Inaonekana hapa nabishana na watoto waliozaliwa Kinondoni, kila kitu wamemalizia hapo hapo Kinondoni na kazi ukapata wilaya hiyo hiyo ya Kinondoni! Huelewi!
Unachofanya kugugu na kuleta facts za gulugulu ambazo nyingi hazirelate na uhalisia wa huku kwetu!
Huo ni wastani wa mwanadamu kutembea mwendo wa kawaida na inawezekana walichukua kipimo cha mtoto wa mama wa pale New York, wenzio huku bongo hatua moja anakukatia mita moja na nusu na speed anayopiga mtoto wa mama unaishia kumfuata kwa kukimbia! Hilo hujaona? Endelea kugugu hesabu zako [emoji23][emoji23][emoji23]
Vitu vingine usipende kuhadithiwa! Fanya kitu kinaitwa roadtrip! Nenda rural huko mbali kabisa na wenzako mnakaa siku tatu week mnajifunza mambo mbalimbali na mtajikuta mnarudi mmebwaga moyo na kujifunza yale yasiyowezekana kumbe yanawezekana!
Sasa niwape story halisi: Nilifika kijiji kinaitwa Mikumbi kata ya Chilangala (we si unajua kutumia gugu, angalia km zake hadi Ndanda mi nilipima kwa gari two times) nilitaka nichukue boda shs 20,000 ili nikalale Ndanda kwenye lodge ili niamke na basi la saa kumi na mbili to DSM, wenyeji wakaniambia utaondoka na wafanyabiashara saa tisa alfajiri na utawahi basi unalotaka fresh tuu, nikasema bora hii 20,000 ya boda na 30,000 ya lodge imepona (kumbuka nilikuwa na gari ila pale kileji hapakuwa driver wa kunipeleka na kulirudisha na sikuwa na sehemu salama pakuliweka hapo Ndanda kwa week mbili). Mbona nilijuta!
Kwanza, mwanamke kabeba tenga la maana la mihogo, wakaniambia wewe na hili begi lako utatutechelewesha weka juu tenga temebea mbele!
Maanina! kumi na mbili kasoro 20 nipo stand Ndanda, nililala kwenye basi kama naumwa na nafika jijini naumwa kweli kweli!
Watu wanapiga hatua na mzigo wa kubeba hilux kichwani!