Iyerdoy
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,755
- 1,939
Mkuu; wewe ni mdadisi sana. Kongole. Unataka uitumie kujipatia maokoto? Nimesema hapo juu PM siji naweka hapa-hapa hadharani ujinga/ujanja unaotumika:Toa hiyo elimu kuhusu namna unavyoweza kusoma majina yaliyokunjwa kwenye karatasi au kama haupo willing kuiweka public nicheki PM. Mana nipo interested walau kujua baadhi ya tricks.
Napenda kujifunza vitu vipya kila siku.
1. Ni lazima/Sharti (Muhimu sana hii) awepo mmoja kati yenu msiyemjua/kumdhania ninafahamiana naye awe naye ameandika na ataandika kitu tutakachokuwa tumekubaliana kabla ya onesho. Huyu ni msiri wangu.
Mimi nitakapofika hapo mlipo na mkiwa tayari mmeshaandika mliyo yaandika na kuzikunja karatasi; nitachukua karatasi lolote miongoni mwa makaratasi yenu mliyokunja-kunja. Nitasoma kwa sauti kwa kuliweka kisogoni kwangu bila hata ya kulikunjua kile msiri wangu alichoandika. Naye atanyosha mkono kukubali kwamba ameandika yy. Then nitalifungua na kulisoma kiukweli. Tahadhari; Hakuna mtu kukaa nyuma yangu-manake siri itabumbuluka. Kuanzia hapo nitakuwa nasoma kile nilichokisoma kwenye karatasi la kwanzaalilokubali msiri wangu. Kamchezo hako ka kijinga kataendelea vivyo hivyo mpaka namaliza karatasi zote.
Siri inabaki kati yangu mimi na Msiri wangu. Aaamen.
na bado anaendelea kuongea kwa mbwembwe zote na maonesho yake.