Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 376
Ni jukumu la kila mwajiri kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wake. Mazingira ya kazi ni lazima yawe mazuri na salama kwaajili ya kufanikisha utendaji mzuri wa kazi.
Hii itasaidia kuondoa hatari ya watu kuumia au kupata ulemavu wakiwa kazini au kusaidia watu wenye ulemavu kufanya kazi pasipo na kuwa katika hatari ya kupata maumivu au kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi vizuri.
Mwajiri anatakiwa kutoa eneo la kazi pamoja na vifaa vya kazi. Mazingira ya eneo la kazi ni lazima yawe mazuri na salama kwa waajiriwa wenye ulemavu.
Mwajiri anatakiwa kuwalinda watu wenye ulemavu dhidi ya vitendo vya ukandamizwaji, unyanyapaa na vitendo viovu vya aina yoyote dhidi ya watu wenye ulemavu.
Mwajiri anatakiwa kuhaikikisha kwamba watu wenye ulemavu wanapata haki zao za msingi zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.
Mwajiri atakiwi kumwachisha mtu kazi kwasababu tu amepata ulemavu bali anatakiwa kuhakikisha watu waliopata ulemavu wakiwa kazini wanarejeshwa na wanaruhusiwa kuendelea na kazi.
Hivyo, kama mtu amepata ulemavu akiwa kazini, kwamfano amepata ajali basi mwajiri anatakiwa kuhakikisha mtu huyo anarejea kazini kuendelea na kazi.
(rejea kusoma kifungu cha 34 cha sheria a watu wenye ulemavu ya mwaka 2010)
NB:
Kama ikitokea kutokana na sababu za kitabibu mtu huyo hawezi kufanya tena kazi ile ni vyema basi akabadilishiwa majukumu lakini sio kufukuzwa kazi.
Ni muhimu kwa waajiri kujali na kuthamini wafanyakazi wao na ni muhimu pia kwa waajiriwa kujali na kuthamini kazi zao na kutekeleza majukumu yao ya kazi kwa ufasaha. Waajiri na waajiriwa wanategemeana katika kufanikisha maendeleo ya kazi husika. Hivyo utu na upendo ni lazima utawale kati yao. AHSANTE.
Imeandaliwa na:
Mr. George Francis
0713736006
Join us
Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓
Facebook: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓No. I