight of hands to perform their illusion kitu ambacho hata wewe ukifundishwa kama una mikono miepesi unaweza, but sometimes they use super natural powers from demons ambacho baadhi ya magician hata walipoulizwa kama wana magic powers, walisema ndio.

Issy Simpson ni mwana mazingaombwe ambaye kwa sasa ana miaka 14 na alianza akiwa na miaka 7. Kwa mdomo wake alisema roll model wake ni babu yake, akaulizwa je babu yake ni mchawi akasema YES.
 
hii thread nimeisoma mwanzo mpaka mwisho nacomment hapa,
kuna watu jf ni story teller na hadithi za kujua kwingi kumbe hamna kitu mfano nicholax alianza kunishawishi huenda ningejifunza kitu kuhusu mazingaombwe yanayoonekana ni complex kama ya dynamo.

mwisho wa siku hata mfano wa magic trick moja aliyosisitizwa aelekeze akazuga kama haoni comment akalala mbele ,

mara mbeleni akaja rakims ,nicholax akavuta pumzi akijua rakims ataokoa jahazi so akawa anamkomalia rakims atoe mfano na uelekezaji wa magical tricks
hahahaaah mmeni discourage mno kama mtu hujui ni mara mia uchangie kikawaida kuliko kuwatoa imani watu walianza kuwaamini

btw mimi naamini kuna tricks(mbinu za kawaida) kwenye mazingaombae na pia kuna mazingaombwe yanayotumia uchawi
Wamekimbia [emoji23]
 
Kuna mpaka ambao unatenganisha kwa beginner utaambiwa ni tricks, but magic is more than tricks. Hata ukiomba ufundishwe utafundishwa tricks za kawaida. Huwezi kufundishwa kuingia ndani ya tv au kumtoa nje mtu aliyepo kwenye tv na kisha ukamrudisha, au mtu akufunike na turubai hapa halafu akifunua within a second haupo kabisa au upo upande mwingine. Hii inaitwa teleportation kama sikosei.

Magician ni kweli wanatumia tricks ambazo ni sleight of hands to perform their illusion kitu ambacho hata wewe ukifundishwa kama una mikono miepesi unaweza, but sometimes they use super natural powers from demons ambacho baadhi ya magician hata walipoulizwa kama wana magic powers, walisema ndio.

Issy Simpson ni mwana mazingaombwe ambaye kwa sasa ana miaka 14 na alianza akiwa na miaka 7. Kwa mdomo wake alisema roll model wake ni babu yake, akaulizwa je babu yake ni mchawi akasema YES.
Umeeleza vizuri kuhusu mazingaombwe (magic) na kiini macho (illusion) lakini kwamba wanatumia nguvu za giza ni uongo. Hakuna magic trick au illusion ambayo haina maelezo ya jinsi ya kufanya. Tatizo linakuja kwamba ili uweze kufanya hivyo vitu ni lazima uwe na special skills kama sleight of hands, cold reading, power of suggestion n.k na ndio maana sio kila mtu anaweza kufanya. Suala la uchawi au demons hakuna.
 
buche buche puuu
buche buche puu

sheby mwanaprofesa anakuja na uchawi wa dunia, buche buche pu.

Afu mwingine alikuwa anasema. . .

Slowly slowly, please give me 2X

Onyo: mkisoma haya maneno, mnapoteza sehemu zinazowatambulisha kama huyu ni Juma au Asha.
ooh baada tu ya kumaliza kusoma mstari wa mwisho imebidi nijishike mbele kwangu nione kama jamaa yupo au ndo kashapotea,maana wachawi sio watu wazuri! siku moja nilipita sehemu nikawakuta hawa watu wa mazingaombwe sasa wakat tunaendelea kuangalia karatasi zinabadilishwa kuwa saa akatokea mlevi mmoja kaanza kuwatukana wale jamaa na kuwaita matapeli tu,wakamuita apite mbele akaenda,chini kulikuwa na begi kuukuu ndani kama vile kuna mnyama ana manyoya mengi wakamwambia aingize mikono humo kwenye begi ili ajue kama wao ni wa kweli au waongo.
Mlevi yule si akaingiza mikono huku anatamba kuwa "hamuwezi kunifanya lolote" akaambiwa atoe mikono na ajiangalie kama uume wake upo jamaa alipojiangalia akakuta kumekuwa flat yaani hakuna kabisa kikojoleo cha aina yoyote..alilia sana akawaomba msamaha,wakampga fine na wakamuweka mpka walipomaliza shughli zao wakamrudishia kikojoleo chake..ndio maana na mimi nikashtuka.
 
Ahahhahahaah wengine walikua waongo sana ! niliwahi kuhusika na mchezo mchafu alikuja Mwanamazingaombwe simkumbuki jina , akaomba vijana watatu wajanja , nami nikala shavu ! kumbe anaenda kutufundisha uwongo wake.

Mimi alinifundisha akipuliza dawa yake nijidai sioni amenipofusha kwa dawa zake !

Mwisho wa siku nikapewa Tsh. 20
Tsh.20😂😂
 
Member wa zamani mmepata umaarufu kwa uongo uongo kama hivi

Ndio maana siku zote nasema Mshana Jr ni mjanja mjanja tu wala hakuna anachofahamu, nakumbuka alikamata hadhira kwa vistori vya uchawi mpaka leo ndio umaarufu wake lakini nachojua si mchawi, mganga wala hajui mambo hayo
Hahahahaha
 
Back
Top Bottom