Mazingira gani ambayo ulipoteza / kuibiwa simu, ambayo hutoyasahau?

Mazingira gani ambayo ulipoteza / kuibiwa simu, ambayo hutoyasahau?

Raj kapool

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2018
Posts
1,352
Reaction score
2,160
Mimi niliibiwa k7 nilinunua mpyaaa baada ya kula mkeka natoka zangu kazini kwenda stand hapo Mohamedy Mwanza ile kunyanyua tu mguu kuingia kwenye gari nakutana na jamaa nae anashuka nilivyompisha tu kujisachi simu sina nikacheka kwanza

Nageuka jamaa simwoni kila ninaemuuliza anasema kapita hapa loooh
Niliumiaga sana hiyo simu niliisaka hadi kituo cha kati na mpaka leo huyo jamaa bado namtafuta

Nikarudi tena kubet ukapita mwezi nikala nikaenda tena kununua kama ile ile kasoro rangi
Natoka zangu job tena saa 3 usiku nikakosa magari kipindi hicho nimehamia Ilemela kwa hiyo nikaamua nitembee mdogo mdogo nafika
Tu maeneo ya Nera jamaa kanikaba kwa nyuma anaingiza mkono achukue simu jamani jamani

Kwanza nilikusanya hasira za ile ya mwanzo nikaunganisha na hii kiukweli wale jamaa hawatanisahau maana niliwafua vya kutosha mpaka nikiwaita njoni mchukue hii hapa wanakimbia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kuibiwa ila jamaa yangu, tupo ofisini then staff mwenzetu halafu mdada bonge la sistaduu akapita nayo mezani!

Alikomaa mpaka mwisho licha ya camera kumuonyesha akipeleka mkono eneo lilipokuwa na simu na kuichomeka kwenye nguo!

Alijua kamera ilipo akajiposition isionyeshe exactly anachokifanya!

Jamaa yangu ilimuuma mno! Hakulala siku kadhaa mawazo coz hakuwa anaamini aliyefanya hilo tukio!
 
Nishaibiwa mara 2 chuo ,

1) 2nd year hiyo tulikua room hostel floor ya 4 tena, niliweka alarm niwahi kuamka afu simu nikaiacha charge, naona alarm haiiti hadi nimeamka mwenyewe dah, kucheki nilipokua nimeweka charge naona charger inabembea tu simu haipo kuulizia members nao wanashangaa tu, nilishangaa mlango haujafunguliwa so inaonesha huyo mwizi alipitia dirishani floor ya 4 aisee.

2) 3rd year hiyo nawahi lecture ya asubuhi, tumegombania shuttle wee, tumeingia hao hadi chuo, nimefika sasa niangalie simu kwa pochi haipo yaani ,kupiga ikaita ila haijapokelewa mara ya 3 ikazimwa kabisa na haikupatikana tena. Walinirudisha nyuma sana boom langu niliplan kusave,ikabidi ninunue simu nyingine fyuu zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitasahau nilikabwa na wahuni wa Tandika tena saa nane mchana, halafu Ilikuwa stand wanaume 5 mwanamke peke yangu [emoji4].

Nilijitahid sana kupambana lakini haikuwa bahati yangu walifanikiwa kuchukua simu ila cover nilibaki nalo na pochi nilibaki nayo......sitakuja kusahau. Watu wamezunguka wanashangaa kama wanaangalia movie vile baada ya kutoa msaada.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Waliingia usiku wakapita na simu mbili, maoja yangu moja ya mshkaji, na laptop moja. Mshkaji ambaye naye simu yake iliibiwa alishikws na tumbo la kuhara kwa mshtuko. Nilicheka sana aisee japo na mimi niliibiwa. Kuanzia siku hiyo hadi leo bado sijanunua smartphone.
 
Back
Top Bottom