Mazishi kwa kuchoma moto mwili wa marehemu( cremation)

Warumi zamani (kwa mujibu wa vitabu na movies) walikuwa wakichoma moto maiti. Unaweza kuelezea ni imani gani?

Wao hawakuwa wakitanguliza kichwa wala miguu. Wanaiweka maiti kwenye kichanja halafu zinajazwa kuni mfano wa kilima kidogo ndipo moto unawashwa.
 
Hao ni Warumi
 

Biblia inakataa kabisa falsafa yote unayoielezea.

Mwili ukichomwa hauiokoi roho wala kuifanya iwe huru

“Wafu hawajui lolote… wala hawana sehemu tena katika mambo yafanyikayo chini ya jua.” — Mhubiri 9:5–6

Roho haiendi kuzunguka, wala kuingia hatua nyingine kwa kuchomwa au kuzikwa. Huo ni uongo wa kipagani, si Biblia.

Hakuna reincarnation katika Biblia “Imewekwa kwa wanadamu kufa mara moja, kisha hukumu.” — Waebrania 9:27

Hakuna rebirth, hakuna realms, hakuna kurudi tena duniani.. Kifo ni mwisho, si daraja la mizunguko.

Mwili hauamui hatima ya roho

“Msihofu hao wauao mwili lakini wasioua roho.” — Mathayo 10:28

Moto, tanuru, mwelekeo wa kichwa au miguu havina mamlaka juu ya roho.

Biblia inakataa ibada zinazohusisha maiti na falsafa za miungu

“Msijifananishe na mataifa.”
— Walawi 18:3

Haya yote unayoyasimulia ni desturi za mataifa, si imani ya Biblia.

Unachokiita “maarifa” ni mchanganyiko wa ibada za kipagani, hadithi na falsafa, lakini Biblia yako inavivunja vyote: Hakuna reincarnation, , Hakuna roho kuachiliwa kwa moto wala Hakuna maana ya kichwa au miguu

Biblia haisaidii simulizi lako — inalikanusha moja kwa moja.
 
Nina mtu wangu wa karibu ameisha tutangazia kuwa mwisho wa uhai wake atataka mwili wake uchomwe. Kupitia mada hii naomba unijuze utaratibu wa kufuatwa ikiwemo gharama zake.
Natanguliza shukrani. 🙏
 
Ndiyo maana mkuu Mshana Jr unapenda maandamano na vurugu sana. Una roho ngumu. Mimi siwezi hata nikasogea mahali mwili wa binadamu unachomwa moto
 
With all due respect, umeelezea/ kuchambua imani ya watu wengine kwa kutumia imani yako. Siyo kila mtu hapa Duniani anaamini Biblia kama wewe unavyo amini.
Itoshe kila mtu aamini anacho amini
 
Ardhi ikija kuwa shida watu watachomwa tu.
 
Kuna mto unaitwa Styx ambao warumi waliamini roho ya marehemu huvuka ili kwenda afterlife.

Ili roho ya marehemu ivuke mto, ilibidi maiti ichomwe na mabaki yawekwe kwenye chombo maalum.
 
Umesoma kwa makini na kuelewa nilichoandika lakini? Maana umeandika as if nimezungumzia kea mtazamo wa Kikristo na Biblia takatifu.. Soma tena hiki kifungu hapa👇🏿👇🏿👇🏿
Japo kwasasa inachukuliwa kama njia ya kuokoa nafasi lakini haya ni mazishi ya kimapokeo na kiimani kwenye hizi dini zinazoabudu miungu
 
Nina mtu wangu wa karibu ameisha tutangazia kuwa mwisho wa uhai wake atataka mwili wake uchomwe. Kupitia mada hii naomba unijuze utaratibu wa kufuatwa ikiwemo gharama zake.
Natanguliza shukrani. 🙏
Kuna kampuni za mazishi pale Muhimbili naweza kukupatia contact zao wakakupa makisio.. Huyu wa kwetu ilikuwa around USD 1500 foreigner
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…