[emoji17]huu mwaka umenikaribisha kwa nuksi saaana[emoji17]
Kuna mtt wa geti kali yaani mda tu akitoka kwao basi ni lazma atoke na mama yake au mdingi.Hapati chance kabisa ya kutoka alone,Pale kwao kuna mti wa Kungu siku moja nikaona mlango wa geti dogo upo wazi vile na sisi tulikuwa tukiishi majirani,mara mama akatoka nje na kuniita akiniomba nipande juu ya mti nikamchumie kungu,bila. Ya kusita nikafanya hivyo,huo ndio ukawa mchezo wangu mara kwa mara nazama ndani kwao napiga story na mtt nikisikia sauti kaali ya kuitwa bint yao fasta nakwea juu ya mti nakujifanya naangua kungu.
Siku ya sherehe ya mwaka mpya sasa mida ya saa2 usiku watu wakijiandaa kuupokea mwaka,mimi huku nampanga mtt tukwee nae juu ya mti,huku mdingi wake akiwa anakula ulabu ndani sittingroom kwao na mama mtu akirekebisha msosi,
Huku na huko nikafanikisha kumpandisha bint wa wawatu juu ya mti,,ile tunaanza tu kupeana mambo,sijui ikawaje katika kushika tawi kumbe akawa amelishika tawi na Kinyonga,gjafla tu akaanza kupiga kelelee “Mamaaa nakufaaa Nyokaaa”,!!!!
Mara akaruka hadi chini[emoji17]
Na vile giza juu ya mti nilijua. Kweli ni nyoka na mimi nikashuka faaaastaaa kufika kumuinua pembeni namwoma kinyonga
Nliskia saut ya mdingi tu ikisema askariii fungulia mbwa hakikisha huyo mtu asitoke
Kibaya zaidi suruali nimeiacha juu ya mti najikuta na boxer tu[emoji17]
Baada ya kuisikia kauli ya yule mzee,nilipita na mlinzi alliokuwa getini akijiandaa kunikamata...Mmhhh namshkuru mungu tu hapo hapakua na ujanja ila kudra za mungu tu ndio zilijaalia
Manake hata sikumbuki nlipitajepitaje pale getini[emoji17]
Tangia huo msala utokee alfajiri nikajivuta standi hadi wa leo sijarudi home,ila tetesi nlizozipata kuwa mtt wa kike alisafirishwa kwa bibi yao Moshi
Kila nikiikumbukia hii ishu naona huu mwaka wa 2018 kwangu umeanza na mkosi[emoji17]